Hi wana jamii forums
Niseme tu it's an honor kupata jukwaa kama hili la kushare life experience.
Kipindi chote nasoma chuo,jijini dizim nilipanga toka niko first year kuwa nikimaliza tu,I will go back to where I came from.
So baada ya kukabidhi kitabu changu (dissertation )nilifunga mabegi yangu tayari kwa safari. Mizigo iliyokuwa mikubwa nilipeleka kwa mama yangu mdogo aishiye Tabata;tukakaa, tukapika tukala then nikamweleza azma yangu ya kurudi nyumbani.Nakumbuka aliniuliza mbona mapema sana?Nilimjibu nisipoondoka sasa ;sintaondoka wacha nende,isitoshe bibi na babu wamenimisi sana nami nimewamisi,wacha nikawasalimu then ntarudi.Ilikuwa Ijumaa.
Nilikuwa nshakata tiketi kabisa ya basi,alfajiri na mapema nikafika ubungo nikapanda basi kwenda kaskazini. Nikiri mimi si wa kaskazini ila maisha yalifanya wazee wangu wakafika kaskazini na kujenga mji.Saa 12 jion nilikuwa kaskazini.Nikapokelewa kwa furaha na bashasha na ndugu na majirani.
Mwezi mmoja baadae nilikuwa busy kila nikiamka nazunguka kwenye maofisi mjini pale nikipeleka cv na kuomba kazi.Wakati huo huo kuna ofisi moja ya kanda nikaenda kuomba kujitolea kwa mambo nilosomea. Mama yule ,Mungu ambariki sana alinambia sawa naweza jitolea ila hana fungu la kunilipa chochote.Nikamwambia mama usijali uzuri natokea nyumbani,haina shida nahitaji kujifunza kazi tu.Walinirusuhu nifanye asubuhi hadi saa 6 mchana then wakawa wananiruhusu nirudi nyumbani.Basi ikawa baada ya saa 6 naenda shinda stendi nikiangalia kama kuna fursa gani nifanye.kila mara nilikuwa najiambia sikusoma nitaabike stendi huku,this is not my place.But nilikuwa nakaa pale stendi toka 6 mchana hadi 12 jioni then narudi nyumbani.
Baada ya mwezi sehemu nilizopeleka barua wakaniita walihitaji mtaalamu,kwa mshahara wa laki 5,jijini Arusha nikakubali.kwani sikuwa na jinsi. Nikaenda nikafanya kazi kama miezi 3,then wakawa na project mwanza wakanipeleka,wakanilipia chakula ,hotel,malazi na mshahara wangu wa mwezi.Nakumbuka nilikaa mwanza miezi 3.Mungu huyu,nilipiga hela sana,si wajua tena mwanza kina ngosha wahana hiana. Nilinenepa hataree.
Project ilipoisha nikarud arusha,nimekaa kama mwezi utumishi wakaita watu kwenye interview,nilikuemo,nikafika na kufanya usaili.Mwaka ulofuata nikaingia serikalini rasmi,yes private kulikuwa na hela sema job security ilikuwa ndogo. But nawashukuru coz they got me wakati sina mbele wala nyuma.
So for any graduate out there usikate tamaa. Saa yako yaja.It's just the matter of time.haimaanishi maisha tumeyapatia,no but tunapata mkate wa kulisha family na siku zinasonga.Jipe moyo.
Sent using
Jamii Forums mobile app