Mwigulu Nchemba "Kumlima" Barua Kinana...?

Mwita Maranya

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2008
Posts
10,565
Reaction score
7,993
Salam ndugu wanaJF.

Miaka ya hivi karibuni tumeshuhudia vijana wengi wakishawishika kujiunga katika shughuli za kisiasa hapa nchini. Mwamko huo wa vijana kujiunga katika shughuli za kisiasa umepelekea vyama vya kisiasa kutafuta namna bora ya kuwavutia na kuwashawishi vijana kujiunga na vyama vyao.

Kutokana na vuguvugu kubwa la vijana kujihusisha na masuala ya siasa, vyama vya siasa hapa nchini hasa vyenye ushindani mkubwa hapa nchini CHADEMA, CUF na CCM vimejikuta vikilazimika kuwateua vijana mahiri katika vyama vyao katika nafasi za juu za uongozi wa kitaifa.

Chadema walimteua Zitto Kabwe kuwa naibu katibu mkuu bara, CUF kwa upande wao wamemteua Julis Mtatiro kuwa naibu katibu mkuu bara huku CCM nao wakimteua Mwigulu Nchemba kuwa naibu katibu mkuu bara. Wote hawa ni vijana walioaminiwa na kuteuliwa na vyama vyao ili watumie ushawishi wao na umahiri wao katika kuwavuta vijana wengi zaidi kujiunga na vyama vyao. Kitu kimoja cha kufurahisha ni kwamba vijana hawa ambao wote ni mahiri sana katika vyama vyao, wote wameteuliwa kushika wadhifa unaofanana/unaolingana-Naibu katibu mkuu!!!

Vyama vyetu vya siasa vimekuwa vikipitia katika vipindi tofauti tofauti vya mlipuko na hamasa za kisiasa, na hasa vinapokuwa vikubwa na kujikusanyia wafuasi wa kila aina; vijana, wazee, akina mama, watu wa makamo, wataalamu waliobobea katika Nyanja mbalimbali na watu wengine wa kawaida. Katika kukua huku kwa vyama vya siasa changamoto mbalimbali zimekuwa zikijitokeza siku moja hadi nyingine. Wajibu wanaokuwa nao viongozi wa chama husika ni kuwa na uwezo wa kupambana, kuhimili na kukabiliana na changamoto zozote zinazojitokeza kwa kushirikiana (collective responsibility).

Ili kushadidia hoja yangu naomba nimtumie naibu katibu mkuu wa ccm ndugu Mwigulu Nchemba. Pamoja na kwamba sina mapenzi yoyote na ccm na sijawahi kuwaunga mkono kwakuwa sasa ni zaidi ya miaka 50 wanatuongoza tanguntupate uhuru lakini tunachoshuhudia ni wananchi kuendelea kuwa masikini lakini pia hali ya usalama wa wananchi na mali zao umeendelea kuwa shakani kwani tumeshuhudia mauaji ya hapa na pale kwa wananchi wasiokuwa na hatia.

Mauaji mengine yamekuwa yakifanywa na vyombo vya dola lakini pia mauaji mengine yamekuwa yakifanywa na majambazi kama ilivyotokea kwa Dr. Mvungi hivi karibuni pamoja na Prof. Mwaikusa na watanzania wengine wengi ambao wameuwawa kikatili kwasababu ya ulegelege wa serikali ya ccm kushindwa kuwahakikishia wananchi wake ulinzi wa maisha yao na mali zao.

Pamoja na kushuhudia ccm ikipita katika misukosuko mingi yenye migawanyiko mingi ndani ya chama lakini viongozi wake wameweza kumudu kuwa na “mshikamano” wa kushangaza, hata kama unaweza kuuita ni mshikamano wa kinafiki lakini umekuwa ukiwasaidia kukivusha chama chao katika changamoto mbalimbali.

Mara zote tunapokaribia uchaguzi mkuu wa nchi au uchaguzi ndani ya ccm tumekuwa tukishuhudia makundi mengi yakijitokeza kushindana na hata kufikia mahali pa kutishia uhai wa chama chao, hadi baadhi ya watu kudhani kwamba ccm inameguka kama si kupasuka. Pamoja na kuwepo na makundi ya uchaguzi kila mara lakini kama nilivyotaja awali ni kwamba makundi hayo yamekuwa yakiendesha siasa za hatari lakini bila kukiumiza chama chao.

Mathalani siku za hivi karibuni tumeshuhudia makundi mbalimbali yakijipanga kwa ajili ya uraisi wa JMT mwaka 2015. Tumeshuhudia kundi la Edward Lowasa wakiwa “busy” kumuuza mgombea wao, na hivi karibuni tunasubiri kuona watu wakienda kula nyama choma Monduli. Kwa upande mwingine kuna kundi la Bernard Membe, na upande mwingine tena kuna kundi la Samwel Sitta. Pia kumekuwa na “miungano”ya makundi mbalimbali ambayo nimekuwa nikiyasikia yakitajwa yakijipanga kuhakikisha kwamba wagombea wao ndio wanaopata fursa ya kupitishwa kupeperusha bendera ya ccm come 2015.

Pamoja na kuwepo minyukano ya mara kwa mara ndani ya ccm lakini hatujawahi kushuhudia viongozi wa juu wa ccm; Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Katibu Mkuu, Manaibu Makatibu Wakuu na Katibu Mwenezi , mmoja wao au wawili miongoni mwao wakifanya kazi za “kiofisi” za chama chao kupitia vyombo vya habari.

Kwa mfano Mwigulu Nchemba ambaye vijana wengi sana wa ccm wanamuamini na kumtumainia sana kwamba ndiye anayeweza kuwanusuru na kipigo cha upinzani katika uchaguzi mkuu ujao wa 2015 amekuwa akitajwa kumuunga mkono Edward Lowasa. Na kwakuwa Mwigulu anamuunga mkono Lowasa basi ni dhahiri kuwa asingependa kuona mgombea wake akiendelea kusakamwa na kuchafuliwa na wanaccm wenzake wanaopingana nae ama kushindana nae.

Katika mazingira hayo ni dhahiri kuwa Mwigulu amekuwa akiwasiliana na bosi wake-Katibu mkuu Kinana katika kuwashauri au kutafuta maelezo au ufafanuzi wa mambo mbalimbali yanayokikumba chama chao. Katika kuwasiliana huko ni wazi kuwa amekuwa akiwasiliana kwa ukaribu zaidi na katibu mkuu wake Kinana na akimsaidia kwa ukaribu katika kutekeleza majukumu yake kwakuwa yeye (Mwigulu) ndiye msaidizi wa karibu zaidi kwa Kinana. Katika kuwasilaiana na Kinana bila shaka amekuwa akitumia njia mbalimbali za mawasiliano kama vile kuzungumza nae ana kwa ana, ama akizungumza nae kwa simu, ama anawasiliana nae kwa barua/barua pepe au fax na njia nyingine za mawasiliano zinazokubalika kiofisi.

Hata mara moja sijawahi kumsikia ama kumuona Mwigulu Nchemba akitoka hadharani kwenye vyombo vya habari na kuuambia umma wa watanzania aidha kupitia press release, au kupitia mitandao ya kijamii, au kupitia magazeti, au television na radaio kwamba amemuandikia rasmi katibu mkuu wake Kinana kumuomba ufafanuzi au maelekezo ya jambo Fulani linalomhusu kiongozi mmoja wa chama chao.

Pamoja na kushuhudia mashambulizi mengi dhidi ya Lowasa kutoka kwa wanaccm wenzake, tena wakati mwingine Lowasa ameshambuliwa hadharani na viongozi wakubwa wa ccm lakini sijawahi kumuona Mwigulu akitoka kwenye vyombo vya habari na kututangazia kwamba amemuandikia barua Katibu mkuu wake Kinana atoe taarifa ya kukanusha mashambulizi yaliyofanywa dhidi ya Lowasa ama akiri kwamba kiongozi huyo (aliyemshambulia Lowasa) ametoa matamshi hayo kwa niaba ya chama hivyo wanachama wa ccm na wananchi kwa ujumla watambue kuwa huo ndio msimamo wa ccm juu ya kada wake Lowasa.

Nionachoamini ni kwamba Mwigulu amekuwa akiwasiliana kwa karibu sana na katibu mkuu wake Kinana katika kumsaidia kutekeleza majukumu yake, ni dhahiri kuwa Mwigulu amekuwa akiitumia ofisi yake ya naibu katibu mkuu pale Lumumba na Dodoma katika kutekeleza majukumu yake ya unaibu katibu mkuu wa ccm. Ni dhahiri kuwa Mwigulu amekuwa akimuandikia barua rasmi za kiofisi kumhoji juu ya mambo Fulani yenye mwelekeo wa kukimuiza chama chao ama viongozi wao ama wanachama wao, lakini kama nilivyogusia tangu hapo awali sijawahi kumuona akivujisha barua zake hizo katika vyombo vya habari kwa sababu iwayo yoyote ile.

Kutokana na mazingira hayo na kutambua kwamba Mwigulu amekwisha kuchagua upande anaouunga mkono (Lowasa), lakini pia naye amekuwa akitajwa kwamba anafikiria kujitosa katika kinyang’anyiro cha uraisi (huenda ni alternative choice incase bid ya Lowasa imekwama), bila shaka amekuwa akipambana ndani ya ccm kuhakikisha kuwa jina lake na la mgombea wake hayachafuliwi bila sababu za msingi.
Kwa mantiki hiyo basi nimekuwa nikitamani sana kumuona ama kumsikia ama kumsoma Mwigulu Nchemba akitoa press release, au akiandika katika mitandao ya kijamii kwamba amemuandikia rasmi barua katibu mkuu wake Kinana kutaka maelezo ama ufafanuzi wa hoja kwamba viongozi na wanachama wa ccm wanaomshambulia “mgombea wake” hadharani kwa kumhusisha na kashfa mbalimbali za ufisadi na zinazoonyesha dhahiri zinamchafua kiongozi huyo.

Kwakuwa Mwigulu anaungwa mkono na vijana wengi ndani ya ccm, na kwakuwa vijana wengi wa ccm wanamuunga mkono Lowasa katika mbio zake za kuwania uraisi, na kwakuwa kuna baadhi ya viongozi wa ccm tena wengine wa kitaifa wamekuwa wakiendelea kumchafua Lowasa, na kutokana na kuendelea kuongezeka kwa upinzani ndani ya ccm dhidi ya Lowasa ni dhahiri kuwa muda si mrefu tutamshuhudia Mwigulu Nchemba akitujuza ni kwa kiwango gani amepambana kuhakikisha kuwa jina la mgombea wake halichafuliwi na atatufahamisha ni barua ngapi amemuandikia Kinana akimtaka atoe tamko la kukubali ama kukanusha taarifa zote zinazoandikwa ama kuchapishwa zikimshambulia Lowasa. Ninausubiri wakati huo kwa hamu sana kwakuwa muda si mrefu tutayashuhudia “maajabu” hayo yakitokea.

Nawasilisha.
 
Japo nakubaliana kwa kiwango kikubwa cha maandiko yako lakini CCM wamekuwa wakinangana mchana peupe siri za baraza la mawaziri zinatoka,siri za CC zinatoka , siri za mkutano mkuu zinatoka, sema wanastadi kubwa sana ya kujua kujikausha na wakati mwingine kukauka kama vile hakuna kilichotokea wakati mwingine wana simplify na kujibishana kwa vijembe na mambo nchi hii huwa yanayeuka kama theluji yakipita yamepita
 
Nakubaliana na wewe kwamba taarifa nyingi za ccm na serikali hata za baraza la mawaziri zimekuwa zikivuja lakini hata mara moja sijawahi kumsikia Mwigulu akitamba hadharani kwamba amemuandikia rasmi Kinana kutaka ufafanuzi wa hoja Fulani tata dhidi ya kiongozi Fulani wa ccm. Huo uthubutu hana na hajawahi kuwa nao, labda kama sasa ataanza kuwa nao.
 
Mwita Maranya,
Hongera sana kwa uchambuzi makini

Pamoja na ushamba wa kisiasa alio nao linapokuja suala la masilahi ya taifa ukichanganya na siasa zake za kifedhuli lakini huyo naibu katibu mkuu wa CCM hajawahi kufikia hatua hiyo
 
Last edited by a moderator:
Nakubaliana na wewe kwamba taarifa nyingi za ccm na serikali hata za baraza la mawaziri zimekuwa zikivuja lakini hata mara moja sijawahi kumsikia Mwigulu akitamba hadharani kwamba amemuandikia rasmi Kinana kutaka ufafanuzi wa hoja Fulani tata dhidi ya kiongozi Fulani wa ccm. Huo uthubutu hana na hajawahi kuwa nao, labda kama sasa ataanza kuwa nao.
Hiyo ni misconduct kusema naibu katibu mkuu amlima katibu mkuu barua ha ha ha vioja vya mwaka waandishi nao how can you pick that issue in such a manner
 
Mkuu huwa naziheshimu sana status zako ila hapa kidogo umeteleza,Nadhani siyo sahihi kumtumia Mwigulu katika kuhalalisha hoja yako ya kumpinga Zitto kwa kitendo chake cha kumwandikia barua Katibu Mkuu kutaka maelezo ya kina juu ya tuhuma anazobebeshwa kwamba anakisaliti Chama ukizingatia kwamba nyaraka hizo zilisemekana kutoka Makao Makuu ya Chama.Kosa lako ni pale unapomlinganisha Mwigulu ambaye siyo muathirika wa moja kwa moja(direct victim) wa character assassination campaign na Zitto ambaye ni direct victim wa hii smear campaign,Nadhani tayari ushaona wapi umeteleza.Zitto ni binadamu,ana hisia na anaumizwa na hizi scandals,Sasa unadhani kama ungekuwa ni wewe Mwita Maranya ungechukua hatua gani?Lema naye pia amechafuliwa na hizi hizi smear campaign ambazo tumekuwa tukizipiga vita siku zote na yeye amekimbilia Bungeni,amemwandikia barua Spika kutaka msaada wa kisheria juu ya kuchafuliwa kwake,Je ina maana na yeye amekosea kwa kumlima barua Spika wa Bunge?I think your whole argument is not powerful in a way.
 
Mkuu hapo nikupe like,for sure hili umuliona sahihu,umeliangalia kwa mapana,umelitafakari kwa uzito wake,Mwita nakushukuru sana,lkn kabla sijahitimisha niseme tu ya kwamba work ethics zipo mpaka kwenye chama,na discpline ni silaha kubwa kwenye mafanikio na hata kuyafanya yawe sustainable.
Mwenye masikio ayakuwa amesikia kwa andiko lako Mwita Maranya.
 
Mwita Maranya umeula wa Chuya,CMM ni mlima na CDM nikichuguu,niambie ni Mbunge gani CCM ambaye amewai kumtuhumu Naibu Katibu mkuu CCM,anajitia upofu bila sababu,punguzeni ubinafsi,mnamambo mengi ya kujifunza CCM nyie ni Chekechea tu,huu Uzi ungeleta na shabiki wa CCM kwenda CDM ungeona anatukwana,kama CDM tumeishauri ishu ya Mapato na Matumizi,ukomo,uchaguzi,eti ooh CCM mnapenda Zito!
Mwambie Lema awe na Adabu kwa Kiongozi wake,Zito sio mbunge tu kama Lema,bali ni Kiongozi wetu,plz plz naomba unitajie mbunge wa CCM anaemkashifu naibu katibu mkuu
"Tusiangalie tulipoangukia tuangalie tulipojikwaa#somo kwenu
#Ex Chadema simper aliquid novi#
 
Last edited by a moderator:
Mkuu huwa naziheshimu sana status zako ila hapa kidogo umeteleza,Nadhani siyo sahihi kumtumia Mwigulu katika kuhalalisha hoja yako ya kumpinga Zitto kwa kitendo chake cha kumwandikia barua Katibu Mkuu kutaka maelezo ya kina juu ya tuhuma anazobebeshwa kwamba anakisaliti Chama ukizingatia kwamba nyaraka hizo zilisemekana kutoka Makao Makuu ya Chama.Kosa lako ni pale unapomlinganisha Mwigulu ambaye siyo muathirika wa moja kwa moja(direct victim) wa character assassination campaign na Zitto ambaye ni direct victim wa hii smear campaign,Nadhani tayari ushaona wapi umeteleza.Zitto ni binadamu,ana hisia na anaumizwa na hizi scandals,Sasa unadhani kama ungekuwa ni wewe Mwita Maranya ungechukua hatua gani?Lema naye pia amechafuliwa na hizi hizi smear campaign ambazo tumekuwa tukizipiga vita siku zote na yeye amekimbilia Bungeni,amemwandikia barua Spika kutaka msaada wa kisheria juu ya kuchafuliwa kwake,Je ina maana na yeye amekosea kwa kumlima barua Spika wa Bunge?I think your whole argument is not powerful in a way.

Mkuu TECH WIZ huo ni mtazamo wako ambao sina tatizo nao kwakuwa ndivyo ulivyoliona.

Kulinganisha sakata la Lema na hili nililoliandika unakuwa unakosea sana. Kwanza Lema sio kiongozi wa bunge kwakuwa viongozi wa bunge ni spika na naibu wake. Pili mawasiliano kati ya mbunge na kiongozi wake wa bunge yanafanyika kwa barua kwakuwa mbunge anakuwa sio sehemu ya kutekeleza majukumu husika.

Sasa nikirudi katika hoja yako ya kuwa Zitto alikuwa ni muathirika wa moja kwa moja, nikubaliane na wewe kwamba ni kweli. Lakini hapo hapo nikukumbushe kuwa Zitto ni naibu katibu mkuu wa Chadema, na sio mwanachama wa kawaida kama sisi ambao hatuna ofisi pale makao makuu.

Kumuandikia barua katibu mkuu katika kumtaka ufafanuzi au msimamo wa chama lilikuwa ni jambo jema sana na wala mimi sijalipinga mahali popote. Nilichokuwa nahoji na kuwalinganisha viongozi vijana hawa manaibu katibu mkuu ni ile silka ya kiuongozi miongoni mwao. Kwanini alipomuandikia barua katibu mkuu akaona haitoshi akakimbilia kwenye vyombo vya habari kuutangazia umma kwamba amemuandikia barua rasmi katibu mkuu? Unafikiri Mwigulu au Mtatiro huwa hawawaandikii barua mabosi wao? lakini mbona hata mara moja hatuwaoni wakija public kutueleza kuwa wamewaandikia barua makatibu wakuu wao juu ya jambo Fulani?

Tukiacha hilo la "taarifa ya siri" mnayodai kuwa imeandaliwa na Chadema makao makuu ambapo na zitto naye ni sehemu yake, sasa nikukumbushe kuwa wakati ule wa sakata la "Ugaidi wa Lwakatare" ni naibu katibu mkuu huyo huyo wa Chadema aliyemuandikia barua Katibu mkuu wake akimtaka chama kijitenge na Lwakatare na kutaka Lwakatare atoswe, na kasha barua hiyo kuvujishwa hapa JF kwa lengo lile lile.

Sasa ukishayaangalia matukio hayo mawili ambayo hayamhusu muathirika mmoja, ndipo sasa unaweza kunielewa kitu nilichokuwa najaribu kukiwasilisha ili kwa pamoja tuweze kuona manufaa ama madhara ambayo vyama vyetu vinayapata kwa kuwekeza kwa hawa vijana mahiri katika vyama husika kwa lengo la kujiongezea ufuasi na uungwaji mkono.

Jambo hili tukilitazama katika uwanda mpana wa kichama au kitaifa ndipo unaweza kuiona mantiki ya hoja yangu. Lakini tukijikitab katika personalities tutajikuta tunarudi kule kule tunakojaribu kutoka.
 
Last edited by a moderator:
Umeandika habari ndefu sana kwa kurudia rudia, inaweza kushindwa kufikia hadhara kwa sababu inachosha.

Lakini kukujibu kwa mbaalii: JF ni mtandao wa wana mageuzi, kwa maana ya vijana wa kidijitali tunaotaka kuona mageuzi yanafanyika. CDM katika kukamata vijana imebidi ijikite sana kwenye mitandao ya kijamii (FB, Twitter, JF etc) ndio maana unaweza kuona:-

i. Katibu Mkuu wa CDM Dr Slaa ana verified account hapa JF wakati yule wa CCM Mr Kinana hana

ii. Mwanzilishi wa CDM ana verified acccount hapa JF, lakini hakuna kiongozi mkubwa kwa maana ya Mwenyekiti/Mwenyekiti mstaafu wa CCM mwenye verified acc hapa

iii. Wasemaji wa Chama Mr Tumaini Makene na Mh Mnyika wana verified acc hapa ambayo huwa wanazitumia kutoa press release za chama, Nape ana acc verified lakini huwa hatoi press release hapa JF (kwa nadra sana)

iv. Wabunge wengi wa CDM wana verified acc JF zaidi ya wabunge wa CCM

With that said, sio kosa kwa chama chetu hiki kutoa matamko kupitia mitandao ya kijamii, lengo ni kutaka hadhira lengwa ifikiwe na habari.
 
Mwita Maranya umeula wa Chuya,CMM ni mlima na CDM nikichuguu,niambie ni Mbunge gani CCM ambaye amewai kumtuhumu Naibu Katibu mkuu CCM,anajitia upofu bila sababu,punguzeni ubinafsi,mnamambo mengi ya kujifunza CCM nyie ni Chekechea tu,huu Uzi ungeleta na shabiki wa CCM kwenda CDM ungeona anatukwana,kama CDM tumeishauri ishu ya Mapato na Matumizi,ukomo,uchaguzi,eti ooh CCM mnapenda Zito!
Mwambie Lema awe na Adabu kwa Kiongozi wake,Zito sio mbunge tu kama Lema,bali ni Kiongozi wetu,plz plz naomba unitajie mbunge wa CCM anaemkashifu naibu katibu mkuu
"Tusiangalie tulipoangukia tuangalie tulipojikwaa#somo kwenu
#Ex Chadema simper aliquid novi#

Sawa sawa mkuu Adharusi huo ni uhuru wako kutoa maoni yako.

Lakini sasa nikuulize swali moja, ni lini uliwasikia wabunge wa cccm au wanachama wa ccm wakimtilia mashaka Mwigulu Nchemba kwamba anakwenda kinyume na miongozo na falsafa ya chama chao? Sitaki kusema kwamba kilichofanywa na Lema ni sahihi au sio sahihi lakini nachosema hapa ni kwamba naibu katibu mkuu wa chama unawezaje kufikia hatua ya kushambuliwa na wanachama wako ambao wewe ni kiongozi wao uliyetakiwa kuwaonyesha njia sahihi za kukijenga na kukiimarisha chama?

Unafikiri huko ccm wabunge na viongozi wao hawagombani au kuwa na misimamo tofauti juu ya mambo yao ya ccm? mara nyingi tu tunayaona lakini angalia namna uongozi wa juu wa ccm unavyosimama pamoja kukitetea chama chao.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Mwita Maranya kwanza nikupongeze kwa kutambua kuwa linapokuja swala la political crisis management lazima vyama vya upinzani vipate somo kutoka CCM. Kukaa na hii mentality ya kwamba CCM ina akili ndogo na haiweza kuongoza CHADEMA yenye akili kubwa ni hoja ambayo ni muflisi katika maeneo fulani ambayo mojawapo ni hili la internal political crisis ulilolitaja.

Kitu ninachokiona siyo kutokuwepo mawasiliano official and unofficial baina ya Katibu Mkuu na Naibu Katibu Mkuu bali ni kukosekana kwa misingi ya uwepo kwa mawasiliano hayo.

Ungewasaidia sana wasomaji wa bandiko lako kama ungejikita zaidi katika uchambuzi wa Katiba, itifaki, falsafa, maadili na kanuni za uendeshaji na utendaji ndani ya CHADEMA na hasa katika mwingiliano kiofisi.

Siamini kama Kanuni, itifaki na maadili ndani ya CHADEMA yako sawa na CCM na kama hayako sawa, yapi mapungufu yake ndani ya CHADEMA yanayosababisha Katibu Mkuu na Naibu Katibu wake washindwe kutumia njia ya mawasiliano kama ya CCM katika utendaji na utekelezaji wa majukumu yao.

Kama mapungufu hayapo, ni nani kati yao ambaye ni kichocheo katika kuvunjika mawasiliano kwa sababu mada yako imejikita kwenye matokeo ya tatizo na siyo chanzo.

Huwezi kuanza kutatua tatizo bila kujua chanzo cha tatizo, na chanzo cha tatizo kitakuwa ndani ya Katiba, Kanuni, Maadili na itifaki za CHADEMA. Ni namna gani zimevunjwa au kufinyangwa finyangwa.

Tafuta kwanza chanzo cha tatizo!.

Nimalizie kwa kusema, kutotatua tatizo ni kuongeza tatizo jingine ambalo wewe mtatuzi ambaye umeshindwa kutatua ndiyo unakuwa ni tatizo na kufanya hivyo, kunajenga precedence ya bora liende.
 
Back
Top Bottom