My 2008 greetings to jf | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

My 2008 greetings to jf

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Calnde, Dec 18, 2008.

 1. Calnde

  Calnde JF-Expert Member

  #1
  Dec 18, 2008
  Joined: Oct 7, 2008
  Messages: 1,373
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Ni katika JF,japo nimejiunga muda mfupi,nimetambua watanzania si wajinga tena.Ubora na umakini wa mijadala hapa unaonesha wazi kuna kitu kinatokea Tz na katika historia ya mabadiliko hayaJF ni namba moja.Jf imekuwa tishio kwa watawala wasiopenda kuhoji na kimbilio kwa wananchi wanaotaka kuhoji na kufahamu.Tukumbuke wapo waliokuwa na kazi ya kusema visivyoeleweka.Waacheni waseme, ni haki yao.Hata kasuku anaweza kusema ila tuu kama utamtajia maneno japo atakuwa hajui anasema nini. Ubora wa hoja za hapa ni elimu tosha kwa mtanzania anayetaka kuelimika na ni tishio kwa wanopenda u-imla wasiotaka mabadiliko.
  Ombi langu:
  Ikiwa unapata nafasi ya kusema kwa ajili ya nchi yako sema.Maana ni wewe peke yako unayeweza kusema.Wengine ni kina mama wanaofia hospitali kwa huduma mbovu,mabinti wanaobakwa kwa sababu ni yatima, machinga wanaosumbuliwa na mgambo, wafungwa waliosingiziwa, watanzania wanaoibiwa ndani ya nchi yao,walimu wanaonyanyaswa malipo yao, wazee wanaonmyimwa mafao yao, wanafunzi wanaofukuzwa vyuoni,na wajane walionyang'anywa mali.Ni kama samaki wanaotamani kusema lakini wana maji vinywani! Sisi tulio na access japo ya kusema neno tuseme kwa ajili yao maana kati ya kumi, mawili yanaweza tekelezwa,who knows.Jamii yetu inawategemea wenye upeo watengeneze njia,ndio sisi,tusiwaangushe hawa! Tunapouaga mwaka huu tutambue hata kama mchango wetu hauonekani wazi ni dhahiri hata mkuu wa kaya anatambua kazi hii njema.Mods,kwa namna yeyote boresheni zaidi kwa mwaka ujao ili tuendelee kuwa chachu ya mabadiliko ya kweli na tusikate tama.Wakina Monsesquieu,Rousseau,Marxist scholars,Martin Luther Jr walipofanya kama sisi hawakuwa na malengo ya kuwekwa kwenye historia ya waleta maendeleo.Leo tunawakumbuka.Nasi siku moja,japo kama kundi,tutakumbukwa.Walipo wengine walioendelea,tunaweza kufika.tutaweza tuu kama tuna nia na nia yakweli huanza na mtu anavyofikiri.JF tunaongoza.

  MARRY XMASS AND HAPPY NEW YEAR
   
Loading...