MAPUMA MIYOGA
JF-Expert Member
- Jan 30, 2013
- 3,792
- 2,370
Katika Kijiji cha Kisana kata ya kisiriri, kulitokea bwana mmoja kwa jina La Sembe Malua. Aliwahi kuwa mwenyekiti wa kijiji kama sikosei (maana mimi sikuwa naishi huko wakati huo) ambaye alifanya vema na akawezesha kiji kupata zahanati.
Bwana Sembe Baadae alihamia Chama cha CUF 2010 akagomea udiwani kata ya kisiriri na kwa kweli alileta picha kubwa kuwa ccm inakataliwa na wananchi. Ingawa matokeo hayakuwa mazuri kwa upande wake Sembe, aliacha nguvu ya upinzani ikikuwa kwa kasi ya ajabu. mapema baada ya Uchaguzi, sisi kama vijana tulimshauri ahamie CHADEMA maana tuliona nguvu ya CHADEMA inaongezeka kila kukicha. Sembe Malua akakua kisiasa na kufikia kuwa Mwenyekiti wa wilaya wa CHADEMA Iramba. CHADEMA ikazidi kukua Iramba. hali hii ilimtisha Mwigulu na kujaribu mara kadhaa kumshawishi arudi ccm lakini alishindwa kwa kuwa Bwana Sembe alikuwa na Imani na CDM pia wananchi walikuwa wanamtaka awe CDM na sio CCM.
Mapema kati July-september 2012 Kule Iramba, katika kijiji cha Kisana (Kinakumi) alikuja bwana mmoja maarufu kwa jina la manyu nyau akitokea Dare salaam. Huyu bwana alikuja kwa ajili eti ya kumtoa/kumrudisha mtu mmoja anyesadikiwa kupotea kimiujiza miaka taktribani mitatu iliyopita.
Manyau nyau akaja na mbwe mbwe nyingi na wapambe wake (waliopotelewa na ndugu) wakidai kuwa HASANI (aliyepotea) atapatikana si muda mrefu kwani alichukuliwa kimiujiza na yupo kwa wachawi hapo kijijini.
Wakazi tukaanza kushangaa mbona hatumuoni Hasani leo siku ya pili, mara siku ya tatu, baadaye manyau nyau akaanza kutaja majina ya watu flani kuwa ni wachawi hapa kijijini na hawa watu kimsingi wanajulikana miaka mingi na wanaogopeka hapa kijijini. lengo Likaanza kupotea (kumrudisha Hasani). Cha ajabu na kushangaza zaidi Sembe Malua akahusishwa katika mambo haya. Eti na yeye ni mchawi, kwa uelewa mdogo wa wananchi na hasa ikichagizwa na yeye malua kutojitokeza katika maandamano yale ya Manyau nyau ikatafsiriwa kuwa kweli na yeye ni mchawi. familai yake ikaanza kuwindwa na wananchi na akatengwa na kijiji. MALUA akakosa mwelekeo maana amehusishwa na uchawi. familia yake ikawa hatari na akakimbilia Igunga kwa Muda.
Kwa takribani week 2 ikawa Hasani, manyau nyau na wananchi wakiandamana sambamba na manyau nyau kuona kama atamrudisha Hasani. Mara polisi waje wamchukue kwa sababu eti hana kibali cha kufanya kazi ile pale. Baada ya week kama mbili hivi alirudi Dar eti anaenda kuongeza dawa na akawaambia wenye mtoto watafute Pesa (700,000/=) kwa sababu akirudi Hasani atatoka na yeye achukue ujira wake.
Akarudi manyau nyau lakini si kumtoa Hasani ila na porojo. Mara MWIGULU NCHEMBA akaja akitokea Nzega, akafnya na mkutano na wananchi waliokuwa wakiandamana kusubiri Manyu nyau amtoe Hasani, akapingana na polisi na DC kuhusu manyau nyau kufanya shughuli yake pale kijijini, tena bila kibali. Baadae wote DC, Manyau nyau na polisi walienda Kiomboi (Wilayani) na kisha manyau nyau alirudi tena jana yake akawaambia wananchi kuwa atarudi baada ya week moja Kumtoa hasani-Hadi leo Hasani hajaonekana wala manyau nyau. Mara baada ya Mwigulu, Malua akiwa bado katengwa tukasikia eti malua anahamia CCM na tayari ameshapewa Kadi ya uanachama na Mwigulu, kisha amekuwa huru hajatengwa tena na jamii. Hali hii binafsi naitafsiri kama hoja hii ya kishirikina iliandaliwa na mwigulu mwenyewe akamtanguliza manyau nyau lakini lengo lao kubwa ilikuwa kumchafua Malua ili wamlegeze msimamo na kisha wamrudishe ccm, azma ambayo wamefanikiwa.
Kwa mbunge kushiriki mambo kama haya ni aibu na ni hatari kwa nchi na jimbo letu. Wanairamba tulihitaji mbunge si mpiga ramli na mtu wa kupigana kutwa nzima kutafuta wananchi wa kuiunga mkono ccm. Jimbo la Iramba wakazi hawana maji, hawana barabara na mengine mengi ya kiamaendeleo, mbunge wao anafanya kazi ya kufarakanisha familia za watu, jamii na wananchi kwa ujumla kwa ajenda za kishirikina.Huyo ndio Mwigulu Nchemba, Mbunge wa Iramba Magharibi.