My fairy tale story | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

My fairy tale story

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Bronty, Dec 21, 2011.

 1. Bronty

  Bronty Member

  #1
  Dec 21, 2011
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 60
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nimekaa ofisini mara kaja kijana mtanashati kufatilia ishu zake, kanipiga jicho na mie nikarudishia la aibu lakini akaondoka, nafika home kila nikijigeuza namwazia yeye, baada ya siku tatu anakuja ofisini, hajanikuta akaacha kitu kwa mwenzangu narudi lunch napewa kufungua nakuta pipi na chocolate, bila namba, kesho yake kaja tena kaishia reception, kamwachia receptionist ujumbe anisalimie, nikaanza kupoteza mawazo

  Baada ya wiki nakutana nae mlimani city kanialika samakisamaki sijajiuliza mara mbili tukala, tukapeana contact kesho yake hakupiga , inayofata nikamrukia,ilikuwa ijumaa kaniita happy hour mahala, yaani namwangalia kwa mahaba nishampenda tayari kabla hata hajasema, ananiangalia naona kanielewa. tukatoka tumeongozana mpaka kwake

  Mahaba niliyopewa hapo sipati kukwambia, sikutaka kuweka pozi wala nini coz nilijua namuhitaji sana na kama mbwai na iwe mbwai,wiki nzima ilikuwa ni mahaba tu jamani, nikaona kama naishi angani peke yangu na mpenzi wangu, nikapumua nikajua baada ya muda mreeeefu wa kusubiri hatimaye Mungu kanishushia lulu, baada ya wiki mbili kaniita dinner ananiambia anasafiri kusoma nje ya nchi atakaa huko mwaka na nusu.....nililia sana jamani nikajiona sina bahati sababu kilichonitokea ni Love at the first site, yaani ni muda mfupi but i was sure its him, just him for the rest of my life.....

  Baada ya wiki kaondoka,now im happy to tell you anarudi baada ya kumngojea muda wote huo, process zote walifanya wazee wake tunakuja funga ndoa, napenda kuwaambia wasichana wenzangu wajue kusoma mioyo yao coz siku ya kwanza tu nilipomwona mapigo yalicheza
  ya moyo na nilijua ndio yeye tu, anarudi mahbuba wangu sijui itakuwaje nitakapompokea Mungu anisaidie iwe perfect.......thats my story...maoni na ushauri unakaribishwa, im excited hapa naandika machozi yananitoka.....

  Nawakilisha
   
 2. m

  mzabzab JF-Expert Member

  #2
  Dec 21, 2011
  Joined: Aug 18, 2011
  Messages: 6,981
  Likes Received: 585
  Trophy Points: 280
  mhm mie utakuja niambia baada ya mwaka mabo niaje......
   
 3. Maganga Mkweli

  Maganga Mkweli JF-Expert Member

  #3
  Dec 21, 2011
  Joined: Jul 14, 2009
  Messages: 2,096
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Mpango Mzima???? Olewa sasa, sawa?
   
 4. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #4
  Dec 21, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,550
  Likes Received: 81,990
  Trophy Points: 280
  Hongera zako na kila la heri katika ndoa yako.

   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 5. Bronty

  Bronty Member

  #5
  Dec 21, 2011
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 60
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hahahah la leo lisingoje kesho mzab
   
 6. Mwali

  Mwali JF-Expert Member

  #6
  Dec 21, 2011
  Joined: Nov 9, 2011
  Messages: 7,032
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Hongera Bronty... tumefurahi kuskia kuna ambao wanapata penzi la dhati...
   
 7. Bronty

  Bronty Member

  #7
  Dec 21, 2011
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 60
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hahahahah thanks BAK im telling you this is not getho love, its real
  muda wote yuko away, hakuna siku hajacommunicate, na a lote
  of romantic staff aishhh ahsante yesu
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 8. m

  mzabzab JF-Expert Member

  #8
  Dec 21, 2011
  Joined: Aug 18, 2011
  Messages: 6,981
  Likes Received: 585
  Trophy Points: 280
  ah mie nsea hivyo maana hapa wenzio kila leo wanakuja lia kuwa wapenzi wao wa mbali wamecheat....leo mwengine alilamba utamu na wifi yake...ghafla kawa lesbian.....sasa wewe sijui utakuja sema nini baada ya mwaka
   
 9. Mmasi

  Mmasi Senior Member

  #9
  Dec 21, 2011
  Joined: Oct 26, 2011
  Messages: 164
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Mnafunga ndoa huku mnajuana nini sasa hicho?
   
 10. m

  mamama Member

  #10
  Dec 21, 2011
  Joined: Oct 29, 2011
  Messages: 24
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hahaaaaaaa........kumbe mapenzi ya dhati bado yapogo????
   
 11. Maganga Mkweli

  Maganga Mkweli JF-Expert Member

  #11
  Dec 21, 2011
  Joined: Jul 14, 2009
  Messages: 2,096
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  hii statementii imenifurahisha,daah baada ya tafakari ya kina nimeuhuzunika sana kumbe wengi ni wahanga wamapenzi
   
 12. Bronty

  Bronty Member

  #12
  Dec 21, 2011
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 60
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  unajua nini, tujifunze kusema pia tunapopata good moment sio kulalama tu, wakati wa kulalama ukifika unalalama, wa furaha just share na watu pia thanks mzab
   
 13. Maganga Mkweli

  Maganga Mkweli JF-Expert Member

  #13
  Dec 21, 2011
  Joined: Jul 14, 2009
  Messages: 2,096
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  ile kitu ni tamu kuliko mvinyo mkuu so kuionja ndio mpango mzimaaaaa
   
 14. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #14
  Dec 21, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,550
  Likes Received: 81,990
  Trophy Points: 280

  Huo ni wimbo tu banaaaa :):) Goodluck and all the best
   
 15. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #15
  Dec 21, 2011
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,606
  Likes Received: 6,182
  Trophy Points: 280
  Ngoma mmepima?
   
 16. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #16
  Dec 21, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,550
  Likes Received: 81,990
  Trophy Points: 280
  Shukrani sana kwa hili.


   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 17. Evarm

  Evarm JF-Expert Member

  #17
  Dec 21, 2011
  Joined: Aug 30, 2010
  Messages: 1,499
  Likes Received: 186
  Trophy Points: 160
  Nakuonea raha!!! Mungu awe nanyi katika ndoa yenu, ijae furaha, upendo na amani tele.
   
 18. Bronty

  Bronty Member

  #18
  Dec 21, 2011
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 60
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ili uhuzunike lazima ufurahi kwanza kwa hiyo ni maisha tu, sio kwamba hatujapitia huko au haitakuja kuwa lakini kwa sasa acha nifurahi
   
 19. Bronty

  Bronty Member

  #19
  Dec 21, 2011
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 60
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  BAK naomba niwekee one moment in time wa whitney houston
   
 20. Maganga Mkweli

  Maganga Mkweli JF-Expert Member

  #20
  Dec 21, 2011
  Joined: Jul 14, 2009
  Messages: 2,096
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  enjoy dada ndio maisha hayo
   
Loading...