Wadau,
Kwa kuanza tu niseme nimefanya mapenzi yasiyo salama na wanawake wengi sana na mnamo mwaka 2006 nilikutana na mmoja wa ma-ex wangu ambaye tulikuwa hatujaonana kwa kadri ya mwaka mmoja hivi...huyu ex alikuwa mwenye hali mbaya kiafya akiwa na dalili zote za ''Gonjwa hili''.Nilipata wakati mgumu sana kimawazo kwani nilijua kuwa nimeshaambukizwa ukizingatia kwamba tulikuwa tunakulana peku peku halafu sana tu.
Hali hiyo ilinifanya kukata tamaa na tangu hapo nilikuwa mvivu sana wa kutumia Condom na nilikuwa na hofu kubwa ya kwenda kupima hivyo zaidi ya aslimia 80 ya wanawake niliokutana nao baada kipindi hicho nilikwenda peku peku huku nikisubiri siku yangu ifike.Nilikuwa mtu nayechukia sana stori zozote zinazohusiana na UKIMWI kwa hio nilishajihisi ni mmoja wa waathirika...nakumbuka nilikosa ajira moja kisa tu niliambiwa moja ya masharti ni kupima UKIMWI.Hili suala lilinifanya hata nisifikirie kuingia katika maisha ya ndoa licha ya kuwa na umri mkubwa tu sasa.
Hivi karibuni nilimpata mwanamke ambaye nastahili kumwita mwanamke wa shoka hasa...huyu tumekuwa marafiki kwa kadri miezi sita na muda wote huu amekuwa akiniambia ananipenda pia ila papuchi akawa mgumu sana kuitoa kwa masharti ya kwamba yeye si mpenzi wa Condom na kama ninahitaji papuchi basi twende hospitali tukapime ndipo anipe mzigo.Kwa masharti hayo nilikuwa tayari kumwacha aende zake hasa nikizingatia historia yangu isiyopendeza.Nilianza kumkwepa kukutana naye na mara nyingi alikuwa akinipigia simu na kuniita mtoto wa kiume coz kaniambia tupime mi nikakimbia.Nakumbuka siku moja nilivaa ujasiri tukaenda mpaka TMJ hospital tukiwa naye akaomba kuwa tupime then tupewe majibu tukiwa pamoja...nilitoka nje kama naenda kupokea simu nikatimka mbaya then nikampigia kuwa kuna dharura nyumbani.
Baada ya hapo akawa mchokozi sana na kuanza kuniambia kila asubuhi kuwa vipi umeshatumia dozi tayari akimaanisha ARV na hapo nilikosa raha sana ukizingatia na historia yangu.Leo nimeamua kupiga moyo konde nikaenda mwenyewe Agha Khan nikajisalimisha na kuamua kama noma na iwe noma...na nikaomba nipimwe kwa Elisa kabisa.Nilienda kwa mshauri kwa ajili ya counselling na hata sikumbuki alikuwa anaongea vitu gani kwani akili yangu haikuwa hapo kabisaa.Niliambiwa nisubiri kwa nusu saa baada ya kutoka maabara ambayo kwangu ilikuwa ni kama mwaka mzima hasa nikiangalia viruka njia niliopita nao peku peku...dah kufikia mida ya saa saba hivi nikaitwa na daktari na baada ya kuingia sikumwona kama ni mtu mchangamfu sana kitu kilicho nifanya nijue nimeshaharibu.
Daktari akaniambia kuwa damu yako iko negative....nimeruka humo ofisini kwake kama mwenda wazimu vile nikatoka mbio kwenda AAR kupima tena kama vipimo viko vile vile nikapewa jibu hilo hilo yaani hapa naandika bado natoa machozi maana siamini kilichotokea.Niko na huyu mtu hapa Sanitas tunaenda kupima niko na full confidence nikikuta tu hana leo hii hii namla.