Mwizi mjinga zaidi Duniani akamatwa huko Marekani

Mwizi mjinga zaidi Duniani akamatwa huko Marekani

Ndio maana mimi nilishaji Delete siku nyingi kwenye FaceBook!
 
FaceBook ya sasa hata ukila Wali wa Maharagwe friends waliokwenye account yako wanajua!
 
Hapa inanikumbusha ile kesi ya mwizi wa Keko mwaka jana. Jamaa alikwenda kuiba nyumbani kwa kibosile fulani, bahati nzuri akabahatika kuingia ndani bila ya kuvunja anything kwani wenyewe walipotoka nyumbani asubuhi walikuwa wamejisahau kwa kutofunga nyumba yao. Jamaa akaingia, kabla ya yote akavua nguo zake alizokwenda nazo na kuanza kuoga. Alipo maliza akatafuta nguo za mwenye nyumba na kuzivaa ili ajaribu. Bahati mbaya kwake alipovaa tu zile nguo wakaja watu wakagonga kengele/alarm basi jamaa akajificha. Walipo ondoka naye jamaa akaona soo akatimua zake na zile nguo za mwenye nyumba zikiwa bado mwilini mwake, kumbe ndani ya zile nguo zake alizovua kulikuwa na vitambulisho vyake pamoja na anuani ya anapoishi. Jamaa alikamatwa kiulainiiiii. Nafikiri mpaka sasa atakuwa ananyea ndoo Keko.

Hahahaha mkuu huyu naye ni zuzu jingine
 
Na yule mwizi aliyeingia kwenye mansion ya tajiri akadondoka/akateleza akavunjika mkono...aka claim toka insurance na akalipwa, alilipwa pesa nyingi tu, kwasababu mwenye nyumba aliweka floor ya very slippery tiles na bila kuweka warning ya watu watembee kwa uangalifu, alipata lawyer mzuri na mwizi akalipwa... ilikuwa hukohuko Marekani..
 
Mi namjua mwizi mjinga zaidi duniani ni CCM. Anaiba akidhani wenye mali ni wale wale wa mwaka 47.
 
View attachment 167539


Dunia ina matukio mengi ambayo unaweza kudhani unaona maigizo lakini mwishoni utaamini unachokiona ni kitu halisi kwa kuwa hautaona majina ya wahusika yakipita hewani kama movie.

CBS Minnesota imeripoti habari ambayo inamhusisha mwizi ambaye polisi walimtaja kuwa mmoja kati ya wezi wapumbavu zaidi duniani, Nicholas Wig mwenye umri wa miaka 26.

Bwana Wig anadaiwa kuvamia nyumba ya mtu wakati mwenye nyumba hayupo na kuiba vitu kadhaa lakini mwisho akagundua kuna computer yenye internet, na ndipo alipoamua kuingia Facebook kufanya yake lakini ghafla aliondoka na kuiacha computer hiyo huku akisahau ku-log out.

Unaambiwa mwenye mali alipofika kwake alitamani kulia machozi baada ya kugundua kuwa tayari amelizwa vitu kadhaa nyumbani kwake, lakini alipoishika computer yake iliyoachwa na mwizi huyo aligundua kuwa mwizi wake aliingia Facebook na akaondoka bila ku-log out kwa hiyo taarifa zake na picha zake zote ziko wazi.
Baada ya kuripoti polisi, hatua za kumsaka zilianza mapema na wakafanikiwa kumkamata jamaa tena akiwa amevaa saa aliyoiba kwenye nyumba hiyo.

Mwanasheria wa County/wilaya ya Dakota, James Backstrom alipofanya mahojiano na SBC alitamka kuwa hajawahi kupata kesi ya mwizi -------- kama ya Wig.


mwizi -------- zaidi Ni yule alievamia nyumba akasomba Mali za kwenye nyumba kwa trip...trip ya mwisho akaamua kufungua friji akate kiu..akantwa via za kutosha mpka akazima eneo la tukio
 
Na yule mwizi aliyeingia kwenye mansion ya tajiri akadondoka/akateleza akavunjika mkono...aka claim toka insurance na akalipwa, alilipwa pesa nyingi tu, kwasababu mwenye nyumba aliweka floor ya very slippery tiles na bila kuweka warning ya watu watembee kwa uangalifu, alipata lawyer mzuri na mwizi akalipwa... ilikuwa hukohuko Marekani..

Marekani na sharia zao....jitu linakula burger kila siku lananenepiana alafu linaenda kuishtaki "mcdonalnads" eti imefanya anenepe.....au mtu unavuta pacti 10 za sigara kwa siku ukipata cancer unaenda kushtaki makampuni ya sigara....hawa mabwege sana!
 
Hamfikii Andrew Chenge, yeye aliiba alipobanwa akasema nimeiba vijisenti!
 
Apelekwe akafanye kazi facebook
Sent from my RM-846_im_mea3_286 using Tapatalk
 
Wig5.jpg

kaka Nicholas Wig unamoyo kweli kweli?kwenda kuliibia shababi kama hili..

Wig8.jpg

ulikua unajiaminmi nini?lingekukuta ndani??walah lingekufunua marinda,kinyumba chenyewe hakina hata sehemu ya kujificha

Wig3.jpg


Wig4.jpg
 
Back
Top Bottom