Mwigulu Nchemba: Mbowe anamlipia mtoto wake chekechea tu dola 15.000 kwa mwaka

Status
Not open for further replies.

Ritz

JF-Expert Member
Jan 1, 2011
46,976
32,376
Wanabodi.

Mbunge wa Iramba na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, Mwigulu Nchemba, leo kwenye Mkutano wa CCM Morogoro, akihutubia Wananchi kasema Mbowe anasema anataka kuwakomboa masikini na kulalamika viongozi wa CCM wanasomesha watoto wao nje ya nchi kwa pesa nyingi wakati yeye Mbowe, anamlipia chekechea tu mtoto wake dola 15,000 kwa mwaka zaidi ya milioni 20.

SOURCE: HABARI STAR TV
 
Huyo kweli hamnazo, alitaka akamlipie na mtoto wake? Je ni hela za wizi kama wao au ni biashara zake? Hana hoja!
 
Mwigulu na first class degree yake bado haelewi nini watu wanaongea! The issue is not about how much you have but rather how you got the money? Ni kwa mtindo wa vijicent, EPA, Deep Green? au kuwa kupitia magezeti, a night club!

Lakini kinachonichekesha ni contradiction ya CCM, wanalalamikia hela za Mbowe, lakini hapo hapo wanaponda aina ya biashara anazofanya!!! Si hawa hawa CCM wamekuwa wanaongelea biashara ya ukumbi wa disco kama biashara uchwara? Mwenzao hachagui kazi na hela kapata, tofauti na wao wanavamia bank kuu na kuiba hela!
 
Katika uzi kama huu ndio utakapowajua CDM, yaani kama wana akili za kushikiwa, wanatetea kila jambo!

Hivi kwa akili zenu, ada kwa mwaka chekechea karibu milioni 20 useme haina shida?
 
Huyo kweli hamnazo, alitaka akamlipie na mtoto wake? Je ni hela za wizi kama wao au ni biashara zake? Hana hoja!

Mapenzi yenu kwa chama yasiwafanye kuwa vipofu, 20 M kwa chekechea kwa mwaka tena TZ ni pesa nyingi sana, kwa mtu anayedai kuwatetea watanzania
 
Wanabodi.

Mbunge wa Iramba na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, Mwigulu Nchemba, leo kwenye Mkutano wa CCM Morogoro, akihutubia Wananchi kasema Mbowe anasema anataka kuwakomboa masikini na kulalamika viongozi wa CCM wanasomesha watoto wao nje ya nchi kwa pesa nyingi wakati yeye Mbowe, anamlipia chekechea tu mtoto wake dola 15,000 kwa mwaka zaidi ya milioni 20.

SOURCE: HABARI STAR TV

Hao viongoz tunawapigia kelele kwakua wanatuibia mbowe n zake so acha amlipie.
Mwigulu huwez fananisha alikotoka mbowe na alikotoka mtu km Pinda au Jeikei.
Leten hoja za msingi. Sawa kalipa milion hata mia,ameiba?nyi si ndo mmeshika dola tuambien?hamna haya nyinyi?hila zenu zinanifanya nizid kuwachukia.
 
Mbowe hayuko serikalini anajulikana ni mfanyabiashara tena wa mali ya kirithi,hao wenzetu wa serikalini wanaiba pesa za walalahoi na kodi zetu kujiletea utajiri wa kutisha!Namshauri huyu mkware akaombe msamaha kwanza igunga ile dhambi bado inamzunguka!!!akaombe radhi kwa yule mume wa yule kada!!
 
Hoja yetu watanzania pesa za mbowe anapata wapi na viongozi wa CCM wanazipata wapi? kuwa na pesa si kigezo cha kutowakomboa wa TZ issue ni kwamba zimepatikanaje? Mbowe ni zake za wana CCM ni za wizi. watafute hoja nyingine. Mbowe peta na hela zako lakini hawa CCM tunataka pesa zetu za walipa kodi warudishe.
 
Katika uzi kama huu ndio utakapowajua CDM, yaani kama wana akili za kushikiwa, wanatetea kila jambo!

Hivi kwa akili zenu, ada kwa mwaka chekechea karibu milioni 20 useme haina shida?
Haina shida kama hizo hela za mbowe ni za halali..... We una wasiwasi na hela za freeman au??
 
Shule gani? IST, French School? au gani.......
Kwa mwaka si mbaya kama ana uwezo wa kumlipia, kwani Mwigulu wa kwake wanasoma wapi?
 
Nadhani umeangalia Startv ya nchi nyingine.
Katika startv ya Mwanza Tanzania, Lameck Madelu amesema Mbowe anamlipia mwanae USD 10,000 sawa na Tsh. 15,000,000
Kusoma haujui hata kusikia na kuona nako huambui kitu??

Muda si mrefu haya maneno yako utayameza Star TV wameona wengi sio mie na wewe! au humjui Mwigulu Nchemba?
 
Huku ni kukosa sera na kubaki kubwatuka tu. Mbona hawezi kuhoji juu ya Fedha za EPA, RICHMOND, TWIGA WALIOTOROSHWA, N.K...?
 
Wanabodi.

Mbunge wa Iramba na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, Mwigulu Nchemba, leo kwenye Mkutano wa CCM Morogoro, akihutubia Wananchi kasema Mbowe anasema anataka kuwakomboa masikini na kulalamika viongozi wa CCM wanasomesha watoto wao nje ya nchi kwa pesa nyingi wakati yeye Mbowe, anamlipia chekechea tu mtoto wake dola 15,000 kwa mwaka zaidi ya milioni 20.

SOURCE: HABARI STAR TV

Mbowe hizo pesa alizonazo ni za Baba yake na pia aliisaidia Nchi wakati wa Uhuru; Nyerere anamfahamu hata Mlezi wa CCM anafahamu Jinsi Mzee Mbowe alivyofaifanyia Nchi yetu.

Hakuingia kwenye siasa alibaki kwenye Biashara zake; kwahiyo hakuchota toka serikalini kama Jamaa walioko serikalini sasa hivi, wana mali ndiyo wanaruhusa ya kuitumia. Na tunaiona kama Machame hotel, Na Disco Club ilioko Dar pia Gazeti

Sasa tukiuliza Lau ana nini mpaka kuwa na Majumba South Afrika lakini hajajenga Mwanza?

Rais wetu kapeleka watoto kusoma Malawi

Mafisadi wengi ndani ya CCM...

Angejaribu kujisafisha yeye Mwenyewe aache Matusi na kuvaa skafu ya bendera ya Taifa ni kosa
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom