Mkuu kilichotokea hapa kina maelezo. Bajeti ya upandishwaji madaraja hufanyika wakati wa PE mwezi Novemba, wakati bajeti inafanyika wewe bado ulikuwa ni Mwalimu Daraja la 3 ndio maana hata barua yako ya promotion imekutoa hapo kukupeleka daraja la pili.
Ila bado ofisi ya Mkurugenzi na ofisi ya TSD hazikwepi lawama kwa kutopitia tena taarifa zao kabla ya kuidhinisha upandaji wa madaraja.
Kwa case yako na kwa mujibu wa waraka wa ubadilishaji kazi/cheo {RECATEGORIZATION} kwa walimu uliotolewa 1/12/2009 wewe unahesabika kama A.E.Msaidizi kuanzia hiyo January 2011 ulipopewa barua ya recategorization, hvyo umehama kabisa kada uliyokuwepo na kuhamia nyingine na unatakiwa uanze na mshahara wa kuingilia yaan entry point ambao ni TGTS C, hata kama ulipokuwa Mwalimu Grade A, ungepanda mpaka kufikia E bado ungeanza na mshahara huo wa C, ila ungeendelea kupata mshahara wa E kama mshahara binafsi kwa kuwa bado upo kwenye ualimu. Na unastahili kupanda utakapotoka mwongozo wa kupandisha walimu walioajiriwa 2011, kubadilishiwa kazi/cheo au kupanda mara ya mwisho 2011 minimum 3yrs 2come.
Remember that hata kama ule mshahara wa Grade A, ungekuwa umefika E, baada ya hyo miaka 3 utapewa D.
Hao waliopanda na kupewa D baada ya kupata Diploma, kama walibadilishiwa kazi/cheo 2008 kurudi nyuma ni sahihi, otherwise ni makosa yamefanyika na ofisi ya Mwajiri au TSD walioidhinisha promotion hizo.