Sesten Zakazaka
JF-Expert Member
- Sep 10, 2017
- 10,557
- 19,107
Dah! Hata kama wewe sio Matiku Matare mwenyewe (maana tulisikia aliitwa mahali kwenda kuonana na PM Warioba na hatima ya uhai wake ikawa ni utata baada ya Chuo Kufungwa kufuatia extended Baraza) lakini ni kweli hasa uliziishi siasa zile za Mzee Punch!NI MIMI.Punch kilikuwa ni kikundi kisichojulikana ambacho hakikuwa na jukwaa la kusemea na hakikujulikana tangu mwaka 1961 UDSM ilipoanza kilikuwapo kukosoa uongozi wa chuo na serikali bila kujulikana. Matiko Matare, Rudovick Bazigiza, James Mbatia, Mosene Nyambabe, Antony Komu ,Kangi Lugola, Harun kimaro, Ally Salehe na Dr.Kebwe walikuwa ni viongozi wa serikali ya DARUSO 1989 hadi 1992 na mashujaa wa wakati huo waliotetea hadhi ya chuo na kuikosoa serikali ya Rais Mwinyi Nkurumah Hall, hadharani na kwenye magazeti. Tume ya Jaji Koroso iliyopewa jukumu la kuchunguza mgogoro huo haikukuta mwanafunzi yeyote na hatia. Rais Mwinyi alitusamehe kama baba na sisi kama watoto tukamwomba msamaha yakaisha . Yale yote tuliyopigania yafanyike, ndiyo yanafanyika sasa chini ya serikali ya awamu ya tano. Sasa utapingaje mtu anayefanya yale unayotaka yafanyike? POLE SANA NDUGU YANGU KWA KUDANGANYWA!
Nakumbuka Matiku akiwauliza Wanachuo pale Nkurumah baada ya aliyekua Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Mr Ngonyani kuwasihi wanafunzi warudi darasani huku wanafunzi wakimtaka Chancellor ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ..... "Should we go back to class? There was an up roar from the crowd "NOOOOO" Kisha akamalizia "No president no class"
Ila VC Prof G. Mmary alaikua kichwa sana. Wakati huo intellectuals wakisimamia taaluma zao kisawasawa hasa. Kulikua hakuna Prof fake Tanzania kama tunaowaona sasa
♀️