Mwisho wa Dunia ndio mwisho wa Jua litakapofikia tamati. Je, kuna mtu anaweza fika miaka bilioni 5,000,000,000 nusu umri wa Jua uliobakia?

Kaka yake shetani

JF-Expert Member
Feb 1, 2023
3,606
8,734
Sayansi na dini zinapishana kidogo kwenye maono na mitazamo.

Siwezi kukataa dini zinavosema wala sayansi inavosema,vitu ambavyo vinaweza kunipa ukweli ni huu msemo kuwa "chenye mwanzo lazima kiwe na mwisho".

Tuje kisayansi maana hapa ndio upande wangu:

Fahamu katika nyota unazoziona angani zote zimezaliwa na zimekufa na zingine zipo mbioni kufa.

Maisha ya nyota si rahisi sana kushuudia yanavokufa kwanza umri wa nyota nyingi aziendani na umri wako kushuudia zilianzaje na kufaje mubashara.

ni kweli katika ulimwengu wa anga unapozungumzia nyota basi tambua nyota zimebeba mkusanyiko wa sayari na mengine yanayozunguka huku yakiakisi vinavozunguka.

Nyota ndio kitovu cha sayari leo zinazo onekana angani nyingi.unapozungumzia nyota unazungumzia Jua au majua kama nilivoeleza mwanzoni.

Hapa nitaeleza Jua letu linalotupa mchana na kuziona sayari zengine wakati wa usiku au ingekuwa tunaishi kwenye nyota nyengine basi ili jua wetu huko tulipo nalo tungeliona nyota kama nyota zengine.

Vitu ambavyo vinaleta mtazamo ni ili:
*Dunia imeanza mda mfupi.

Naposema muda mfupi simaanishi kuona muda bali leo teknolojia tunazotumia leo zingeanza nyuma sana yani hizi smart,tv,ndege,internet,Jf na maendeleo mengine yangeazia miaka hata milioni iliyopita angalau wakati dunia kitaalamu ina umri wa miaka bilioni 4.5.

Umri wa dunia unapimwa kupitia miamba ya mawe iliyopimwa kuona ilikaa mda mgani na mwambwa huu ulipatikana cananda ndio mwamba mzee tokea dunia kuanza.

Kwa hiyo hapa kuna mwanzo na mwisho wa maisha ya dunia.

*
Tafiti za kisayansi kuhusu nyota (jua).

Kugundulika kwa tafiti za wanasaysnsi kuhusu kufa na kuzaliwa majua kunatokana na chunguzi zinazo fanana baada kuchunguza nyota ambazo zenye majua ambayo yamezaliwa,yanaendelea,yana karibia kufa na yaliyokufa.

maxresdefault.jpg


Watu wa Dini wanamitazamo yao ila kisayansi jua litakavo zidi kuzeeka ndivo litazidi kubadilisha dunia kuwa kwenye joto sijui hapa dini watasema moto kuwaka.

Kisayansi ukanda wa unaofanya mwanadamu na viumbe kuishi sayari utasogea na syari yetu kuwa karibu kabisa jua limetanuka tayari.
inddddex.jpg


Kisansi inaitwa habitable zone:
image_3870e-Habitable-Zone.jpg


DINI IMESHINDWA KUJUA LINI AU NI SIKU GANI ILA SAYANSI IMEELEZA KUWA NI USHAIDI WA UMRI:

Hapa ndio tunapata jibu kuwa mwisho wa dunia utakuwepo ila kuwepo kwake basi mwanadamu atakuwa ameshaondoka kutafuta makazi mengine ambayo mimi na wewe kuwepo hakuna.

Ninaposema dunia sio ya muda mrefu ni kweli kabisa kuthibitisha chenye mwanzo lazima kiwe na mwisho hapa. Je, mwisho mwanadamu hatakuwepo wakati ikifika mwisho

imcxdcages.jpg


Mwisho:
maisha ya jua letu ndo mwisho wa maisha yetu hapa dunia ila tutakuwa sayari nyengine
inxcddcdex.jpg
 
Dini zinasema jua lima mwisho, ambao ndio mwisho wa dunia. Science nayo inasema jua lina mwisho, na kwakuwa kuna uhusiano mkubwa kati ya jua na dunia, basi ni wazi kuwa, mwisho wa jua ndio mwisho wa dunia. Ukichunguza hapo utabaini kuwa science na dini vinakwenda pamoja; maana pande zote mbili zinasema jambo moja, kwamba kutakuwa na mwisho wa dunia. Kupishana kwa (science na dini) litakuwa ni suala la muda wa mwisho wa dunia. Kwa upande wa scince, wao wanakwenda na namba (mahesabu), lakini mahesabu hayo yamejaa dhana (assumptions) na makadirio mengi sana. Makadirio hayo either yatarudisha nyuma au kupeleka mbele mwisho wa dunia. Kwa hivyo ni bora kuiamini dini, ambayo inasema hakuna mtu aijuaye siku ya mwisho wa dunia!
 
Kabla ya jua kufa hakuna kiumbe wala sayari itakayokuwa hai kushuhudia maana miaka bilioni kadhaa wakati jua linapoanza kuingia katika hatua za kifo chake litatanuka na kumeza sayari na takataka zote zinazoizunguka na litaongezeka joto maradufu kuwa "red giant" kabla halijageuka kuwa "dwarf star"
 
Mwisho wa dunia ni mungu peke yake anaejua hata malaika hawajui Sasa hao Wana sayansi ni kitu gani
Yeye anaongelea mwisho wa jua, yaani jua litakapoishiwa nishati yake inayoliwezesha kuwaka Kwa nguvu za kiatomiki. Wewe umemjibu Kwa mujibu wa Biblia.
 
Dini zinasema jua lima mwisho, ambao ndio mwisho wa dunia. Science nayo inasema jua lina mwisho, na kwakuwa kuna uhusiano mkubwa kati ya jua na dunia, basi ni wazi kuwa, mwisho wa jua ndio mwisho wa dunia. Ukichunguza hapo utabaini kuwa science na dini vinakwenda pamoja; maana pande zote mbili zinasema jambo moja, kwamba kutakuwa na mwisho wa dunia. Kupishana kwa (science na dini) litakuwa ni suala la muda wa mwisho wa dunia. Kwa upande wa scince, wao wanakwenda na namba (mahesabu), lakini mahesabu hayo yamejaa dhana (assumptions) na makadirio mengi sana. Makadirio hayo either yatarudisha nyuma au kupeleka mbele mwisho wa dunia. Kwa hivyo ni bora kuiamini dini, ambayo inasema hakuna mtu aijuaye siku ya mwisho wa dunia!
Kiuhalisia, hakuna mtu atakayeshuhudia mwisho wa dunia kwa macho makavu ya nyama!
Maana mwisho wa dunia utatokana na majanga asilia yatakayosababisha ukomo wa binadamu.
Kwa mfano jua likitoweka, ama kuisogelea dunia hakuna kiumbe kitakachobakia.
 
Back
Top Bottom