mwizi huyo aliyekamatwa mida ya saa moja na nusu ya jioni hii akiwa block katika harakati za kuiba PC za wanafunzi wa chuo kikuu cha dar es salaam waishio katika hostel hii, mwizi huyo alipo ulizwa kama ni mwanafunzi alishindwa kujitetea na kusema kuwa kaacha kitambulisho chake getini kitu ambacho kiliwapandisha jazba wanafunzi hao kwa sababu utaratibu huo haupo hapa mabibo. Baada ya hapo alianza kushushiwa kipigo cha mbwa mwitu mpaka pale ambapo polisi walipoingilia kati.
Binafsi niliwapongeza sana na kufurahishwa na kitendo kile kwani ni jana tu usiku baada ya umeme kukatika tu na sisi tukiwa cafeteria tukipata chakula cha jioni tuliibiwa PC nne moja ambayo ni yangu ya 650000 Dell, HP ya 600000 na toshiba 2 zenye thamani ya 520000@
my take wizi ni kitu kibaya sana kwani kinarudisha maendeleo nyuma.
Nimeishi hapo Mabibo hostel, Block F kwa miaka 4, kumetokea incidents nyingi za wizi na watu kuuliwa!, kiukweli nothing justifies taking someones life kwa wizi wa kitu chochote, material thing!, iwe ni simu, laptop au pc, au kitu chochote cha thamani, kwasababu hakuna kitu chochote duniani chenye thamani zaidi ya uhai wa binadamu, yaani life!, ila wanafunzi wa hapo kutokana na mob psychology, wanageuka sio binadamu tena, ni ma wild beast!, kama vichaa kabisa!.
Wakati nikiwa mwanafunzi wa UDSM, nikiwa naishi Bock F hapo Mabibo Hostel, kuna mwanafunzi aliuliwa kwa kusingiziwa tuu mwizi na demu wake!, baada ya demu kutoa kilio cha mwizi!, watu walimshushia kipigo huyo kijana bila hata kuuliza kaiba nini?, by the time wale auxilary polisi wamefika eneo la tukio, wanafunzi walikuwa ni wengi wamemzingira huyo kijana na hawakumwacha mpaka walipohakikisha wameua!, huku wakishangilia kwa hamasa na furaha ya ushujaa wa kuua mwizi!.
Kesho yake baada ya kujulikana aliyeuwawa ni nani, na aliyepiga yowe la mwizi ni nani, ndipo room mate wa yule girlfriend wake akaumia kwa kitendo alichotendewa huyo mvulana wa watu!, akaleak data kuwa kijana yule, hakuwa mwizi, bali alikuwa ni boyfriend aliyepigwa tuu kibuti!, akaja kuomba msamaha, akafukuzwa kama mbwa!, jamaa akagoma kutoka room na kusema hatoki hadi msamaha wake ukubaliwe!, demu akamwambia, usipotoka nakuitia mwizi!, jamaa akagoma, demu akapiga yowe la mwizi na kilichomkuta ni kifo, by mob justice.
Incident nyingine kama hiyo ilitokea tena, nikajaribu kuwazuia watu wasiue kwanza, angalau tuulize nani kaibiwa na kaibiwa nini!, watu wenye uchu wa kuua wakataka kunigeukia mimi kwa kunipa kipigo eti ndio natetea wezi!, nikawakumbushia tukio la kifo cha yule kijana aliyesingiziwa mwizi, japo hawakutulia waliendelea kupiga ila at least nilifanikiwa to save his life japo alishapigika sana!. Kiukweli japo Mabibo Hostel ni jamii ya wasomi wa chuo kikuu, lakini kwenye mob psychology, wana loose all senses of reasoning na kuachana kabisa na utu, na badala yake kugeuka wananyama kabisa!, hawana tofauti yoyote na wale wahuni wa Manzese!.
Poleni kuibiwa, but its shame mwizi wa kuku kupigwa hadi kifo au kuchomwa moto huku watu wamehamasika na kushangilia kuitoa roho ya binadamu mwenzao kwa wizi wa kitu kidogo kama kuku!, huku mujizi ya rrasilimali zetu, kama yale mabilioni ya EPA, yakiachwa bila kufanywa chochote huku serikali yetu, ikiyaomba majizi hayo kurejesha kile ilichokwapua as if waliazima tuu ile mihela!.
Pasco.