My all time favourite games | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

My all time favourite games

Discussion in 'Tech, Gadgets & Science Forum' started by Endangered, Oct 31, 2012.

 1. Endangered

  Endangered JF-Expert Member

  #1
  Oct 31, 2012
  Joined: Sep 22, 2011
  Messages: 929
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  wakuu hali, kuna anayeumwa? Pole.

  ok, then mi mzima, let us proceed.

  below ni msururu wa all time favourite games ambazo sitakaa nichoke kuzicheza. (hizi sio lifetime games - tofauti na kombolela, kula mbakishie baba ..anda anda stop nk) these are tv/pc. Unaweza ongezea za kwako pia ili tujikumbushie kuanzia enzi.


  1. Super Mario.
  kuanzia mlio wake mpaka steji ya mwisho kumuokoa Princess, siwezi isahau hii game, ndio iliyokuwa basically ya kwanza kucheza (achilia mbali brick game enzi hizo 1500 roho inauma niliponunua 97-98s) family game kitambo hicho. ukichoka Mario unaingia duck hunt au tank, au gunman.
  [​IMG]
  [​IMG]

  kuna watoto wengine hawamjui Mario wa zamani, wao wamekuta na wa new millenium.

  2. Galaga

  [​IMG]
  Kama ni spaceship ndo nimeanza kuzijua kutokea hapa. hii game mpaka kesho nitaicheza tu. no wonder hata kwenye avengers (the film) kuna jamaa alikuwa anacheza badala ya kufanya kazi inayompeleka chooni. Zaidi ni pale ndege yako inapotekwa, na ukaikomboa afu zije kuungana hapo chini, utaipenda hiyo 'duet.'

  3. Mappy


  [​IMG]
  Japo utaona ni kama kamdudu kanarukaruka kwenye kamba, (huyu ni panya polisi anayewakamata wezi) ninaipenda hii puzzle, kasoundtrack kake ka kusikitisha kimtindo, nawe unapoiga mahesabu ya kuwakwepa maadui ili uvuke stage. napendelea zaidi bonus stage yake, maputo kila kona, kazi kwako.

  Playstation One era.

  4. C-12 Final Resistance


  [​IMG]
  Jamaa nilikuwa namuona mgumu until nilipokutana na "the way of the gods". Ila kwa PSOne, hii game ilikuwa nzuri, wamejiotahidi kwa kiasi chao na missions za kukimbizana na midege. I just like the guy, mpaka naimaliza sikujuta. Pia website yake kipindi hicho cha 2002 ilikuwa imetengenezwa kweli, so interactive..

  5. Gran Turismo
  [​IMG]
  Kwa PSOne, I really liked the way ninavyotune na kcheza more races huku nikishinda na kuongeza magari garage. It is cool. No wonder wakasema 'the real driving simulator'.

  6. Tekken 3
  [​IMG]
  The King of Iron Fist Tournament ndo inayozungumziwa hapa, nikikamata dualshock yangu na kukuchagulia Bryan Fury - hata uwe nani hutoki, nakumaliza. Next to him is Hwoarang,. utantaka!

  7. FIfa 2000

  [​IMG]

  Sidhani kama kuna mtu anaichukia starting sequence ya fifa, wachezaji wa zamani wanatokea, oopposite kuna jamaa wa kisasa na mpira. game on! huku mziki ukipigwa nyuma yake by Robbie Williams (baby it's allright it's only us) Ninaipenda hii, probably labda kwasababu ndo ya kwanza kwanza kuicheza, sidhani kama ntaichoka anyway. Kwa waliozaliwa 2001 wanaweza kuitazama video hapa

  Okay, sasa tuingie Playstation 2 era.

  8. Need for Speed: Most Wanted

  [​IMG]
  Hapa hunitoi hata kwa mapapai :)
  I like kuanzia trailer, mpaka credit titles.
  Namkubali Sergeant Cross, yuko fiti vibaya mno. sema nimemzidi kidogo ndo maana nikamaliza. hata stroyline kwangu imekaa vizuri, na hao blacklist unavyowakata sasa (gia za M3 zote zako.). lazima utawakubali tu EA Games. chezea Electronic Arts! NB: I happen to like it most, of all the NFS so far.

  9. Black

  [​IMG]
  Hapa sasa action games were redefined. EA Games kwa mara nyingine utawapenda tu.
  graphics (noma), sound (ndo usiseme).
  sijui nikuelezee nni kuhusu hii game. itafute tu angalau hata youtube videos uione.

  10. god of war II


  Kwa mtu ambaye hajaicheza hii game, nahisi amekosa nutrients muhimu. KRATOS, not only a bad ass, but pia namuona kwamba sio mtu mzuri (baada ya kumcheza kwenye 3) revenge is just like breakfast to him. hapa anamqusetion babaake.

  "...is this the best you can do father, you send a broken mortal, to defeat me? the god of war?"
  yaani hapo inaonesha ni mbaya kiasi gani kumdharau. tuma jeshi kamili, sio watu wa hovyo hovyo.

  despite kwamba nimeiainisha II, ila pia III can come in here, nimeshangazwa na jinsi alivyomuua Poseidon. the point of view ni balaa, no wonder SCEA wametumia at least 6 weeks kumdevelop character mmoja tu. (afu yeye anawaua in a minute, teh teh.) tofauti na a few hours za gow2.

  Kwa jinsi ninavyomkubali, sitakuwekea screen shot yoyote. we mtafute tu, kuanzia David Jaffe (director wa series ya kwanza) to Cory Barlog GoW2, to Stig Asmussen wa 3. I like the team, sound, animators, combat designers na kila kitu about the game. (though sadly ile ya David Jaffe sijaicheza.)

  11. Command and Conquer (C&C)

  [​IMG]
  Kwa real time strategy fans, hapana shaka mmeshacheza series kadhaa za hii game.
  this include the classic C&C Red Alert (PC, PS One), C&C Red Alert 2, C&C Red Alert 2 Yuri's Revenge expansion pack, C&C Red Alert 3 (PC/Mac) C&C Generals, C&C Generals Zero hour, nk.

  [​IMG]
  this game takes up to 3 hours ukiwa unacheza/pigana vita moja tu (hapo ni kama uko vizuri, vinginevyo ushatunguliwa zamani). What i like ni reality ya vitu, all the equipment used are basically adapted from real war, achili mbali zile za sci-fi, including mind manipulating and the chronosphere. But ukiicheza hii game, then ukaenda kambi ya jeshi, hautakuwa mgeni, maana utakuwa unajua features ya devices unazoonyeshwa.
  [​IMG]
  to make it even better, unaweza tafuta mods zake online, ukaenhance unavyotaka (at your own risk kama unataka kugombana na Mama yako kwa sababu utasahau kula)

  [​IMG].  12. Second Sight
  [​IMG]
  Kwa walioichez hii game, (mind manipulation inahusika) the guy travel places kurekeb isha situation ilivyotukia, na pia akiwa na uwezo wa kucheza na mind ya adui. hence unaingia ndani ya adui na unajirusha ghorofani. (suicide suceeded)
  from guns to lifting objects with your mind. I love this PS2 game.

  13. Splinter Cell (SC)

  [​IMG]
  Last but not least, kuna SC series, zake Tom Clancy
  ziko nyingi nyingi, ikla ninayoikubali most ni hii Conviction. Niliicheza kwenye nokia(s60v3), niakona nitafura ya PC. iko vizuri. You can try it, along the list pia kuna SC-PT (Pandora Tomorrow), SC-CT (Chaos Theory), SC-DA (Double Agent) nk

  So, this is it. the doors and windows are open kwa list yako.
   
 2. UncleUber

  UncleUber JF-Expert Member

  #2
  Oct 31, 2012
  Joined: Apr 25, 2011
  Messages: 4,945
  Likes Received: 100
  Trophy Points: 145
  enzi za 8bit games nilikuwa mpenzi wa supermario, dangerous dave,

  enzi za magemu makubwa nilikuwa mshabiki wa mortal kombat, nfs,

  sasa hivi ni fifa13, gta, nfs
   
 3. Chief-Mkwawa

  Chief-Mkwawa Platinum Member

  #3
  Oct 31, 2012
  Joined: May 25, 2011
  Messages: 17,810
  Likes Received: 7,133
  Trophy Points: 280
  haha mimi fifa 1998 kuna kina clement kahabuka, golini mwameja,mbele thomas masamaki. Sjui hata kama hawa wachezaji wanajua kama wapo kwenye game.

  Anyway mimi all time favourite game yangi ni fire emblem kuanzia nes, kuja snes, kuja gameboy kwenda nintedo ds hadi gamecube mwisho nintendo wii nimelicheza fire emblem
   
 4. Mad Max

  Mad Max JF-Expert Member

  #4
  Oct 31, 2012
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 3,434
  Likes Received: 422
  Trophy Points: 180
  Super Mario nilikua nacheza kwa watu. Dah, game video tunatumia cartridge flani hivi na pad za nyaya
   
 5. Endangered

  Endangered JF-Expert Member

  #5
  Nov 1, 2012
  Joined: Sep 22, 2011
  Messages: 929
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  haha, umenikumbusha hiyo dave, kuna mwenzake pia prince of persia.
   
 6. Endangered

  Endangered JF-Expert Member

  #6
  Nov 1, 2012
  Joined: Sep 22, 2011
  Messages: 929
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Kweli mkuu, na kuna njemba zilikuwa nyeusi si mchezo. I wonder saivi hamna kitu kama hicho. Naona we ni mzee wa Nintendo kwa sana tu.
   
 7. elmagnifico

  elmagnifico JF-Expert Member

  #7
  Nov 1, 2012
  Joined: Jul 7, 2011
  Messages: 7,913
  Likes Received: 7,458
  Trophy Points: 280
  A call for duty, Assasin creed, NFS
   
Loading...