Mwisho wa Penzi.

Mwisho wa Penzi.

JembePoli

JF-Expert Member
Joined
Jul 14, 2015
Posts
1,324
Reaction score
999
Habari...
Msaada wenu tafadhari, Nimekuwa kwenye mahusiano kwa miaka 3 sasa,mimi na mpenzi wangu tumefanya mambo mengi pamoja ikiwemo kununua kiwanja,kuanzisha mradi wa pamoja lakini Juzi kaniambia Mimi na yeye BAASI.
Na vyote tulivyofanya,kununua pamoja vyote haitaji wala hataki tugawane.
Nimefanya uchunguzi ikiwemo kuuliza kwa Ndugu zake wawili watatu ninaowafahamu kama kuna tatizo nililomfanyia ndugu Yao wamekana kufahamu kwa nini amebadilika.
Jana cousin wake kanitonya kuwa Dada Yao alifanya kikao siku 3 zilizopita na ndugu zake na kuwa Jamaa yake alikuwa masomoni Nje karudi na Anataka kwenda kutoa mahali kwao hivyo kaamua aniache Mimi.
Ukweli nilipomtokea mwanzoni mwa 2015 alikili kuwa kwenye uhusiano na jamaa yake yupo masomoni nje ya nchi na atakaa miaka 4.
kinachoniuma tayari nimemzoea lakini pia mali tulizonunua yeye pia alitoa pesa yake kitendo cha kusema haitaji ni kama analipa gharama za muda alionipotezea.
Nimepanga niuze vyote tulivyonunua pamoja nianze Upya maisha ya upweke.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Piga moyo konde, moyo utauma lakini baadae utapona tu. Bora amekupiga kibuti alfajiri hii kuliko ingekuwa mchana, jioni au usiku wakati ushamuoa na wototo pia mmejaliwa.
 
Back
Top Bottom