Mwongozo wa utumishi wa umma

Ndebile

JF-Expert Member
Sep 14, 2011
7,242
9,802
WanaJF nisaidie sheria za kazi zinasemaje kuhusu mtumishi wa umma anayeenda kusomea kada tofauti na ile aliyoajiriwa nayo?

Mf. niliajiliwa kama mwalimu nina miaka 8 kazini na nimejiendeleza kwenye evening class nikafikia vigezo vya kusomea Udaktari MD,mwajiri yaani serikari atanilipia masomo?mshahara wangu wa ualimu nitaendelea kupata wakati ninasoma?nikimaliza masomo nitaomba kuajiliwa upya au nitaamishwa tu kwenda department nyingine?

Naomba msaada japo kidogo tu, nawasilisha.
 
SG8

JF-Expert Member
Dec 12, 2009
3,931
2,039
Kwa Muijibu wa waraka Na. 11 wa Mwaka 2002 baada ya kuijiendeleza kuna kitu kinaitwa RECATEGORIZATION (Kubadilishwa kazi/Cheo) hii inahusu watu walioiendelza fani za awali na waliobadilisha fani.

Kwa kuwa wewe umebadilisha fani ngoza nijikite huko. Kama unasoma huku unafanya kazi i.e kwa evening au umeenda kampus kwa kufuata taratibu za ruhusa hapa mshahara wako utaendelea ku flow ila kama ulitoroka mshahara utasimamishwa na utafunguliwa mashtaka (utalipwa nusus mshahara mpaka utakapokutwa na hatia ya utoro wa siku 5).

Baada ya kuhitimu kuna namna mbili> Ya kwanza toa taarifa kwa Mwajiri wako kuwa umehitmu na kupeleka academeic transcript. Kakam kuna nafasi kwa fani husika atakubadilishia majukumu au kazi kwenda kwenye fani husika kama ni daktari unaweza kupelekwa kwenye hospitali ya Wilaya husika (japo sina hakika kama zinamilikiwa na Halmashauri au Wizara ya Afya).

Namna ya pili ni kuomba kazi nyingine ukipata fuata taratibu pitisha maombi kwa mwajiri wako ukifuzu usaili na kuajiriwa utaondoka na haki zako zote ulizokuwa nazo kwenye Ualimu.

Kila la heri
 
Mwakalinga Bujo

JF-Expert Member
Oct 22, 2008
2,720
1,438
Maelezo mazuri .Alama nyekundu ni kukuwekea msisitizo kuwa hospital za wilaya zipo chini ya wakurugenzi wa Manispaa/ Halmashauri
Ya kwanza toa taarifa kwa Mwajiri wako kuwa umehitmu na kupeleka academeic transcript. Kakam kuna nafasi kwa fani husika atakubadilishia majukumu au kazi kwenda kwenye fani husika kama ni daktari unaweza kupelekwa kwenye hospitali ya Wilaya husika (japo sina hakika kama zinamilikiwa na Halmashauri au Wizara ya Afya).
 
MPUMBWI

Member
Sep 11, 2011
28
4
HALLO GERRADI NAKUSHUKURU KWA KUMPA MWONGOZO NDEBILE MUNGU AKUBARIKI.

NA MIMI NINATATIZO KAMA LA NDEBILE NILILIAJIIIWA MWAKA 2006 NA MWAKA 2008 NIKAENDA KUJIENDELEZA 2010 NIKAHITIMU KISHA NIKAMWANDIKIA BARUA 

MWAJIRI WANGU YAKUOMBA KUBADILISHIWA MUUNDO/KAZI MAY 2011 AKANIJIBU KUWA NIMEBADILISHIWA KAZI /CHEO TOKA MWL.DARAJA IIIA KUWA AFISA ELIMU MSAIDIZI DARAJA 3.

ILIPOFIKA MWEZI UNI 2011 KWAKUWA TANGIA NIANZE KAZI TULIKUWA HATUJAWAHI KUPANDISHA MADARAJA/VYEO ZIKATOKA BARUA ZAKUPANDISHWA MADARAJA NAMI NIKAPATA CHA AJABU NIKAAMBIWA NAPONGEZWA KWA KUPANDISHWA CHEO TOKA MWALIM DARAJA 3A KUWA MWALIMU DARAJA LA2 TGTS C1 WAKATI BARUA YAKUBADILISHIWA MUUNDO WAUTUMISHI INASEMA NIMEBADILISHWA KAZI TANGU JANUARI 2011 KUWA AFISA ELIMU MSAIDIZI DRJ3 NGAZI TGTSCI  WAKATI WENGINE WALIOJIENDELEZA NAKUFIKIA NGAZI YA DIPLOMA WALIPANDISHWA KWENDA AFISA ELIMU MSAIDIZI DRJ 2 TGTS D1 WANA  

JF NAMI NAOMBA MSAADA WENU JE NIFANYEJE 
 
Apta Kayla

JF-Expert Member
Nov 18, 2010
324
70
Kwa Muijibu wa waraka Na. 11 wa Mwaka 2002 baada ya kuijiendeleza kuna kitu kinaitwa RECATEGORIZATION (Kubadilishwa kazi/Cheo) hii inahusu watu walioiendelza fani za awali na waliobadilisha fani. Kwa kuwa wewe umebadilisha fani ngoza nijikite huko. Kama unasoma huku unafanya kazi i.e kwa evening au umeenda kampus kwa kufuata taratibu za ruhusa hapa mshahara wako utaendelea ku flow ila kama ulitoroka mshahara utasimamishwa na utafunguliwa mashtaka (utalipwa nusus mshahara mpaka utakapokutwa na hatia ya utoro wa siku 5).
Baada ya kuhitimu kuna namna mbili> Ya kwanza toa taarifa kwa Mwajiri wako kuwa umehitmu na kupeleka academeic transcript. Kakam kuna nafasi kwa fani husika atakubadilishia majukumu au kazi kwenda kwenye fani husika kama ni daktari unaweza kupelekwa kwenye hospitali ya Wilaya husika (japo sina hakika kama zinamilikiwa na Halmashauri au Wizara ya Afya). Namna ya pili ni kuomba kazi nyingine ukipata fuata taratibu pitisha maombi kwa mwajiri wako ukifuzu usaili na kuajiriwa utaondoka na haki zako zote ulizokuwa nazo kwenye Ualimu.

Kila la heri

Mkuu waraka wa RECATEGORIZATION umebadilishwa kwa Waraka Na. 5{not so sure} but ni wa tarehe 1 Desemba 2009, mtumishi yeyote anapojiendeleza kada tofauti, anaweza kuajiriwa kwenye kada hiyo mpya kama mwajiriwa mpya na ataanza na mshahara wa kuingilia 'entry point' katika kada hiyo. Atahesabika kama mwajiriwa mpya na atapoteza haki zake zote katika kazi ya mwanzo yaan seniority yake na mshahara wake wa awali. So kama daktari anaajiriwa kwa Mshahara wa kuanzia let say lak5, na mwalimu huyu aliyebadilishiwa kazi/cheo alishafika let say lak 6, ataenda kuanza na mshahara wa laki 5 tena kama mwajiriwa mpya.
Pia kuna waraka{siukumbuki namba wala mwaka ila nina uhakika na maelezo nitakayotoa nitakapoupata nitatoa namba na mwaka for reference} ambao unatoa maelekezo kwa walimu wanaojiendeleza nje ya fani zao.
Mwalimu anaetaka kujiendeleza fani nyingine anatakiwa aombe likizo bila malipo kwa muda wote awapo masomoni na especially kama ni full time studies.
 
Apta Kayla

JF-Expert Member
Nov 18, 2010
324
70
HALLO GERRADI NAKUSHUKURU KWA KUMPA MWONGOZO NDEBILE MUNGU AKUBARIKI.NA MIMI NINATATIZO KAMA LA NDEBILE NILILIAJIIIWA MWAKA 2006 NA MWAKA 2008 NIKAENDA KUJIENDELEZA 2010 NIKAHITIMU KISHA NIKAMWANDIKIA BARUA  MWAJIRI WANGU YAKUOMBA KUBADILISHIWA MUUNDO/KAZI MAY 2011 AKANIJIBU KUWA NIMEBADILISHIWA KAZI /CHEO TOKA MWL.DARAJA IIIA KUWA AFISA ELIMU MSAIDIZI DARAJA 3 NA ILIPOFIKA MWEZI UNI 2011 KWAKUWA TANGIA NIANZE KAZI TULIKUWA HATUJAWAHI KUPANDISHA MADARAJA/VYEO ZIKATOKA BARUA ZAKUPANDISHWA MADARAJA NAMI NIKAPATA CHA AJABU NIKAAMBIWA NAPONGEZWA KWA KUPANDISHWA CHEO TOKA MWALIM DARAJA 3A KUWA MWALIMU DARAJA LA2 TGTS C1 WAKATI BARUA YAKUBADILISHIWA MUUNDO WAUTUMISHI INASEMA NIMEBADILISHWA KAZI TANGU JANUARI 2011 KUWA AFISA ELIMU MSAIDIZI DRJ3 NGAZI TGTSCI  WAKATI WENGINE WALIOJIENDELEZA NAKUFIKIA NGAZI YA DIPLOMA WALIPANDISHWA KWENDA AFISA ELIMU MSAIDIZI DRJ 2 TGTS D1 WANA   JF NAMI NAOMBA MSAADA WENU JE NIFANYEJE 

Mkuu kilichotokea hapa kina maelezo. Bajeti ya upandishwaji madaraja hufanyika wakati wa PE mwezi Novemba, wakati bajeti inafanyika wewe bado ulikuwa ni Mwalimu Daraja la 3 ndio maana hata barua yako ya promotion imekutoa hapo kukupeleka daraja la pili.
Ila bado ofisi ya Mkurugenzi na ofisi ya TSD hazikwepi lawama kwa kutopitia tena taarifa zao kabla ya kuidhinisha upandaji wa madaraja.
Kwa case yako na kwa mujibu wa waraka wa ubadilishaji kazi/cheo {RECATEGORIZATION} kwa walimu uliotolewa 1/12/2009 wewe unahesabika kama A.E.Msaidizi kuanzia hiyo January 2011 ulipopewa barua ya recategorization, hvyo umehama kabisa kada uliyokuwepo na kuhamia nyingine na unatakiwa uanze na mshahara wa kuingilia yaan entry point ambao ni TGTS C, hata kama ulipokuwa Mwalimu Grade A, ungepanda mpaka kufikia E bado ungeanza na mshahara huo wa C, ila ungeendelea kupata mshahara wa E kama mshahara binafsi kwa kuwa bado upo kwenye ualimu. Na unastahili kupanda utakapotoka mwongozo wa kupandisha walimu walioajiriwa 2011, kubadilishiwa kazi/cheo au kupanda mara ya mwisho 2011 minimum 3yrs 2come.
Remember that hata kama ule mshahara wa Grade A, ungekuwa umefika E, baada ya hyo miaka 3 utapewa D.
Hao waliopanda na kupewa D baada ya kupata Diploma, kama walibadilishiwa kazi/cheo 2008 kurudi nyuma ni sahihi, otherwise ni makosa yamefanyika na ofisi ya Mwajiri au TSD walioidhinisha promotion hizo.
 
Chingaboy

Member
Sep 25, 2011
22
4
Mkuu waraka wa RECATEGORIZATION umebadilishwa kwa Waraka Na. 5{not so sure} but ni wa tarehe 1 Desemba 2009, mtumishi yeyote anapojiendeleza kada tofauti, anaweza kuajiriwa kwenye kada hiyo mpya kama mwajiriwa mpya na ataanza na mshahara wa kuingilia 'entry point' katika kada hiyo. Atahesabika kama mwajiriwa mpya na atapoteza haki zake zote katika kazi ya mwanzo yaan seniority yake na mshahara wake wa awali. So kama daktari anaajiriwa kwa Mshahara wa kuanzia let say lak5, na mwalin ni kweli waraka unaouzungumzia nimewahi kuona kwamba wanaosoma nje ya fani waombe likizo bila malipo
 
SG8

JF-Expert Member
Dec 12, 2009
3,931
2,039
Mkuu waraka wa RECATEGORIZATION umebadilishwa kwa Waraka Na. 5{not so sure} but ni wa tarehe 1 Desemba 2009, mtumishi yeyote anapojiendeleza kada tofauti, anaweza kuajiriwa kwenye kada hiyo mpya kama mwajiriwa mpya na ataanza na mshahara wa kuingilia 'entry point' katika kada hiyo. Atahesabika kama mwajiriwa mpya na atapoteza haki zake zote katika kazi ya mwanzo yaan seniority yake na mshahara wake wa awali. So kama daktari anaajiriwa kwa Mshahara wa kuanzia let say lak5, na mwalimu huyu aliyebadilishiwa kazi/cheo alishafika let say lak 6, ataenda kuanza na mshahara wa laki 5 tena kama mwajiriwa mpya.
Pia kuna waraka{siukumbuki namba wala mwaka ila nina uhakika na maelezo nitakayotoa nitakapoupata nitatoa namba na mwaka for reference} ambao unatoa maelekezo kwa walimu wanaojiendeleza nje ya fani zao.
Mwalimu anaetaka kujiendeleza fani nyingine anatakiwa aombe likizo bila malipo kwa muda wote awapo masomoni na especially kama ni full time studies.
Nakubaliana na wewe Mkuu lakini Waraka na 5 wa desemba 2009 ulitolewa kwa ajili ya ku effect ule wa 2002 amabo ulikuwa haujaanza kutumika. Kabla ya hapo Mwalimu alikuwa nafanyiwa recategorization na kupandishwa cheo kama alistahili. Kwa sasa akifanyiwa recategorization atalazimika kutumikia Cheo kipya miaka Mitatu na si zaidi ya miaka mitano ndipo aende cheo kinachofuata. Waraka unaofafanua walimu wanaojiendeleza nje ya fani zao ni huo huo wa 2009 ukikzia ule wa 2002 lakini kwa kuwa nyaraka zote za maendeleo ya Utumishi zilitolewa 2002 ndizo zinazotumika kama reference zaidi ya hapo ni marekebisho tu madogo kulingana na mabadiliko ya sheria na kanuni za Utumishi zinavyobadilika
 
SG8

JF-Expert Member
Dec 12, 2009
3,931
2,039
HALLO GERRADI NAKUSHUKURU KWA KUMPA MWONGOZO NDEBILE MUNGU AKUBARIKI.NA MIMI NINATATIZO KAMA LA NDEBILE NILILIAJIIIWA MWAKA 2006 NA MWAKA 2008 NIKAENDA KUJIENDELEZA 2010 NIKAHITIMU KISHA NIKAMWANDIKIA BARUA  MWAJIRI WANGU YAKUOMBA KUBADILISHIWA MUUNDO/KAZI MAY 2011 AKANIJIBU KUWA NIMEBADILISHIWA KAZI /CHEO TOKA MWL.DARAJA IIIA KUWA AFISA ELIMU MSAIDIZI DARAJA 3 NA ILIPOFIKA MWEZI UNI 2011 KWAKUWA TANGIA NIANZE KAZI TULIKUWA HATUJAWAHI KUPANDISHA MADARAJA/VYEO ZIKATOKA BARUA ZAKUPANDISHWA MADARAJA NAMI NIKAPATA CHA AJABU NIKAAMBIWA NAPONGEZWA KWA KUPANDISHWA CHEO TOKA MWALIM DARAJA 3A KUWA MWALIMU DARAJA LA2 TGTS C1 WAKATI BARUA YAKUBADILISHIWA MUUNDO WAUTUMISHI INASEMA NIMEBADILISHWA KAZI TANGU JANUARI 2011 KUWA AFISA ELIMU MSAIDIZI DRJ3 NGAZI TGTSCI  WAKATI WENGINE WALIOJIENDELEZA NAKUFIKIA NGAZI YA DIPLOMA WALIPANDISHWA KWENDA AFISA ELIMU MSAIDIZI DRJ 2 TGTS D1 WANA   JF NAMI NAOMBA MSAADA WENU JE NIFANYEJE 
Kama ajira yako ni ya 2006 ulitakiwa upate promotion mwaka 2009 au 2010 kabla hujamaliza masomo.So ungetoka Mwalimu Drj III kwenda Drj III TGTS C. Baada ya kuhitimu ulitakiwa kuandika barua ikiambatana na result slip kwa mwajiri wako ukiomba kubadilishiwa Cheo toka Mwalimu kwenda Afisa Elimu Msaidizi TGTS C. Cheo hicho unaanzia kwenye entry point na utakitumikia miaka isiyopungua mitatu na isizidi mitano then unapanda kwenda cheo kinachofuata (kwa kesi yako Afisa Elimu Msaidizi daraja la II TGTS D). Hata kama ungekuwa umefika cheo cha Mwalimu Mwandamizi TGTS E ungebadilishwa baada ya kusoma kuwa AEM III na kuanza kwenye entry point.

Ni hayo tu mengine Mkuu Apta ameeleza vizuri sana
 
SG8

JF-Expert Member
Dec 12, 2009
3,931
2,039
wanaJF nisaidie sheria za kazi zinasemaje kuhusu mtumishi wa umma anayeenda kusomea kada tofauti na ile aliyoajiriwa nayo? mf.niliajiliwa kama mwalimu nina miaka 8 kazini na nimejiendeleza kwenye evening class nikafikia vigezo vya kusomea Udaktari MD,mwajiri yaani serikari atanilipia masomo?mshahara wangu wa ualimu nitaendelea kupata wakati ninasoma?nikimaliza masomo nitaomba kuajiliwa upya au nitaamishwa tu kwenda department nyingine? Naomba msaada japo kidogo tu,nawasilishaj.
Hapo kwenye kulipiwa nilipitiwa sikujibu> Ni hivi kama nilivyosema awali kama Mwajiri anakuhitaji baada ya kuhitimu kwenye huo u daktari anaweza kukulipia bila taabu zaidi ya hapo itabid tu utafute namna nyingine ya kujigharimia hasa kwa kupitia Loan Board kama unachukua Adv Diploma au MD. Ila mshahara waajiri wengi huwa wako fair ukifuata taratibu ataendelea kukulipa tu hasa ukizingatia wewe ni senior kwenye service, miaka 8 sio haba
 
Ndebile

JF-Expert Member
Sep 14, 2011
7,242
9,802
asante mkuu, niliogopa kumuuliza yeyote si unajua hizi underground movements sio vizuri kuzi-expose utakatishwa tamaa mpaka basi!
 
Ndebile

JF-Expert Member
Sep 14, 2011
7,242
9,802
Mkuu waraka wa RECATEGORIZATION umebadilishwa kwa Waraka Na. 5{not so sure} but ni wa tarehe 1 Desemba 2009, mtumishi yeyote anapojiendeleza kada tofauti, anaweza kuajiriwa kwenye kada hiyo mpya kama mwajiriwa mpya na ataanza na mshahara wa kuingilia 'entry point' katika kada hiyo. Atahesabika kama mwajiriwa mpya na atapoteza haki zake zote katika kazi ya mwanzo yaan seniority yake na mshahara wake wa awali. So kama daktari anaajiriwa kwa Mshahara wa kuanzia let say lak5, na mwalin ni kweli waraka unaouzungumzia nimewahi kuona kwamba wanaosoma nje ya fani waombe likizo bila malipo

asante,ila mimi sina tatizo na kuanza na mshahara wa 'first appointment' kikubwa tu kutimiza ndoto yangu.
 
mbasamwoga

Member
Jul 6, 2011
70
12
Kweli jf tunatisha kwa knowledge anuwai. kaka gerrad kwanini waajili wengine hawabadili increment za mshahara kwa wakati?

yaani ni vigezo gani vinatumika kupandisha madaraja ya mshahara?? Are they open ???
 
Laurence

JF-Expert Member
Jun 11, 2011
3,104
418
Hapo hapo mkuu Gerrad inabidi uendelee kutupatia somo zaidi,mfano mimi nimeajiriwa mwl wa cheti mwaka 2006 na juzi tu nimemaliza BA ed na juzi mwezi wa 7 ndio nmepata first appointment na zaidi nmeomba ajira mpya,je unanishauri nn kwamba nienda ajira mpya au niandike barua kwa mwajiri wangu? Na zaidi nahofu je kweli watanihamisha pale nlipokuwepo awali na kwenda sehem nyingine? Nishauri mkuu maana naambiwa wakuu wapo Moro wanapangia watu Mikoa,natanguliza shukrani
 
Inanambo

JF-Expert Member
Jun 26, 2011
3,798
2,527
asanteni sana. Utumishi wa UMMA wa TANZANIA hauna haja na mtu aliyejiendeleza kwenye kada ambayo haifanyii kazi. kama umejiendeleza mfano Secretary na kupata degree ya HR hawakubadilishi kwa kulipa mshahara wa digrii. Hata kama una miaka 5 ili ustaafu wanakuambia umepoteza haki zako zote kwa hiyo hiyo HR uanze kwenye entry point kama unataka kuifanya. Mimi huwa naishangaa sana Miongozo hii ambayo haifikirii. Sielewi kama unaweza kupata Digrii ya Secretary. Utumishi wa UMMA hawataki mtu ambaye ni Multidisplinary japo sasa hivi Elimu ziko za kila aina na mtu unapaswa ujiendeleze kwenye fani utakayo ili uweze kujituma vizuri karne. Hata vyuoni wanafundisha kuwa kwenye Recruitment kuna INTERNAL na EXTERNAL. INTERNAL ni kutangaza nafasi ya kazi ndani kwenu ili kama kuna Mtumishi mwenye kusomea fani unayotaka kuajiri nayo watu aifanye kwa kuwa unampa Motisha ya kujiona anadhaminiwa na anaijua vema Culture ya Organization yenu. Kama hayupo ndio unatafuta EXTERNAL. Cha kushangaza utaona wanaleta mfanyakazi mpya toka nje na siyo kukufanyia RECATOGERAZATION wewe uliyesoma fani tofauti. Utumishi wa UMMA unatuvunja moyo kujiendeleza kwenye masomo ya juu hasa sisi ambao kazi zetu hazina elimu ya Digrii. Dereva, Mhudumu, Secretary, na wengine digrii za fani yetu zinapatikana wapi? Mimi nadhani hii ni kuvunja wafanyakazi moyo hasa wale waliosahaulika waajiri wao kuendelezwa kimasomo wakajitahidi wenyewe kutimiza ndoto zao za One day kupata Digrii walitumikie taifa. Watu wengi hasa akina mama waliitika mwito wa kujiendeleza kimasomo wakiwa kazini wakatumia muda wao wa Jioni kujiandikisha na kujisomea vyuo mbalimbali kwa ada zao hadi kuGraduate lakini kazini wanawakatisha tamaa kuwa miongozo inakataa kuwapandisha vyeo au kuwapa mishahara ya Degree walizosomea kwa kuwa hawana Experience. Wengine tumepata Degree miaka miwili iliyopita bado kazini hawatutofautishi na wasiokuwa nazo. Tunaambiwa kama umesoma usichofanyia kazi Work done is equal to Zero. Tumebakisha miaka 8 Tustaafu na digrii tulizopata hazibadilishi maisha yetu. Wenzetu wanasema kama kusoma kwenyewe ndio huku basi watastaafu bila digrii. Hivyo wanajamii wengine Degree zetu ni za LAST RESPECT kwamba marehemu alisoma shahada ya Ualimu, Uhasibu, Utawala wa Biashara na alifanya kazi kama Secretary Ofisi ya UMMA. PLEASE UTUMISHI wa UMMA mnapotoa MIONGOZO someni ALAMA ZA NYAKATI msiwe kama viongozi wa ZAMA ZA MAWE. Nyakati hizi elimu ziko nyingi na mfanyakazi anaweza kusoma atakacho kwa faida yake, Utumishi na taifa lake. Ndio sababu Watanzania tunaambiwa hatuuziki kikazi Kimataifa. Miongozo ya kurudisha wafanyakazi nyuma na kuwanyima Uhuru wa Kusoma inakatisha tamaa. Jiulizeni huyu aliyejisomesha mwenyewe mlimpatia nafasi ya kusoma na kumlipia mtakacho akashindwa? Wengi wanasoma watakacho baada ya KUSOTA miaka mingi bila kuendelezwa na nafasi za kujiendeleza mkawapa Damu changa kazini hasa pale mnaposhindwa Diversity Management na kuwahesabia wafanyakazi UMRI.
 
Bei Mbaya

JF-Expert Member
Nov 24, 2010
2,262
840
Mkuu waraka wa RECATEGORIZATION umebadilishwa kwa Waraka Na. 5{not so sure} but ni wa tarehe 1 Desemba 2009, mtumishi yeyote anapojiendeleza kada tofauti, anaweza kuajiriwa kwenye kada hiyo mpya kama mwajiriwa mpya na ataanza na mshahara wa kuingilia 'entry point' katika kada hiyo. Atahesabika kama mwajiriwa mpya na atapoteza haki zake zote katika kazi ya mwanzo yaan seniority yake na mshahara wake wa awali. So kama daktari anaajiriwa kwa Mshahara wa kuanzia let say lak5, na mwalin ni kweli waraka unaouzungumzia nimewahi kuona kwamba wanaosoma nje ya fani waombe likizo bila malipo

vile vile atatakiwa kufanyiwa usaili upya kwa kada hiyo mpya
 
Pasco_jr_ngumi

JF-Expert Member
Nov 20, 2010
1,802
279
Mmmmm.......nimefurahi sanaaa na hii topic!!! imenigusa patamu, nna diploma ya ualimu na nimeaajiriwa as tutor katika chuo cha ualimu!! Mwaka 2008 nilienda kulamba digrii na nimeipata hii ya B.A.ACCOUNTING AND FINANCE........... hadi bosi wangu mpyaaa aliniita na kunishangaaa... as still niko young man, with 30yrs of age. Wacha nipige timing by next year nikapige MBA, hapo nitajipanga nitoke au???? loooooohhhhhhhh
 
2 Reactions
Reply
Top Bottom