Mwl Nyerere Alistahili kupewa nobel prizes | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwl Nyerere Alistahili kupewa nobel prizes

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Semenya, Oct 11, 2009.

 1. Semenya

  Semenya JF-Expert Member

  #1
  Oct 11, 2009
  Joined: Sep 5, 2009
  Messages: 572
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 35
  jamani mwaka 1984 Desond Tutu alipata Nobel Peace prize, me nachoshangaa kuona mtu kama mwalim JK Nyerere hakuwahi kupata tuzo hiyo...sababu moja nayoona ni kwamba Mwalim alikua anapenda socialism, labda ndo maana hawakumpa...nikifika kwenye hayo mawazo napata pia wasiwasi na hizi tuzo.....nikiangalia Obama na JK Nterere na Tutu, hata mandela mwenyewe hawajafanya makubwa kwa waaFrica kama Nyerere....mnaonaje hili jamani? Me naona alistahili kupewa....
   
 2. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #2
  Oct 11, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  It is water under the bridge. Mwalimu mchango wake mkubwa ulikuwa barani Afrika na enzi hizo Afrika haikuwa na uzito wowote katika medani ya siasa za kimataifa.
   
 3. Semenya

  Semenya JF-Expert Member

  #3
  Oct 11, 2009
  Joined: Sep 5, 2009
  Messages: 572
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 35
  watu kama akina Desmond tutu, Mandela na Obama wamepata tuzo ya Nobel Peace Prize, hao wote hawajawahi na sidhani kama watamfikia baba wa Taifa kwa kukomboa Africa... hiyo SA JK Nyerere alichangia sana kupata uhuru...nachoshangaa hakupata tuzo hiyo...me naona alistahili kupata hiyo tuzo..au kwasababu alikua ni socialist? anyways kwangu mimi kafanya makubwa kuliko hao watu niliowataja kwa Africa......Mnaonaje jamani?
   
 4. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #4
  Oct 11, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Hata mtu kama Mahatma Ghandhi haja pewa Nobel peace prize so that should tell you a lot. Tuzo hizo nazo zina siasa za chini chini ndani yake.
   
 5. Mbogela

  Mbogela JF-Expert Member

  #5
  Oct 11, 2009
  Joined: Jan 28, 2008
  Messages: 1,369
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  semenya Binafsi nimeshukuru na kufurahi na changamoto yako, lakini naomba kukuliza wewe mwenyewe ungekuwa kwenye kamati ya kuscreen watu wa kuwapa Nobel Prize ungeweza kumteteaje mwalimu JKN kuwa apewe na anastahili hiyo award/prize? Maana katika bandiko lako unasema kafanya mengi kwa bara la Africa mengi yepi? Nobel Prze zilianzishwa na mtu ambaye alilaani vita JKN alipigana vita na Uganda, vita ambayo hata hapa JF tumequestion mantiki yake. Sababu alizosema tulikuwa nazo za kwenda uganda leo hii wengi wetu hatuzioni?? wangapi walikufa Uganda? kwa kufa kiasi hicho cha watu tayari anakuwa disquliafied kupata NOBEL.

  Ukiangalia hotuba zake, tafuta hata You tube zipo utaioona hotuba moja anayosema kuwa aliombwa apatanishwe na Idd Amin lakini kwa maneno yake mwenyewe anasema aliwauliza watu wanaosema kuwa aache kumpiga Idd Amini kuwa walikuwa wapi??? Sasa Mkuu Nobel Prize haaziendi kwa Jicho kwa jicho, zinaenda kwa ukipigwa shavu la kushoto geuza la kulia.

  Desmond Tutu siku moja alipokuwa anatembea mtaanzai aliona Mob wanamtandika kijana alienda akamwangukia juu akamfunika watu wakaanza kumpa kibano yeye mpaka alipookolewa na dola. Nelson Mandela alipoteza uraia wake kwa kuchoma Passport, kuna watu wameadnika Historia kubwa sana kama akina Steve Biko, Chris Hann, Bob Moses lakini bado hawajatambuliwa.

  JKN alihamisha watu kutoka kwenye vijiji vyao kwa nguvu, watu wengi walipigwa na migambo, walichomewa nyumba zao, walipoteza mifugo, waliliwa na simba, acha waliokufa kwa maralia, Taifodi, vipindupindu kwenye maeneo waliyowekwa yasioyofaa kwa maisha ya Binadamu.

  JKN alitaifisha mali za watu kwa azimio lake la arusha (hii ni sawa na anachofanya comrade Mugabe-Jongwe)

  Pitia vigezo vya Nobel alafu toa mchanganuo cha alichofanya JKN kuweza kutunukiwa hiyo Prize. Ni Mtazamo Tu
   
 6. Semenya

  Semenya JF-Expert Member

  #6
  Oct 11, 2009
  Joined: Sep 5, 2009
  Messages: 572
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 35
  watu kama Desmond Tutu, Nelson Mandela na Barack Obama wamepata Nobel Peace prize, Kwa Mtazamo wangu Mwalim JK Nyerere amefanya mengi makubwa kwa Africa kuliko hao watu na hamna hata mmoja anaemfikia...kwahiyo kwa mtazamo wangu alistahili kupata nobel peace prize [JK Nyerere]. Mawazo yananiijia kuwa hakupewa kwasababu ni socialist, nikiwaza hivyo nachanganyikiwa na credibility ya hii tuzo, ya kwamba je siasa ndo inatawala nobel peace prize?

  Mnaonaje jamani?
   
 7. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #7
  Oct 11, 2009
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,579
  Likes Received: 3,881
  Trophy Points: 280
  Kweli Nyerere alistahili, lakini haujakatazwa kupeleka jina lake.

  Hitler, Musollini,Stalini wote jao wameshawahi kuwa nominated!!!.

  Nani alipeleka jina la Nyerere?

  My take is that forget what is Nobel Prize itakupa pressure, is not a bible or Quran

  Dunia ina watu wengi wanaostahili mambo fulani lakin hawapati

  Mpaka leo Nobel prize wanalalamikiwa kwa kutowapa

  Mahatma Gandhi, Eleanor Roosevelt, Václav Havel, Ken Saro-Wiwa, Sari Nusseibeh, Corazon Aquino and Liu Xiaobo.

  Obama mwenyewe hakustahili, sasa kitu gani kinakusukuma kuwa lazima upate, HII YA WAZUNGU WAMEANZSHA WAO KWA MANUFAA YAO, POLITICS HAZITAKOSA, ACHILIA MBALI UPENDELEAJI.
   
 8. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #8
  Oct 11, 2009
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  Semenya u r turning me on big time,sikujua kuwa una bongo iliyo deep namna hiyo.....i thought u were just another woman.
   
 9. Semenya

  Semenya JF-Expert Member

  #9
  Oct 11, 2009
  Joined: Sep 5, 2009
  Messages: 572
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 35
  mkuu tutu kapewa mwaka 1984, unataka kuniambia mwalim hakustahili hata kipindi hicho?
   
 10. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #10
  Oct 11, 2009
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  semenya semenya...............
   
 11. Semenya

  Semenya JF-Expert Member

  #11
  Oct 11, 2009
  Joined: Sep 5, 2009
  Messages: 572
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 35
  kaka Africa hii leo ipo kwa mchango wa Mwalim, Mbona Obama bado anapeleka majeshi Afkhanstan na ameshinda...mwalim kakomboa bara la Africa including huyo Mandela aliepoteza uraia wake....iddi amin sinauhakika sana lakini nahisi UN walitoa ruhusa [i stand to be corrected] na iddi amin alikua dikteta, hata nchi yake alikimbia.

  mambo ya kuchukua ardhi ya mugabe kaka ni haki yake kwa upande mmoja ila alikosea mda...Nyerere alifanya mambo hayo wakati ule mapema na bila hivyo sidhani hata wewe ungekua na kiwanja hapa Tanzania....Mugabe alikubaliana na Uk kuwa kuna portion ya ardhi inabidi irudi kwa weusi, ila blair alikataa, akidai hakuwepo katika huo mkataba

  me Nyerere ningempa kwa kigezo kimoja ambacho ni kikubwa kuliko kwa Obama, Mandela Tutu kuwa amelikomboa bara la Africa...sidhani kama obama kalikomboa bara la Africa..labda kuwa the first African American President..bear in mind sio totaly african ni anamama mzungu anyway sio big deal
   
 12. S

  Shamu JF-Expert Member

  #12
  Oct 11, 2009
  Joined: Dec 29, 2008
  Messages: 511
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hii tuzo hawapewi MADICTETA, na Nyerere alikuwa mmoja wao hao MADICTETA.
   
 13. M

  Mkandara Verified User

  #13
  Oct 11, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Arafat, De Klack, Perez hao wahakuwa madikteta!
   
 14. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #14
  Oct 11, 2009
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  We semenya vipi??????hii umeiposti mara ngapi humu???????

  Hii thread ya tatu but topic ni hiyo hiyo,why????
  We nyerere ni babu yako wa damu nini???????
   
 15. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #15
  Oct 11, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Mbogela,
  Speak for yourself. Sijawahi kuquestion sababu za kwenda vitani na Uganda na hata hapa JF wanaoquestion au walioquestion wana agenda zao. Kila Mtanzania makini anajua sababu za kupigana na Idi Amin. Na katika vijiji vya ujamaa ni watu kama wewe mnaoamini bila ushahidi kuwa kuna binadamu walioliwa na simba. Naona mnajaribu kuandika historia upya.
   
 16. M

  Mkandara Verified User

  #16
  Oct 11, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Jasusi,
  Ni hawa hawa waliosema na kuamini kuwa ktk Ujamaa tulikuwa tuki share hadi wake/waume ktk ndoa zetu..
   
 17. Richard

  Richard JF-Expert Member

  #17
  Oct 11, 2009
  Joined: Oct 23, 2006
  Messages: 8,253
  Likes Received: 4,275
  Trophy Points: 280
  Lakini wakulu hii Nobel Prize ilianzishwa katika kumuenzi yule mzungu Alfred Nobel kupitia mfuko wa Nobel yaani Nobel Foundation.

  Mfuko huo unatoa tuzo kwenye maeneo ya Sayansi, Fisikia, Kemia, Madawa, Fasihi na mwisho ni hio Amani.

  Sasa ukifanya jambo la maana la ama kuvumbua au kutatua kama si kutafuta suluhisho la suala moja kati ya hayo basi jina lako linaweza kuorodheshwa katika orodha ya wanaopendekezwa kupewa tuzo mojawapo.

  Kuna orodha ndeefu ya waliowahi kupewa tuzo hio lakini tuangalie wachache

  1964 - Martin Luther King Jr.

  1984 - Desmond Tutu

  1993 - Nelson Mandela, F.W. de Klerk (hii bado najiuliza)

  1994 - Yasser Arafat, Shimon Peres, Yitzhak Rabin (hawa pia sielewi)

  2001 - United Nations, Kofi Annan

  2004 - Wangari Maathai

  Raisi Obama alikuwa ni miongozi mwa wale waliopendekezwa kupewa tuzo hio na akapewa.

  Sasa si kuna Nyerer Foundation nao wangejaribu kutoa mfano kwa kutoa tuzo kwa watanzania mbalimbali halafu baadae kwa waafrika kama ikiwezekana.
   
 18. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #18
  Oct 11, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Richard,
  Nyerere Foundation iko kwenye kitanda cha mgonjwa. Inasubiri kufufuliwa na akina Kagame na Museveni.
   
 19. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #19
  Oct 11, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Anashindwa kumfahamu Nyerere na undergorund zake ,msione watu wanapewa hizo Nobel mkaona ni mambo ya kuonekana ukiwa mstari wa mbele ,unachunguzwa sana sana kiasi ya kutoonekana ni mnyanyasaji na mwenye kubeba lawama ,Nyerere amevamia Zanzibar ,amevania Uganda amevamia Malawi kuna watu wametoweka katika Tanzania chini ya utawala wake na hawajulikani walipo hadi leo ,sasa hayo mambo wanaotoa hiyo Nobel wanayafuatilia japo ni shutuma na hazina ushahidi lakini ni madoa ambayo hayatakiwi yawepo. Sasa huo utakatifu mliombatiza kwani haujamtosha huko aliko ? Obama huyo hapo hata mwaka hajatimiza amepewa Nobel ,watu serikalini wamejaa utajiri usiojulikana wameupata vipi afu mnataka kiongozi bado apewe na Nobel ? Nyie vipi ?
   
 20. s

  shabanimzungu Senior Member

  #20
  Oct 11, 2009
  Joined: Jul 7, 2009
  Messages: 182
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nyerere? forget it ..nobel peace prize is only if you toe the western line....mwalimu was honest and did not care about west..though he was awarded a prize by INDIA...that is good enough!!!!!!!!!
   
Loading...