Mwigulu Nchemba ni Waziri asiye na chembe ya huruma kama Mustafa Mkulo na Basili Mramba

Fundi Madirisha

Senior Member
Jun 30, 2020
184
987
Inashangaza sana Waziri anachukua maoni ya kina Zungu na kuyapeleka kwenye baraza la mawaziri kuyajadili,kisha kuyarudisha tena bungeni wakayapitisha kwa kishindo bila huruma. Hii siyo roho ya kizalendo ni maumivu makubwa kwa watanzania wote wanaccm, wapinzani na wasio na vyama.

Waziri kwa ubabe tu inashauri mamlaka ziridhie mpango wa kinyonyaji? Na wewe kwa sababu hauna huruma kwa ubabe unatetea maumivu haya?

Unaenda kuvunja rekodi ya kina Mstafa Mkulo na Basili Mramba ambao walisema bora watu wale nyasi lakini ndege ya Rais lazima inunuliwe na wala hawakujali hisia na maumivu ya watu, sasa hivi wako wapi? Unapokua kiongozi jifunze kuishi maisha wanayoishi wenzako kwa uhalisia tusitafute sifa kuwaumiza wasiokua na uwezo.

Mpaka sasa sina imani na Mwigulu Nchemba na wala simpendi, asijiengue kwenye hili eti hakupitisha kodi hizi peke yake, kwani mapendekezo ya mipango yote ya kodi anaandaa nani?
 
Wanaojaza mafuta kwenye bei nafuu wahamie wakaishi hukohuko

Huyu ndiye mchumi.

Huyu ndiye mzalendo.

Huyu ndiye alitia nia ya Urais.

Hafanyi utafiti.

Haunganishi Watanzania.

NB: Anataka kuinua uchumi.
 
Serikali haifanyi maamuzi yake kukufurahisha wewe peke yako.

Kuna wakati maamuzi yatakufurahisha huku mwingine yakimkasirisha.

Mtazamo wako ndio muamuzi!
 
Back
Top Bottom