Mwisho wa Daudi Ballali

Mwisho wa Daudi Ballali

huu sio uthibitisho. huwezi kusafiri amerika kutuletea picha ya kaburi tu tukuamini. tumia akili za mwanahabari anayeijua kazi yake.

well said mkuu! Waandishi wetu wengi utafiti unawashindaga. Analeta picha ya kaburi!!!?
 
We ulitakaje?? Achukue mifupa afanya DNA?? Yeye ni muandishi kaishia hapo

Unaelewa maana ya habari za utafiti wewe au unalinganisha na habari za msafara wa kinana na nape? Je kilichompeleka marekani nikupiga picha makaburi nakutuletea kama habari? Tatizo vijana wa lumumba mnafikiria kwakutumia matumbo.
 
Kaburi pekee siyo uthibitisho...Leteni video ya mazishi na ionekane halisi! mbona mnaficha.?

Mwaka huu mbona watatafutana na habari zao za kutupoteza. Yani hapo ndiyo nachoka kwamba kwasababu walimwoneshwa kaburi basi kakubali ndugu yetu alifariki.
 
Bado mwandishi hajafanikiwa kutuaminisha kuwa balali alifariki. kuna maswali mengi ambayo hayajawahi kujibiwa. gazeti la mananchi linazidi kujipotezea heshima kwa jamii. siku hizi gazeti hili linafanya kazi kama gazeti la habari leo au daily news.
 
Unaelewa maana ya habari za utafiti wewe au unalinganisha na habari za msafara wa kinana na nape? Je kilichompeleka marekani nikupiga picha makaburi nakutuletea kama habari? Tatizo vijana wa lumumba mnafikiria kwakutumia matumbo.

kazoea habri za udaku kuweka picha za bongo muvis utafti kwake ni jambo jipya
 
Haka kanchi kaajbu kweli kweli, yaani picha ya kaburi ndio uthibitisho? kwahiyo na mimi nikiiba pale Bank mabilioni ya pesa then ndugu zangu wakasema nimekufa na kutengeneza kaburi nzuriiiiiiiiiiiiiiiiiiii basi itakuwa imetosha kuwa uthibisho nimekufa. NYAMBAFU ZAO KWANZA KWANINI HII STORI IMEKUJA MUDA HUUUUUUUUUU?
 
Siku hizi hili Gazeti silielewielewi, linazidi kuja na tamthilia za ajabu ajabu


Nyie magamba hamuwezi kulielewa hili gazeti kwasababu linawakumbusha machungu ya ufisadi wenu mliowafanyia wananchi!! Endelea kusoma gazeti lenu la Uhuru!!
 
Swala la kuona kaburi haitoshi kujiridhisha kwamba aliyezikwa ndio mwenyewe(original),kama alikufa kweli iweje kusiwe na picha za maombolezo,maziko,wawakilishi wa familia,kuaga mwili etc.
Hata hiyo anwani ya kaburi si wanawweza kuandika kaburi lolote tu kwaajili ya picha na kuaminisha watu? Eti kaburi limetafutwa kwa siku 2! Kaburi la mtu maarufu kama huyo litafutwe siku 2? Au ndio zilikuwa siku za kuandika anwani kwenye kaburi la mtu mwingiene? Waweke picha inayoonesha makaburi mengine hapo isije kuwa wamepaint kaukuta fulani kimtindo tena ikiwa hapa hapa bongo! Nchi ya kusadikika hii ni vigumu kuwaamini!
 
Alikufa kwa Ebola au? maana magonjwa haya ndiyo vifo ni vya kufichwa mtu asisogelee......Strange
 
Haka kanchi kaajbu kweli kweli, yaani picha ya kaburi ndio uthibitisho? kwahiyo na mimi nikiiba pale Bank mabilioni ya pesa then ndugu zangu wakasema nimekufa na kutengeneza kaburi nzuriiiiiiiiiiiiiiiiiiii basi itakuwa imetosha kuwa uthibisho nimekufa. NYAMBAFU ZAO KWANZA KWANINI HII STORI IMEKUJA MUDA HUUUUUUUUUU?
Hakuna haja ya kutengeneza kaburi. Unakwenda tu pale Kinondoni unajichagulia kaburi moja wapo na kuweka maandishi yako ya muda kwaajili ya picha tu halafu unayafuta au unakwenda kwenye vile vijiwe vya wakereketwa wa CCM uanandika anwani ya "marehemu" kisha unapiga picha ukimaliza unafuta. Unaweza kutumia stika au temporary colours kama zile wanazojipaka watu mwilini kule Bra71li. Huyu "mwandishi Mchunguzi" atawaponza wengi!
 
well said mkuu! Waandishi wetu wengi utafiti unawashindaga. Analeta picha ya kaburi!!!?
Ajabu! Yaani picha za mtoto wa boksi akiwa hai na mfu tunaoneshwa lakini mtu maarufu kama Governor hata picha ya hospitali alikolazwa haipatikana kutona na ugonjwa aliokuwa anaugua wa EPA ambao kamera huwa zinaungua akipigwa picha akiwa hai au mfu!
 
Huu ni upuuzi mwingine wa kucheza na akili za watanzania wa karne ya 21 kwa mitindo yao ileile ya karne ya 20,hakuna kitu hapo nd'o kwanza kwa michezo yenu hii ya kuigiza mnazidi kujiumbua.Ballaliawe hai au amekufa niscandal mbaya sana,kwani bado ana deni kubwa kwetu watz ambalo sijui atalilipaje? Usalama wa taifa acheni upuuzi huu.
 
Kiongozi wa juu nchi hii.. Aliyeshika nafasi kubwa ya taasisi kubwa na nyeti nchi hii..... akazikwa kimya kimya bila ndugu zake kushiriki mazishi...


Upumbavu mwingine bana!!

-------- mwenyewe umapenda kutimia misiba kujijenga kisiasa hivi familia ya wangwe mliitembelea lina au ile ya mtema
 
tamthilia inaanza na mkazi wa Iringa. Hii kama hadithi za Shigongo. Na huyo mkazi shida yake nini na makaburi!!! Tunakumbuka ambavyo watu hata majirani hawakuruhusiwa hata kusalimiwa wafiwa halafu huyu mwandishi kanjanja analeta utumbo wa photoshop ya kaburi.
 
Hakika hawa ndio waandishi tulionao tanzania eti hyo nayo ni habari ya uchunguzi. Inasikitisha kuona mtu anatumia garama kubwa kiasi h4cho then anatuletea habari isiyokua na utafiti hata chembe au hyo safari alilipiwa na serikali ya ccm nini?

kama kalipiwa kila kitu kuna shida
 
Back
Top Bottom