Mzawa_G
JF-Expert Member
- Feb 27, 2014
- 667
- 1,467
Angani kumetawaliwa na makundi mengi ya nyota yenye idadi isiyoweza kusemeka huku zimeendelea kutuacha na maswali mengi sana katika mawazo yetu kutokana na umbali baina ya nyota hizo na tulipo sisi huku duniani
Dunia yetu ni moja ya sayari iliyopo katika mfumo wa nyota unaofahamika kama solar system hii inamaanisha kwamba nyota yetu ambayo ni jua ina jumla ya sayari nane na magimba madogo madogo mbalimbali yaliyomo ndani yake
Kama mtu atakuwa yupo mbali sana na mfumo wetu wa nyota jua basi atakuwa anaona nyota inayowaka ambayo imebeba kiasi cha sayari nane kwa ujumla
Jambo hili ni sawa na sisi hapa duniani kwetu tunavyoweza kuona baadhi ya nyota nyingi angani bila kutambua pengine tunatizama majua ya viumbe wengine katika eneo lengine kabisa la ulimwengu wetu
Kama tunavyofahamu asilimia kubwa ya nyota nyingi zina sayari zake haijalishi ni aina gani za sayari kwa maana kama tunavyofahamu kuna aina mbalimbali za sayari ambapo kuna zile zilizo na uso mgumu yaani kama ilivyo dunia yetu na zile zilizojawa hewa ndani yake mfano kama ilivyo sayari ya Jupiter au saturn ambazo hazina sehemu yoyote ile ya kukanyaga
Kwa chunguzi zilizoweza kufanywa hadi sasa zimebaini kuwa baadhi ya mifumo mengine inafanana sawa sawa na mfumo wa nyota Jua letu na zina sayari ambazo kwa kiasi fulani zimafanana na sayari yetu dunia ila bado hatujaweza kufahamu kama zinaweza kuwa na viumbe au lah
Nyota iliyokaribu zaidi na mfumo wetu wa nyota Jua ni mfumo wa nyota unaofahamika kama Proxima centauri ambapo upo umbali wa miaka ya mwanga 4.2
Mwaka mmoja mwanga ni sawa na umbali wa kilomita trillioni 9.4 yaani kama utawasha chombo chako cha hapa duniani kitabidi kisafiri umbali wa kilomita trillion 9.4 ili kiweze kufikia umbali unaoweza kusafiri mwanga kwa mwaka mmoja
Tunafahamu kasi ya mwanga ni 300,000 km kwa sekunde
Mwanga ndio kitu kinachosafiri kwa kasi sana ulimwenguni
Sasa kwa kasi ya mwanga utaweza kuchukua miaka 4.2 kuweza kufika katika mfumo wa nyota iliyokaribu zaidi na nyota Jua yetu ambao unaofahamika kama Proxima centauri , umeona kulivyo mbali
Moudyswema
Gerald
geraldchristopher1@gmail.com