Mwitikio wa Baraza, wale waliotemwa na Mengineyo

Mwitikio wa Baraza, wale waliotemwa na Mengineyo

Katika hali inayotia matumaini ,mkuu wa serikali kwa mujibu wa NEC, Jk ametangaza serikali mpya ambapo J.P.Magufuli amerudi ofisi yake ya zamani iliyompa umaarufu. Magufuli amerudi wizara ya Ujenzi iliyoundwa baada ya kuua Wizara ya Miundombinu. Naibu waziri Harisson Mwakyembe,naisi katibu mkuu ni Patric Rutabanzibwa. Kweli hii ni "solid ministry" Dr.Magufuli karudi penyewe,ama kweli 'kichaa kapewa rungu' sina maana nyingine ila ni kwamba kakabidhiwa "rungu" analojua kutumia kwa umahiri mkubwa. Pia prof.ANA Kajumlo Tibaijuka kapewa makazi,ni dalili nzuri. Kwa aya tu wananchi wanaona kuwa kikwete katumia familia yake ktk kampeni ili akwepe mafisadi kwenye nafasi za uwaziri,kwa ili amejitahidi, Jk sasa atakuwa peke yake kwenye serikali kuu kati ya list ya mafisadi "list of shame" ni maendeleo mazuri. Kwa wizara zingine sina neno kwa sasa maana ni sura mpya ila kama kawaida jk anaweza kuunda tena baraza jipya baada ya miaka2 kama kawaida yake. Mzee sita kapewa Afrika mashariki ,kapozwa ila mama 6 kawekwa pembeni. Binafsi simkubali JK ila kwa baraza ili Nampongeza. Na mwisho namshauri amuondoe makongoro Mahanga maana wananchi hatuna imani naye. JK mkoa wa dsm sasa uweke mkuu wa mkoa msomi,mpaka sasa ilikuwa ikipokezana kutoka kwa darasa la7 mpaka fomu4. Weka msomi apange mji huu. Ni ayo tu,tunasubiri katiba mpya na tume huru!
 
wana JF mwenye orodho yote ya hizo wizara na mawaziri wake plz tuwekeeni javinii

mbona orodha imetolewa kwenye hiyo thread nyingine? au jaribu michuzi, ndiyo kazi yake
 
Nakuomba hurudi kundini,ushirikiane na wana Chadema wenzako.Kuendelea kuimba wimbo wa ccm kunakumaliza kisiasa na wenyewe awana shukrani.Umri unaruhusu na uwezo bado unao.
 
Mawaziri waliotemwa,kwenda kukaa beki bencha bungeni hawa....

Prof.Juma Kapuye
Prof.David Mwakyusa
Prof.Peter Msolla
Mh.Chiligati
Mh.Summari
Mh.Seif Khatibu
Mh.J.Wanjancha
Mh.H Chibulunje.....

Kama kuna aliyesaulika ongezea....
 
kwani kwenye hiyo orodha kuna umakini gani? mbona baraza limekuwa kubwa kuliko la awali? nilidhani walikuwa wanajitahidi kuojipanga kutekeleza kilio cha wananchi wengi kuhusu ukubwa wa baraza la mawaziri na kuchambua hoja mbali mbali. kuchelewa huku watu wengi walitafsiri kwamba wanapunguza baraza na kwamba ilihitaji restructuring ya serikali, amabayo tungeelewa kwamba inahitaji muda.

Kwani kulikuwa na makubaliano ya kupunguza baraza? Mbona mnataka kuingilia kazi ya Rais? Ni uamuzi wake na chama chake kupanga safu kwa jinsi wanavyoona ni bora na kwa manufaa ya nchi.

Hii ni Serikali yake, Anatekeleza ilani ya chama chake, hamwezi ku-influence chochote katika uundwaji wake.

Tulio wengi tumeridhika sana na hili baraza. Ni kazi nzuri.
 
angalau kuna mwonekano wa jeshi la miavuli kurudi na kuna mabadiliko aliyoona alichemsha kuyabadili na amerudia muundo wa Mkapa
 
Ndugu wana JF nimelisikiliza baraza la mawaziri kwa umakini mkubwa hivi Nahodha na balozi Swedi kagasheki nani alipaswa kuwa waziri wa mambo yandani?
je,Sitta na mwakyembe ndo wamenyamazishwa??
je vijana walioingia wanatosha???


Kwa kweli vijana bado. Kiu kama alitaka kuigusa apotea pale alipo mrudisha Hawa Ghasia na Sophia Simba hv wa nini wale???? huyo mahanga nae hana muda maana anayo kesi ya kujibu kwa kura alizoiba.
 
Mwakyembe na sitta tunategemea wakapambane huko waliko! Nadhani mapambano bado yanaendelea. Wasiwe wamaneno tuu wapambane kwa vitendo sasa.
 
Ninahisi nchi inaelekea kwenye hatari. JK anaanza kujihami kwa kuweka watu watakao mtii kwa lolote atakalowaagiza hata kama ni kuuwa raia.

Someni alama za nyakati.
 
Baada ya kutangazwa baraza la mawaziri leo hii napata maswali mengi kichwani,
JK anataka kuarchive nini?Je yale yote yaliosemwa na wapinzani kayapuuza au!
Kweli kibaya kibaya tu...
Mbona kapatia kwenye wizara ya Ujenzi??kumbe akiamuwa anaweza,so ni kiburi na Ubinafsi wake tu!
 
Mkuu huku tuyaache hayo bwana wacha wafanye kazi sasa
 
Nakuomba hurudi kundini,ushirikiane na wana Chadema wenzako.Kuendelea kuimba wimbo wa ccm kunakumaliza kisiasa na wenyewe awana shukrani.Umri unaruhusu na uwezo bado unao.

Kwa wenye kuona mbali wanamwangalia kwa macho ya ziada maana unafki kwenye masuala yahusuyo nchi ni hatari sana
 
Amejitahidi kuliko baraza lililopita. Kiu hawezi kuikata kwa sababu chaguo langu lilikua Dr.Silaa
 
Kumbe mmemjua Chiligati kuwa huwa mtu wa kukurupuka kwenye kauli zake!!!!!!!!!!
 
Back
Top Bottom