Nukuu ya ndg Polepole darasa la itikadi na uzalendo tawi la UVCCM Mabibo Hostel

Egnecious

JF-Expert Member
Jul 8, 2015
875
960
*NUKUU ZA NDG. HUMPHREY POLEPOLE KATIKA DARASA LA ITIKADI NA UZALENDO - TAWI LA UVCCM MABIBO HOSTEL UDSM*

05 Januari 2018

1. "Vijana wa CCM lazima muwe mstari wa mbele katika masomo, kuwa na nidhamu na bidii ili muwe mfano bora kwa wengine" Ndg. Polepole

2. "Serikali yetu imetenga pesa nyingi kwaajili ya Mikopo ya wanafunzi wa Vyuo Vikuu na kati ya Mwaka 2015 -2018 chini ya uongozi wa Ndg. Magufuli limekuwepo ongezeko kubwa la bajeti ya Mikopo ya wanafunzi wa juu karibu asilimia 500% na CCM itaendelea kuisimamia Serikali yake ili Changamoto za Mikopo zilizopo ziishe" Ndg. Polepole

3. "CCM tunataka kuendelea kuwanoa na kuwazatiti Vijana wetu kwa hoja na maarifa na kwa kuanzia tumeanza kwa ujenzi wa Chuo Kikuu cha Uongozi cha Mwalimu Nyerere, na vipo vyuo vya Kikanda ambavyo ni Chuo Cha Chama cha Kaole - Kanda ya Mashariki, Chuo cha Tunguu - Kanda ya Zanzibar, Chuo cha Ihemi - Nyanda ya juu kusini na Chuo cha Katunguru - Kanda ya ziwa" Ndg. Polepole

4. "Itikadi ni ujumla wa mawazo, fikra, misingi, maono, malengo na uzoefu wa muda mrefu ambao unatutaarifu namna ya kuenenda na kuishi" Ndg. Polepole

5. "Mwalimu Nyerere alisema Ujamaa ni usoshalisti wa kitanzania na sio wa Karl Marx na katika misingi ya Taifa la kijamaa ni muhimu shughuli zetu zote za kijamii, kiuchumi na kisiasa zitambue utu, usawa na haki za watu" Ndg. Polepole

6."Kwenye jamii ya kijamaa lazima tukatae kupe, watu wanaonyonya wengine na kwenye ujamaa hatukatai matajiri ila lazima wawe matajiri ambao hawanyonyi wengine, hawakwepi kodi na wanasaidia wengine kufanikiwa" Ndg. Polepole

7. "Chama na Serikali tutaendelea kutengeneza mazingira mazuri ya kuzalisha ajira nyingi zaidi, lakini lazima Vijana msichague kazi za kufanya mtafanikiwa" Ndg. Polepole

8."Serikali ya CCM imefanya na inafanya mambo makubwa ya maendeleo kwa wananchi ikiwemo ujenzi wa Reli ya SGR, ununuzi wa Ndege, Ujenzi na ukarabati wa meli, ujenzi wa Zahanati, Vituo vya afya na Hospitali za Wilaya, utolewaji wa Mikopo isiyo na riba na mengi mazuri naomba muendelee kuiunga Mkono Serikali ya CCM na kuwa nayo bega kwa bega" Ndg. Polepole

Katika Darasa la Itikadi na Uzalendo Ndg. Polepole amekabidhi kadi za uanachama wa CCM kwa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es es salaam 380 waliojiunga na CCM leo.

Imetolewa na,

*IDARA YA ITIKADI NA UENEZI*
*CHAMA CHA MAPINDUZI*

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom