Mwisho wa Penzi.

Mwisho wa Penzi.

Kwnn miaka yote hiyo hukuwahi kumtolea posa? Acha aende hata km ningekuwa mm ningeenda tu
 
Sioni kosa la huyo dada! Wewe uko naye kwenye mahusiano tu miaka 3+ kaja huyo anatoa mahari ulitaka afanyeje? Asubiri hadi miaka 8 kama AY halafu ukibadili mawazo? Kiufupi ukiwa na mtu aliyeko tayari kuoa/kuolewa achana na huyo wa ahadi chukua fursa
 
Kwa kuwa alikuambia ukweli kosa ni lako mwenyewe ulitakiwa kabla miaka 4 haijatimia uwe umeisha tangaza ndoa.
Mwenzako alikuwa mjanja ww alikufanya spare. Tyre kama jamaa akirudi toka Ulaya na kumuacha basi awe amejiandaa kisaikolojia sasa wewe hukuusoma mchezo ila kiuungwana tafuta mwingine utapata bila shaka.
 
Kwa kuwa Mungu hunena mara moja,Naam, hata mara ya pili, ajapokuwa mtu hajali.
15 Katika ndoto, katika maono ya usiku,Usingizi mzito uwajiliapo watu,Katika usingizi kitandani;
 
Kama kakuachia mali poa nikadhani kaondoka nazo hapo ningekwambia mtafute ila poa jipange tu wakati mwingine usimzoee mtu kiasi hicho bakisha kidogo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndg achana naye huyo,alikuwa busy time kwako alikuwa hana true love2u sasa cha kufanya tulia kidogo kaza moyo mwanaume baada ya muda utakaa flesh,kisha tafuta demu mkali oa endelea na maisha sawa!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habari...
Msaada wenu tafadhari, Nimekuwa kwenye mahusiano kwa miaka 3 sasa,mimi na mpenzi wangu tumefanya mambo mengi pamoja ikiwemo kununua kiwanja,kuanzisha mradi wa pamoja lakini Juzi kaniambia Mimi na yeye BAASI.
Na vyote tulivyofanya,kununua pamoja vyote haitaji wala hataki tugawane.
Nimefanya uchunguzi ikiwemo kuuliza kwa Ndugu zake wawili watatu ninaowafahamu kama kuna tatizo nililomfanyia ndugu Yao wamekana kufahamu kwa nini amebadilika.
Jana cousin wake kanitonya kuwa Dada Yao alifanya kikao siku 3 zilizopita na ndugu zake na kuwa Jamaa yake alikuwa masomoni Nje karudi na Anataka kwenda kutoa mahali kwao hivyo kaamua aniache Mimi.
Ukweli nilipomtokea mwanzoni mwa 2015 alikili kuwa kwenye uhusiano na jamaa yake yupo masomoni nje ya nchi na atakaa miaka 4.
kinachoniuma tayari nimemzoea lakini pia mali tulizonunua yeye pia alitoa pesa yake kitendo cha kusema haitaji ni kama analipa gharama za muda alionipotezea.
Nimepanga niuze vyote tulivyonunua pamoja nianze Upya maisha ya upweke.

Sent using Jamii Forums mobile app
Naelewa nini maana ya mapenzi na nini maana ya kupenda pole sana kwa magumu yote unayopitia jipe nia ya kumsahau naamni utashinda uwe na,moyo mkuu
 
Back
Top Bottom