Mwisho wa unafiki wa Mengi!

Mwisho wa unafiki wa Mengi!

Mkuu bila shaka una yako na Mengi hivi unafikiri hizo tv zake unaangalia peke yako... Nimeangalia hizo tv zake jana na leo ikiwemo itv wameonesha habari nyingi kuhusu Mh Magufuli na kuapishwa leo na tena zilikuwa za kwanza na haitoshi waliweka kipindi maalum kuhusu Magufuli...hebu acha uongo na uchochezi alafu watu waseme ni mwana CCM...!

Uliangalia kipindi cha saa kumi na mbili jioni pale EATV jana?
 
kweli kabisa vyombo vya habari vya IPP vinaelemea upande mmoja tu wanatakiwa wajifunze uadilifu wa kutobagua kama wenzao TBC na STAR TV wanavyofanya
Teh teh kweli magamba hakuna akili
 
Mengi hakuna anayeweza kumgusa,news tycoon ameingia kila nyanja ya uchumi was nchi hii nani atamgusa? kumbuka list ya maadui zake halafu ulete mrejesho
 
Hii nchi si ya vyama vingi???? Sasa tatizo nini au mlitaka kuhodhi media zoote!
 
Ile siyo kituo cha TV cha CCM wala serikali. Mengi anafanya biashara na hapati ruzuku serikalini hivyo ana uhuru wa kuamua atangaze nini na kwa muda gani. Unafiki wa mengi ni kuwa balanced kwenye habari au kitu gani. mbona siku ya kufunga kampeni alionyesha na UKAWA wakakosa airtime
 
Mzee huyu kwa miaka mingi aliweza kuchanga karata zake vizuri kwa kuuma na kupuliza lakini mwaka huu baada ya kuuma amebanwa pumzi na hivyo basi anashindwa kupuliza.

Hili ni funzo kubwa sana kwa wote wanaoishi kwa unafiki.

Pole sana kwa Mengi kwani mwisho wa unafiki ni mwaka huu...uliyemkataa kuwa rais wa JMT ndio anaapishwa leo.


HATA KAMA NI VIPOFU NITAWAONESHA TU!

Kaanzishe TV yako na wewe tuone utakavyo operate acha kumpangia mtu na mali yake.
 
Mengi hakuwa fair alikuwa ni purely Team lowassa ...mbaya zaidi hadi leo anaonesha kutoridhishwa na matokeo na anatumia media kuonesha Tanzania kuna vurugu.

Nimeangalia EATV jana kati ya habari zaje muhimu kitaifa eti kuapishwa rais haikuwepo!!

Mzee mnafiki sana na kama alizoea kukwepa kodi mwisho wa hilo ni leo.

Nimegundua kuna watu wapuuzi sana ndiyo maana biashara za bongo zinakutavkila uchwao.

ITV ni tasisi inayofanya kazi kwa taratibu na malengo waliojiwekea kwa uweeledi
 
Mengi hakuwa fair alikuwa ni purely Team lowassa ...mbaya zaidi hadi leo anaonesha kutoridhishwa na matokeo na anatumia media kuonesha Tanzania kuna vurugu.

Nimeangalia EATV jana kati ya habari zaje muhimu kitaifa eti kuapishwa rais haikuwepo!!

Mzee mnafiki sana na kama alizoea kukwepa kodi mwisho wa hilo ni leo.

TBC na Star TV walikuwa sahihi kuwa upande wa CCM pekee? Kama Star Tv ni halali, basi na ITV ni halali. Vinginevyo tunahaki za kuwahoji au kuwalalamikia wote.
 
kosa lake haku declare interest kwamba yy ni mwanachama wa ukawa, ITV ilitumika kuhujumu CCM kwa kuipendelea chadema na kufanya proganda za chadema kuiangamiza ccm. Hiyo mtu yeyote mwenye akili timamu anajua hilo.
Dialo yeye hana kosa maana anajulikana ni mwana CCM na ni mwenyekiti wa mkoa wa CCM.

well said mkuu.. sijaona tu kitufe cha kulike nngekupa za kutosha
 
Wengine tunajiuliza
1. Magazeti mangapi Tz yanamilikiwa na vyama vya siasa?
2. Radio ngapi zinamilikiwa na vyama vya siasa?
3. TV ngapi Tz zinamilikiwa na vyama vya siasa?
4. Je chombo cha Habar kisichomilikiwa na Chama chochote cha siasa kina uhalali wa kutoa Habar zinazopendelea Chama fulani tu cha siasa?
 
Mleta mada usidanganye na kudanganyika!

Katika hali ya kipekee wakati wa kampeni; sote tumeshuhudi wazi vyombo vya Mhe Mengi vikiuhabarisha uma kwa kuzingatia misingi ya haki na usawa kwa kila mgombea.
Pamoja na hali kuwa hivyo eti kwa kuwa kashinda yule mnayempenda hapo mnadai kwamba kulikuwa na unafki katika vyombo vya habari vya mzee Mengi !!
Jambo hili linaibua maswali mengi kuliko majibu yake.

Ndugu zangu jaribuni kufikiri kidogo kuwa iwapo angeshinda mhe Lowasa je watu hawa wanaolishabikia hili wangeliwasifia TBC na Star Tv kwa kusimama katikati kama kweli ni mahakimu wa haki wanaopaswa kuliamua hili?

Huu kama si unafiki uliozeeka na kupofuka ni nini basi?
Ndiyo, unafikiwa kumkeea aliyeweka usawa katika habari na kuwaacha wale waliolala na kuegemea upande mmoja mwanzo mwisho!!
Loh! Hii nchi ina mauzauza jamani !!
 
Mengi hakuwa fair alikuwa ni purely Team lowassa ...mbaya zaidi hadi leo anaonesha kutoridhishwa na matokeo na anatumia media kuonesha Tanzania kuna vurugu.

Nimeangalia EATV jana kati ya habari zaje muhimu kitaifa eti kuapishwa rais haikuwepo!!

Mzee mnafiki sana na kama alizoea kukwepa kodi mwisho wa hilo ni leo.

Kwani magufuli aliapishwa Jana au kaapishwa Leo?
 
Back
Top Bottom