Mwigulu Nchemba: Mbowe anamlipia mtoto wake chekechea tu dola 15.000 kwa mwaka

Status
Not open for further replies.
Mwigulu na first class degree yake bado haelewi nini watu wanaongea! The issue is not about how much you have but rather how you got the money? Ni kwa mtindo wa vijicent, EPA, Deep Green? au kuwa kupitia magezeti, a night club!

Lakini kinachonichekesha ni contradiction ya CCM, wanalalamikia hela za Mbowe, lakini hapo hapo wanaponda aina ya biashara anazofanya!!! Si hawa hawa CCM wamekuwa wanaongelea biashara ya ukumbi wa disco kama biashara uchwara? Mwenzao hachagui kazi na hela kapata, tofauti na wao wanavamia bank kuu na kuiba hela!

Akiwa hachagui kazi tutampaje nchi kabisa na trillioni zetu azishike?
 
Mr. Zero,
Mie utanionea bure sio maneno yangu aliyosema ni Mwigulu Nchembe.


Ritz,

Kwa hiyo hizi page 11 kujadili hii kitu ilikuwa ni kupoteza muda siyo........... ndiyo maana kuna watu wamehoji ni Mbowe yupi lakini halikujibiwa. Halafu wote tunajua kuwa Mwigulu ni mropokaji inawezekana yamemtoka tu hata ahakumbuki alikuwa anasema nini. Maana jamaa inaelekea hata hiyo 1st class wanayoisema inaelekea ilikuwa ya kuegesha tu!!!
 
Mapenzi yenu kwa chama yasiwafanye kuwa vipofu, 20 M kwa chekechea kwa mwaka tena TZ ni pesa nyingi sana, kwa mtu anayedai kuwatetea watanzania


ifike mahali tujadili hoja kwa uzito wake badala ya kujadili watu. Mbowe anafanya biashara zake kwa ajili ya familia yake. kodi anazolipa ndio mgawo wake kwa umma. sasa kama ana uwezo wa kulipa hiyo ada kutoka vyanzo halali tatizo liko wapi? Tatizo la kimfumo tulilo nalo TZ ni ile kuaminishwa kwamba umaskini ndio uadilifu kumbe sio.. tunacholalamikia viongozi wengi wa CCM na serikali yake wanalipia watoto wao ada kubwa kwa hela za rushwa ambazo hawajazitolea jasho na zinaongeza umaskini wa waTZ... Open your eyes.....
 
Akiwa hachagui kazi tutampaje nchi kabisa na trillioni zetu azishike?

Viongozi hawako pale kushika hela zetu.............. hii ni dhana potofu amabayo CCM wametujengea. Ndiyo maana tunaona kupata madaraka Bongo ni kuula/kuukata/kuuchinja........ na si kutumikia wananchi.

Kiongozi anatakiwa kusimamia matumizi mapato na matumizi ya pesa zetu. Kama Mbowe ameweza kusimamia biashara zake na kutajirika then this is the man kuliko kuhangaika na hawa maskini ambao juzi walikuwa wakuu wa wilaya leo wanamagolofa masaki!!
 
Katika uzi kama huu ndio utakapowajua CDM, yaani kama wana akili za kushikiwa, wanatetea kila jambo!

Hivi kwa akili zenu, ada kwa mwaka chekechea karibu milioni 20 useme haina shida?
Kwa wewe mwenye akili mingi, ungeongelea suala la msingi linalohusu nchi la je, analipa kodi inavyostahili? Suala la ni namna gani unatumia kipato chako ni haki ya msingi ya binadamu, haihojiwi popote labda tu kama matumizi yako yana uvunjaji wa sheria. Tatizo la Mbowe ni kumpeleka mwanae shule anayoipenda? Mbona viongozi wengi tu wa CCM akiwemo mwigulu ni wacheza kamari wazuri pale New Africa Casino? Na wengine wamesomesha vimada wao na kutelekeza watoto wao kama somebody wa mabarabara (bintiye na kimada wake walisoma pamoja CBE), wao matumizi ya mabilioni ya kodi wakitumia kwa anasa ruksa sio? Maige kanunua jumba la 700 milion lakini toka 2009, kalipa kodi 200,000/- (Provision tax, nenda TRA Temeke kuna file lake), mkichunguza wabunge wengi wa CCM hawana sifa za kuwa wabunge (Ni wakwepa kodi). Mnatetea wavunja sheria kwa very cheap political propaganda, shame on you.
 
Mwigulu hujui familia ya akina Mbowe walianza saka ngawila toka enzi za uhuru!
Sasa wewe kama familia yenu imeibuka ivi karibuni then unataka jifananisha na Mbowe imekula kwako!
Imagine kumiliki kitu kama Bilicanas ktk ya mji si mchezo lazima uwe una historia toka miaka ya 1960 kamasio 1950s
 
Katika uzi kama huu ndio utakapowajua CDM, yaani kama wana akili za kushikiwa, wanatetea kila jambo!

Hivi kwa akili zenu, ada kwa mwaka chekechea karibu milioni 20 useme haina shida?

Issue sio CDM, issue ni siasa ya maji taka wanayotumia CCM. Mbowe pesa anazo siku nyingi kwa biashara zinazofahamika, hao wengine je? Wametoa wapi kama sio kuiba mali za umma?
 
Nsisitiza PHD yako ni empty box, wapi katika post yangu au ya mwanzilishi wa uzi imemtaja mbowe mwizi? umeona una phd lakini unatoka nje ya mada!!?

Mkuu unaimanisha PhD? Kama ndivyo utakuwa unahitaji kwanza uongeze sana daraja la elimu uweze kumuelewa Tumbiri maana hata kulink mawazo ya mtu na context husika huwezi.
 
Mapenzi yenu kwa chama yasiwafanye kuwa vipofu, 20 M kwa chekechea kwa mwaka tena TZ ni pesa nyingi sana, kwa mtu anayedai kuwatetea watanzania

Mbona mna wivu... Point ni kwamba Elimu ya hapa ni Mbovu, Waalimu wana mgomo baridi.. Sasa Mbowe kama ana Hela za kwake binafsi kuna tatizo gani kumsomesha mwanae hata kwa 100Mil? Je hao wanaolangua madini yetu na kujinufaisha mbona hamuwasemi??

Embu watu ambie Mbowe tangu ameanza Siasa miaka ya 1990 hadi leo ametumia SH ngapi? kuwaelimisha waTZ?

Hawana Point Kabisa naona mnatokwa na Povu tu... Pale alipo hachukui hata senti tano kutoka bungenu hela zote zinaenda Hai kwenye halimashari yake... Tuambieni ni wabunge wangapi CCM wanapeleka Posha na Mishahara yao kwa wananchi?
 
mimi hawa jamaa wa cdm yaani wacha tu....ufisadi wa ccm wanaupigia ukelele lakini wa cdm au wao ni Miungu watu............kwa njia hii wakipata madaraka watasema zamu yao ya kula imefika na hakutakuwa na uwajibikaji wowote ule.....

Pesa za Mbowe zinakuhusu nini nyinyiem, Mbona hamtaki muzungumzia Rasilimali za Nchi hii... Hivi unaweza kutuhumiwa kwa uwizi wa rasili mali za nchi hii the ukaja na hoja nyepesi eti Mbowe anasomesha mwanae kwa 20Mil? Nadhani hata matahira hapa hawatawaelewa.

Issue hapa ni CCM wajenge hoja kwa nini Bajet ya serikali inategemea wahisani kwa asilimia 30?????? Na je kwa nini MTZ ndiyo anaongezewa Kodi kila siku ile hali wakoloni aka wawekezaji wakiendelea kutesha kwenye Grace periods za miaka mitano isiyoiisha???
 
Inawezekana kuna mahali imetajwa sijabahatika kusoma, ni shule gani hiyo iliyotajwa? Tutatoana macho ukute hakuna hata huyo mtoto anayesomeshwa huko!
 
Bruno Kims


Ukiwa Mpinzani ama Mtawala sio kupinga ama kusifia kila kitu
- KAMA KWELI MH. MBOWE ALILIRUDIA LILE GARI KIMYA KIMYA napinga na ntaendelea kumpinga kwani alituaminisha kuwa hatolitumia ili kupinga posho na matumizi yasiyo ya lazima.

Wenye Shida ni Hao Waliompatia Hilo Gari Na Kuacha Kutumia Hizo Hela Kununua madawati ya Shule!! Hapo ndio Tuanze Kujadili!!
 
Kuwa CDM si kuwa DULL minded like ur.... fruitless, thinking 00%.... huu ugonjwa huu.... kiongozi tunayemueweka frontline ..... Analipa 15,000 USD chekechea hapo hajapata KITI KIKUU.... ndio mfano wa kuigwa...? Don't tell me fedha zake... Shut up... We are looking IMAGE he tries to reflect to us wananchi atakaye tuongoza.... shame to him... Shame to u dull minded & kipofu usiye ona hili.... Ooh shame 2 u all msiepinfa hili....
Shame to u for looking a poor candidate ambae ataiba fedha za umma ili apeleke watoto wake wakasome ulaya! Tunahitaji kiongozi aliyejitosheleza kifikra na kipesa na sio omba omba wanaopiga magoti kwa wawekezaji ili wapate 10% za uwekezaji,shem to them!!
 
Ulitaka akulipie wewe Mwigulu? Mlishaharibu mfumo wa elimu na chama lako mnataka wasome shule zenu za kindez ili muwadominate milele tumestuka
 
Kama Nchemba kaiba jina la mtu mwingine ili atumie vyeti visivyo vyake haina haja ya kumtilia maanani
 
Nawafahamu watoto wa Mbowe, hakuna anayesoma nursery school. Lakini hiyo familia ya akina Mbowe ni ya kitajiri -- tena utajiri halali, sio kama wa wakwere fulani wanaohangaika kujitajirisha sasa kwa kutumia mgongo wa ofisi kuu.
 
MIMI SIONI TATIZO mtanzania yeyote kutumia fedha zake kwa manufaa ya familia yake, cha muhimu hapa ni je hiyo fedha ni halali? kama ameipata kwa misingi ya haki kwangu mimi sioni tatizo mtu kumpeleka mtoto wake kwenye shule bora.
TATIZO ni kama tutampa nchi mtu halafu akatujengea vishule dhaifu halafu yeye kwa kutumia kodi za wananchi anawapeleka watoto wake kwenye shule za gharama.
 
Nikijua tu Kuwa ni yule yule Lameck MKumbo, huwa naanza kusinzia na kuona Aibu kuwa huyu ndio mbunge wa jimbo ninalotoka tena mwenye 1st class degree, sisi wengine tuliosoma kayumba degree sijui tutasema nini sasa?? Hizi Degree za viongozi wengi wa ccm kuna haja zikachunguzwa, huenda ni zile za mjomba njoo uchukue degree yako iko tayari.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom