Mwigulu: Watanzania msikimbie nchi tutarekebisha makosa

Uongozi ni pamoja na kuchunga ulimi wako usikupotoshe. Lakini ulimi hauwezi kutamka kile usichopanga kusema akilini. Madiru amewatangazia walipakodi wasiotaka kulipa Kodi za Tanzania wahamie Burundi. Ni tamko linalohitaji ujasili kulitamka hadharani kwa kiongozi tena Waziri la fedha.

Mwelekeo wa mkuu wa nchi ni kuifungua na kuisimamisha nchi kiuchumi na hii kauli aliitoa hadharani na Madiru alisikia. Najiuliza tu, kama hawa walipakodi wakihamia Burundi huyu waziri
atakusanya kodi kutoka vyanzo gani?.

Hivi tunarudi kutegemea misaada ya wafadhili kuendesha nchi? Najiuliza pia, hivi mkuu wa nchi hii alilenga nini kuwaasa waliohamishia biashara nje ya nchi warudi nyumbani huku waziri wake mkusanyakodi akikejeli watu wanaopaswa kuchangia kujenga nchi wahamie nchi jirani?

Nadhani kuna kitu hakiko sawa. Viongozi hawaongei lugha moja.

Jana tu Madiru ameendelea kula matapishi yake kwa kuwaomba watanzania wasikimbie nchi wakati yeye ndie aliyetoa ushauri huo, hivi anadhani anaongoza watoto wa chekechea?....... Du nchi inayumba Sasa!.
 
Unatumiwa na shetani. Mungu hawezi kuwa na furaha kiumbe wake anapoteswa kwa kusingiziwa. Hiyo yako ni ya kishetani. Jiulize mara mbili sababu ya furaha yako hiyo.
Furaha yetu ni kama furaha yenu mafisadi baada ya kifo cha magu ,mcheki mkwele alivyo nenepa ghafla baada ya kifo cha jpm
 
Kazi ya Mungu haina makosa. Uhuni wa CCM ni laana. Ushetani wako unakupa furaha mtu mwingine anapoonewa bila sababu.
Furaha yetu ni kama furaha yenu mafisadi baada ya kifo cha magu ,mcheki mkwele alivyo nenepa ghafla baada ya kifo cha jpm
 
Wafanyabishara wamekimbilia zambia siyo kwasababu ya kodi tu bali sera zinazo badilika badilika (uncertainty policies)
 
Kama kuna mawaziri wajinga basi huyu ni namba moja

Mimi nafikiri wananchi sisi ni wajinga zaidi, tunatozwa kodi za kipumbavu, kisa tumedanganywa mama anafuatilia, eti tumekaa kimya na wanaendelea kututoza. Kwanini kama anafuatilia asingesimamisha?
 
Mimi nafikiri wananchi sisi ni wajinga zaidi, tunatozwa kodi za kipumbavu, kisa tumedanganywa mama anafuatilia, eti tumekaa kimya na wanaendelea kututoza. Kwanini kama anafuatilia asingesimamisha?
Kwaongezeko hili la tozo serikali na mitandao ya simu vyote vinakosa pesa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…