MWL. J. K. Nyerere kuhusu vyama vya upinzani

ASIWAJU

JF-Expert Member
Nov 18, 2022
1,939
1,625
Habari za saa wanachama wote natumai ni njema .

Kama kichwa cha mada kisemavyo "Mwalimu nyerere kuhusu vyama vya upinzani”.

Ningependa kuwa karibisha wadau wote kutoa maoni na michango huru kutokana na mazungumzo mafupi katika video hii nilio weka hapa ikumuonesha Mwalimu Julius Kambarage Nyerere akizungumza kuhusu vyama vya upinzani na mienendo yake hapa nchini.


Maswali:
1. Je, maneno hayo ya Mwalimu yana akisi vyama vya upinzani vilivyopo sasa nchini?

2. Je, ushauri alio toa Mwalimu kwa vyama vya upinzani wakati huo pia unaweza kuwa bora au mbaya kwa vyama vya upinzani sasa?

3. Mwalimu ali kusudia nini kuita vyama vya upinzani ni vyama vya ruzuku?

4. Je, tuna kila sababu kupunguza utitiri wa vyama vingi vili vyopo hapa nchini?

5. Nini maoni yako ya jumla kuhusu yote aliyo zungumza mwalimu katika hiyo video fupi?

KARIBUNI.
 
Historia ya vyama vya UPINZANI Tanganyika Tanzania ni kubwa Sana.

Mwalimu aliwahi kufuta vyama vya UPINZANI kabla hajavirejesha tena 1992.

ALIYEWAANDAA AKINA SEIF, POLOSYA, MTEI,LIPUMBA,MREMA NK ni Mwalimu.

Alitengeneza mamluki wa kuisaidia ccm.
Nchi inateketea.
 
Historia ya vyama vya UPINZANI Tanganyika Tanzania ni kubwa Sana.

Mwalimu aliwahi kufuta vyama vya UPINZANI kabla hajavirejesha tena 1992.

ALIYEWAANDAA AKINA SEIF, POLOSYA, MTEI,LIPUMBA,MREMA NK ni Mwalimu.

Alitengeneza mamluki wa kuisaidia ccm.
Nchi inateketea.
Kwa hiyo ndugu una maanisha vyama vya upinzani hapa nchini ni vyama vya mamluki wa CCM ?
 
Tanzania tuna idadi ya vyama ishirini na mbili [22] vya siasa.
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom