Mwitikio wa Baraza, wale waliotemwa na Mengineyo

Mwitikio wa Baraza, wale waliotemwa na Mengineyo

Mimi nna wasiwasi na huyu Mlungu mbunge wa chunya mbeya , kwanza bwana huyu shule yake mwenyewe imewahi kufungiwa na baraza la mtiani kwa kosa la wizi wa mitihani ukiacha hilo pia ana kasfa kibao za utapeli mjini mbeya sasa kumkabizi mtu kama huyu unaibu waziri wa wizara ya elimu hapa naona badala ya kujenga jk ana bomoa :embarrassed:
 
Ngeleja nilishamdelete tangu mwanzo hanipi furaha hata kidogo, nakumbuka alipopewa madini kwa mara ya kwanza alisema kwa nguvu zote kuhusu wadanganyika kutoyafaidi but hadi leo hajaleta jipya!
 
Ni mpaka pale uwaziri utakapoacha kutolewa kama zawadi au ajira kwa maswahiba ndipo tutaondokana na huu upuuzi!
 
duu.... kwahiyo from Marcopolo sasa bodi ni Yutong

Ofcousf ni mvinyo uleule ktk chupa mpya. Hakuna cha kushangaza hapo, huwezi kutegemea machungwa toka kwenye mdimu. Kosa lilifanyika tarehe 31 October kuacha mdimu (ccm) kuendelea kuwepo.
 
BarazaJipya.jpg
Kikwete.jpg
1. Ofisi ya Rais (Utawala Bora) Mathias Chikawe

2. Ofisi ya Rais – Mahusiano na Uratibu: Stephen Wassira
3.Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma Hawa Ghasia
4. Ofisi ya Makamu wa Rais – ( Muungano): Samia Suluhu
5. . Ofisi ya Makamu wa Rais – (Mazingira) Dr. Terezya Luoga Hovisa
6. Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge): William Lukuvi
7. Uwekezaji na Uwezeshaji Dr. Mary Nagu
8. Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) George Huruma Mkuchika
Naibu: Aggrey Mwanri
Naibu: Kassim Majaliwa
9. Wizara ya Fedha Mustapha Mkulo
Naibu: Gregory Teu
Naibu: Pereira Ame Silima
10. Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Shamsi Vuai Nahodha
Naibu: Balozi Khamis Suedi Kagasheki
11. Wizara ya Katiba na Sheria Celina Kombani
12. Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernard K. Membe Naibu: Mahadhi Juma Mahadhi
13 . Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dr. Hussein Ali Hassan Mwinyi
14. Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Dr. Mathayo David Mathayo
Naibu: Benedict Ole Nangoro
15. Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof. Makame Mnyaa Mbarawa
Naibu: Charles Kitwanga
16. Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Prof. Anna Tibaijuka Naibu: Goodluck Ole Madeye
17. Wizara ya Maliasili na Utalii Ezekiel Maige
18. Wizara ya Nishati na Madini William Mganga Ngeleja 1. Adam Kigoma Malima
19. Wizara ya Ujenzi Dr. John Pombe Magufuli
Naibu: Dr. Harrison Mwakyembe
20. Wizara ya Uchukuzi Omari Nundu
Naibu: Athumani Mfutakamba
21. Wizara ya Viwanda na Biashara Dr. Cyril Chami
Naibu: Lazaro Nyalandu
22. Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dr. Shukuru Kawambwa
Naibu: Philipo Mulugo
23. Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dr. Haji Hussein Mpanda
Naibu: Dr. Lucy Nkya
24. Wizara ya Kazi na Ajira Gaudensia Kabaka Makongoro Mahanga
25. Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Sophia Simba
Naibu: Umi Ali Mwalimu
26. Wizara ya Habari, Vijana na Michezo Emmanuel John Nchimbi
Naibu😀r. Fenella Mukangara
27. Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki Samuel John Sitta
Naibu Dr. Abdallah Juma Abdallah
28. Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika Prof. Jumanne Maghembe
Naibu: Christopher Chiza
29. Wizara ya Maji: Prof. Mark James Mwandosya
Naibu: Eng. Gerson Lwinge


 
Without prejudice! I dont see what was termed earlier as ethical and hardworking!....To my suprise instead of reducing the number,they have increased. That means it was to keep the older cabinet and replace the one lost in elections plus some bonuses to the chosen few! Save a few new comers like Prof Tibaijuka ,John magufuli and Dr Mwakyembe i have nothing to cheer about the new line-up!
 
rais amechagua baraza kubwa na kuna mawaziri na manaibu wengi wageni ambao rekodi zao za utendaji hazijulikani. uteuzi wa mkuchika tamisemi na maige utalii nadhani ndio utezi mbovu zaidi. kama rais amekosa mwanaccm bungeni mwenye uwezo wa kuongoza wizara ya utalii,bado anao uwezo wa kuteua mbunge kutoka ktk viti vyake 10.hii wizara inahitaji waziri anayeijua vzr sekta ya utalii. nimefurahishwa na uteuzi wa magufuli na mwakyembe ujenzi na mama tibaijuka ardhi na makazi.
 
SIASA ni mchezo mgumu. Kama ilivyo katika kandanda, aliye nje anayaona makosa, mengi. Walio uwanjani wanaujua uchungu wa game.


Jana nimemwona JK akitangaza baraza lake, si JK wa siku zote. Alikunja uso mara kwa mara. Kuna aliowakunjia uso. Wanasema; kumkoma nyani giladi. Ukitaka kumwua nyani usimtazame usoni.


Sura mpya zilikuwa nyingi. Majina mapya. Kuna majina aliyataja huku akionyesha kuwa anaowataja si watu wake wa karibu. Hakukuwa na ' mtani wangu nanihii!'


Kama kocha, kikosi kile kinaweza kufanya maajabu. Chaweza kuwa kikosi cha kujituma, maana, wengi waliongizwa kikosini ni wapya. Wanajua nje kwenye benchi kuna wapya wengine, kuna wazoefu. Wakiboronga mchezo, kuna watazamaji watakaopiga kelele majukwaani; " JK mwingize nanihii!, Mwingize nanihii!". Ndio mchezo wa siasa ulivyo, kama kandanda vile, kocha ana kazi ngumu, na walio uwanjani pia.


Habari kubwa jana; Samwel Sitta na Harrison Mwakyembe. Kwanini JK amemchezesha Harry Mwakyembe katikati pamoja na akina Jo' Magufuli na Anna Tibaijuka? Huenda hata Mwakyembe mwenyewe ameshangaa kocha kumpanga katikati. Na labda ameuliza; " Kocha nifunge wapi?"


JK atamjibu; " Funga Kote Kote! Anampima akili yake? Na Kwanini Sam Sitta katupwa wingi ya kulia? Nahofia, Sitta ataisubiri sana mipira. Mingi itaishia katikati, hataipata! Ni lazima afanye jitihada binafsi kuitafuta mipira. Na kuna watazamaji jukwaani wanaofikiri, kuwa ingekuwa busara Sam Sitta angechagua kukaa kwenye benchi kulinda heshima yake.



Wanaosema hivyo hawaujui ugumu wa mchezo wa siasa. Sitta atalazimika Ku- 'Like The Situation' - Kuipenda Hali, basi. Masikini Samwel Sitta, si huyu aliyekuwa na mhimili wake wa dola aliokuwa akiuongoza.

Na ni Sitta huyu huyu aliyepata kutamka bungeni; " Wapinzani mtaitwa hivyo hivyo, wapinzani, maana nyie mnapinga-pinga tu!". Alimjibu aliyekuwa Kiongozi wa upinzani Bungeni Hamad Rashid aliyesema kuwa wakati umefika kwa kambi ya Upinzani kuitwa ' Kambi ya Ushindani' ili kuondoa dhana ya upinzani ambayo jamii inaitafsiri vibaya.



Masikini Sitta, akiwa Spika wa Bunge alikuwa na nafasi ya kuacha legacy ya kuwezesha hoja ya Watanzania kupata Katiba Mpya na Tume Huru ya Uchaguzi ijadiliwe bungeni. Ndio, Samwel Sitta sasa atakumbukwa pia kwa kuwa Spika wa kwanza kujenga ofisi yake ya Spika kwao Urambo Mashariki. Ofisi yenye thamani ya mamilioni ya fedha za walipa kodi. Hivi alidhani Uspika ni Usultani?!

Naam. Na kwenye mchezo mgumu wa siasa kuna kinachoitwa ' Inner cabinet'. Kikundi kidogo cha mawaziri kinachoweza kukutana na Rais hata isipo rasmi. Kitapanga mikakati kabla ya kukutana na baraza zima. Kama kuna ' Inner Cainet' pale Magogoni, basi, sina hakika kama Sam Sitta na Harry Mwakyembe watakuwamo. Si ni juzi tu walikuwa ' a political loose cannons' ndani ya chama- Mizinga inayoning'inia, inapiga Kote Kote! Na bado ndani ya chama kuna hofu ya uwepo wa masalia ya ' Weapons Of Mass Political Destructions'. Anne Kilango, Ole Sendeka.....


Naam. Katika miaka ya karibuni, inaaminika kuwa Bungeni Sitta aliipa tabu sana Serikali. Bado hatujaandika, na itakuja, simulizi ya ' Mitume 12' iliyopambana na ufisadi ndani na nje ya bunge. Samwel Sitta alikuwa mmoja wa mitume hiyo. Harry Mwakyembe nae alikuwamo. Hawakujua kuwa, ni kazi ngumu sana kupambana na ufisadi kwa kelele za bungeni tu. Dawa ni Katiba Mpya na Tume Huru ya Uchaguzi. Ndio, tatizo ni MFUMO uliopo ambao nao walikuwa ni sehemu ya mfumo huo.



Katika mchezo wa siasa; adui yako usimwache nje ya hema akunanilihii haja ndogo ukiwa ndani ya hema. Mwingize ndani ya hema ananilihii haja ndogo nje akiwa ndani ya hema.



Naam. Wanaosema siasa ni mchezo mchafu wanakosea. Siasa ni mchezo mgumu, basi.


Maggid
Iringa
Novemba 25, 2010

http://mjengwa.blogspot.com
 
Maggid, kama unavyoeleza mchezo wa siasa unatafsiri nyingi sipingani na mawazo hata kidogo ila mtazamo wangu siasa ni mchezo rahisi sana kama mtawala atawatumikia wananchi wake kwa upendo, ugumu wa siasa unajitokeza pale mtawala anapokuwa na ajenda za siri, mfano unaweza ukajiliuliza je Dr. Mwakyembe amewekwa kwenye baraza la mawaziri ili aongeze tija na ufanisi wa serikali au amewekwa kama njia ya kumziba mdomo? kwani yeye sasa ni sehemu ya serikali hataweza kuhoji madhambi ya serikali. Hivyo basi siasa siku zote ni mchezo laini wanaoutia ugumu ni hawa wanasiasa wetu wenye ajenda za siri na waliokosa upendo kwa wananchi wanaowatawala.
 
asante kwa kutuletea lugha yenye maigizo ndani yake na kutuchezesha mpira tukapat burudani ya akili.ila mimi naungana na wewe hao waliopewa nafasi sasa waonyeshe kazi kuzitafuta hizo walizokuwa wakizipigia makelele ambazo kiukweli ni ngumu kuzitpata na kuzitolea maelezo.mwakyembe kazi anayo kujibu maswali bungeni wakati maswali yenyewe yatakuwa na uhozo uliokwisha fanywa na wengine kazi anayo huyu 6 na mwakyembe..
 
kwa mtizamo awamu hii amelazimika kusikiliza maoni ya vigogo wa chama na wananchi baada dhoruba lililowakumba kwenye uchaguzi.kimsingi mtandao uliomwingiza madarakani ndio uliomwangusha kwa kiasi kikubwa na hivyo basi kwa wateule hawa wapya kuna matumaini ya kurudisha imani iliyopotea kama watatimiza wajibu wao kwa umma wa Watanzania.Tatizo ninaloliona ni kuwaacha baadhi ya mawaziri walioonekana kuwa mizigo wakiwamo Prof.Maghembe,Mkuchika na Wasira ambao sidhani kama kuna mategemeo wakabadilika kwa kipindi hiki kifupi.Kazi kubwa waliyonayo ni kutimiza ahadi walizoahidi wakati wa kampeni ambazo nyingi zinaelekea kuwa mzigo mkubwa kutimizwa.Tunawatakia kila la kheri kuelekea 2015
 
:laser:Nimefurahishwa na POWERTILLER(JPM) kuwekwa Chungu kimoja na TURBOCHARGER(HM), Wakandarasi watakoma kazi kwenu.
Hapa Jembe linakwangua, pale naona Turbo linachungulia kanuni za kisheria.:target:
 
Nachelea kutoa maoni yangu hapa kwani nahisi suala la uadilifu halikuzingatiwa kwenye uteuzi.
nahisi aliyeteua ana vigezo vinavyokosekana pia
 
Joyce,
Bila Ahsante, na naamini, siasa ni burudani pia!
 
Vipi umeshtuka ndotoni au bado uko ndotoni, limekidhi mahitaji ya wadanganyika including wewe, naona umeshtukia siku hizi unapost night!!!
 
Vyombo vya Habari Tanzania vimekupoteza ndg, kama vilivyotupoteza siku ya Kupiga kura ya Uchaguzi mkuu kwa kusema watu waliojitokeza kupiga kura n wengi mnoooo! Kuumbe hata nusu hawakufika.
Pole kwa kuviamini inawezekana vinajikomba kwa wakuu wa nchi hasa wakati huu ambapo ccm inatafuta mchawi wa anguko lake
 
nimefatilia mijadala mingi kupitia Mlimani Tv, itv, star tv na vyombo vingi vya habari kwamba watu wengi wameonyesha kupendezewa na barza jipya la mawaziri.ni baraza lilojaa watu wenye uchungu wa nchi hii. hili ni moja ya baraza ambalo limekidhi haya ya watz, wasomi, watu mashuhuri na watu wenye uchungu na nchi hii wametoa maoni hayo

MS uko sawa. ama kwa hakika limekidhi haya ya watanzania na si haja. Ngoja miaka mi-5 ipite ndo tutajua kama wamekidhi au la.

Hata hivyo naomba nikusaidie kufahamu haja ya watanzania haitimilizwi kwa sura za baraza la mawaziri bali na sera zenye kuwagusa wananchi katika maeneo ya msingi ya maisha yao ya kila siku.

Je kuna sera inayoeleweka ya kufuatwa na mawaziri hawa ambayo itakidhi kweli haja za watanzania????

FOR ME, PAMOJA NA KUWA NA SURA ZINAZOKUBALIKA NA JAMII KUBWA YA WATANZANIA THE BUSINESS WILL BE AS USUAL
 
Kama tulivyotegemea, JK kasha limwaga baraza lake linalojumuisha vikongwe na Serengeti Boys/Girls, mnalionaje, tutakwenda mbele kweli?
 
Nilijua tu umeingia leo, hii mkuu tushaijadili muda kitambo. Leta nyingine, shida ya hapa mkuu lazima nikueleze, likitokea jambo lolote nchini basi elewa kuwa ni dakika tu linakuwa lishaletwa hapa jamvini sasa baada ya wiki ukileta habari kama ni breaking newz kumbe ishakuwa used utatulaumu tu. Anyways it was a good initiative. Karibu jamvini!
 
Back
Top Bottom