Mwigulu Nchemba "Kumlima" Barua Kinana...?

Mwigulu Nchemba "Kumlima" Barua Kinana...?

Dear Leader Ukweli Usemwe nimekusoma mkuu haya ni mawazo yako na unao uhuru wa kuwa na msimamo huo. Lakini nadhani umejaribu kupotosha hoja yangu kwa makusudi, najua kwamba umenielewa nilichokiandika.

ahaa haaa, Mwita Maranya bwana. Nyie ndiyo mnaowaharibu viongozi wetu kwa kutokuwa wa kweli. Unalinganishaje vitu ambavyo havilinganishwi?

i) ulishaona mjumbe wa Kamati Kuu wa CCM akimnanga Kiongozi wake kama vile Naibu Katibu Mkuu hadharani kama alivyofanya Lema?

Kwanza sijawahi kuona naibu katibu mkuu wa ccm anakuwa wa kwanza kuwalalamikia wabunge wenzake wa ccm kwenye mitandao kama alivyofanya Zitto kwa Lema.

Kwa mtazamo wangu suala la Lema kumnanga zitto lilikuwa si la kichama kama ambavyo unalitazama. Sote tunafahamu kuwa mnyukano wa Lema na Zitto ulianzia huko kwenye vikao vya ndani vya bunge, na zitto ndiye alilitoa nje suala hilo kwa kuliandika kwenye mitandao ya kijamii, akimlalamikia Lema kwa kile alichodai kumshambulia katika kikao chao cha wabunge. Kama Zitto asingeliandika kwenye mitandao ya kijamii ni wazi kuwa tusingepata fursa ya kumsoma Lema kwa kile alichokuja kuandika baadae.

Sasa labda hapa wewe uniambie hiyo busara ya Naibu Katibu Mkuu kwenda kwenye mitandao kumshambulia mjumbe wa kamati kuu aliitoa wapi? Hapo ni dhahiri kuwa yeye mwenyewe naibu katibu mkuu ndiye alimchokoza Lema, na alichofanya Lema ni kujibu mapigo, sasa kwanini tena ionekane yeye ndiye kaonewa kwamba anachafuliwa?

ii) Ulishaona viongozi wa Mkoa wa CCM wakasambaza waraka wa kumchafua kiongozi wao kama vile Naibu Katibu Mkuu kama alivyofanya Kileo ambaye ni Katibu wa Mkoa wa CDM wa Kinondoni kupitia blog yake?

Sijawahi kuona lakini na wewe nikuulize swali, ulishawahi kuona viongozi wa mkoa ama wilaya au wanachama wa kawaida wa ccm wanamlalamikia naibu katibu mkuu wao kwamba anashirikiana na wapinzani wao kuwahujumu? umeshawahi kusikia kiongozi wa ccm wa wilaya au mkoa anamlalamikia naibu katibu mkuu wake kwamba ameshirikiana na vyombo vya dola kumbambikia kesi ya uongo, tena kesi nzito ya ugaidi ili kummaliza?

Kwanini naibu katibu mkuu wa Chadema yeye anatuhumiwa na wanachama wenzake ambao anatakiwa kuwaongoza, kwamba anakisaliti chama kwa kushirikiana na wapinzani wa Chadema hata kufikia hatua ya kuwatengenezea kesi za uongo ili kuwamaliza? Na Henry Kilewo ametaja waziwazi jinsi naibu katibu mkuu wake alivyoshiriki katika kumtengenezea kesi ya ugaidi, iliyokuja kufutwa baadae na mahakama kuu.

iii) Ulishaona Katibu Mkuu wa CCM akashangilia post inayomchafua Naibu Katibu Mkuu wa chama chake kama alivyofanya Dk Slaa hapa JF alivyokuwa ana-like post zilizokuwa zinamnanga Naibu Katibu Mkuu wake?

Kwanza kabisa nikukumbushe kuwa katibu mkuu wa ccm hana verified user account hapa JF, sasa kama yupo na unamfahamu labda unisaidie kumtambua ili nijaribu kumfuatilia kuona huwa analike posts za namna gani hapa JF.

Lakini pili nikuulize, wewe ukiona mtu amelike post ya mtu huwa unapata tafsiri gani kichwani kwako? Kwa mfano mimi nimelike post yako ambayo ndiyo hii ninayoi challenge, wewe umepata tafsiri gani kwa mimi kuilike post yako??

iv) Umeshawahi kuona kijana anayemchafua Naibu Katibu Mkuu wa CCM mitandaoni na ambaye ana kesi pending akaajiriwa makao makuu ya CCM kwa kazi maalumu kama ambavyo Ben sanane ameajiriwa makao makuu na Katibu Mkuu wa CDM kwa kazi maalumu ya kumshughulikia Naibu Katibu Mkuu?

Bahati mbaya sana naibu katibu mkuu wa ccm hajakuwa na hizo skendo za kukihujumu chama chake. Hata mara moja sijawahi kusikia vijana wa ccm wakimlalamikia naibu katibu mkuu wao kwamba anaunda magenge ndani ya chama chao yenye lengo la kukidhoofisha ccm. Tumekuwa tukimshuhudia naibu katibu mkuu wa ccm akitajwa mara kwa mara na wanaChadema kuwa amekuwa mstari wa mbele katika kufanya vitendo vya hujuma dhidi ya chama chao.

Jambo la kushangaza ni kwamba naibu katibu mkuu wa Chadema yeye anatuhumiwa kuunda genge la uhalifu ndani ya chama chake kwa nia ya kutaka kukivuruga na kukisambaratisha. Vijana wale waliofukuzwa na Bavicha Juliana, Mtela, Mchange, Kisandu, Makatta na wengine ambao hawakufukuzwa kama Ben Saanane, Nyakarungu, Gwakisa na Mamuya walipata kukiri kwamba walikuwa wanamuunga mkono naibu katibu mkuu wao kuliko kiongozi mwingine yeyote ndani ya chama.

Hata taarifa za wao kutumika kukihujumu chama zilipotoka zikimu-implicate naibu katibu mkuu, na baada ya baadhi yao kufukuzwa uanachama, na naibu katibu mkuu akawakana kuwatambua walijitokeza kwenye vyombo vya habari kumshutumu kuwa hana msimamo na kimsingi kitendo cha kuwakana vijana wale ambao walikuwa wanajipambanua waziwazi kuwa ni vijana wake ilionyesha kiwango cha juu cha UNAFIKI.

Nadhani Ben Saanane anaonekana mwiba mkali kwa naibu katibu mkuu wake kwa kuwa ametajwa kuwa naye bega kwa bega katik harakati za kukihujumu chama kabla hajabadilisha msimamo na kujitoa katika kundi maarufu la PM7 na huo ndio ukawa mwanza wa kuchukiwa kwake na kupakaziwa kila aina ya kashfa ili kumuonyesha kuwa yeye ni mtu asiyefaa katika jamii. Hata polisi inapotokea mtu mmoja jambazi amekwenda kuwapa taarifa za ujambazi uliokuwa unafanywa na wenzake mtu huyo hashitakiwi bali anakuwa shahidi wa upande wa Jamhuri, kwahiyo sioni mantiki ya kumshambulia Ben katika hili.

Tumeambiwa waraka wa uchafuzi umechomolewa kutoka makao ya CDM ambaye mtunzanji wake mkuu ni Katibu Mkuu. Tumeambiwa utafiti wa kumfuatilia Naibu Katibu Mkuu umefanyika tangu 2008 na umefanywa na vijana wa chama waliopewa kazi maalumu. Hakuna mtu makao makuu aliyekanusha jambo hili kwa wiki mbili na bado ulitaka Zitto akae kimya? Ulitaka barua ya malalamiko aipeleke kwa nani wakati utaratibu unaeleza kwamba malalamiko yote yanaelekezwa kwa Katibu Mkuu, hata kama mwenyekiti ana malalamiko?

Kwanza mimi sijapinga wala kukataa naibu katibu mkuu kumuandikia barua ya malalamiko katibu mkuu wake. Nilichohoji ni utamaduni alioanza kuujenga wa kuutangazia umma kila mara anapomuandikia barua katibu mkuu wake. Kwani kulikuwa na ulazima gani wa kutoa press release akielezea jinsi alivyomuandikia barua katibu mkuu wake akimtaka akanushe au athibitishe tuhumma zile?

Utakumbuka tu kwamba siku moja kabla ya kutoa press release ile alifanya mkutano Kaliua Urambo na kuutangazia umma kwamba ndani ya Chadema hakuna mgogoro wowote, lakini kesho yake anaibuka na press release inayoshadidia hoja aliyokuwa ameikana jana yake. Sasa kama huo sio UNAFIKI ni nini?

Pili zipo taarifa rasmi kwamba chama kilishatoa taarifa rasmi za kuukana waraka ule na mawasiliano ya kimtandao (email) yaliyofanyika baina ya Mnyika na mshirika wa naibu katibu mkuu Andrea Cordes na Naibu katibu mkuu alikuwa copied kwenye majibu yale ya Mnyika. Sasa sijui ulitaka kifanyike kitu gani ili uridhike.

Sikiliza Maranya, nyie ndiyo mnaokiharibu chama na kuwapa kiburi viongozi wetu kwa kuendekeza unafiki. Unafiki wenyewe ni kwamba akifanya kosa "A" ni kosa, lakini kosa hilohilo akifanya "B" si kosa. UNAFIKI. Ukweli pekee ndiyo utakaotuponya. Wiki ijayo tuna Kamati Kuu na tunaendelea kuandaa nyaraka hapa. Dk amejaribu sana kukwepesha ajenda ya kujadili huu mgogoro, anataka tukajadili mambo ya kawaida tu kama vile hakuna tatizo katika chama. Wajumbe wamegangamala kwamba jambo hili lazima lishughulikiwe kikao kijacho cha KK.

Nyie endeleeni kuwalisha viongozi wetu ----- mkidhani mnakisaidia chama.

Mkuu sasa kumbe wewe ni mtu mkubwa sana unayehudhuria vikao vya kamati kuu sasa mbona tena unakuja kulialia hapa kama mtu asiyekuwa na nafasi ya kutoa hoja katika vikao vikubwa vya maamuzi kama KK.

Mimi kama mwanachama ninayetambua wajibu wangu ni kuwaambia ukweli viongozi wangu pale wanapokosea, hata hii thread niliianzisha nikifanya comparison kwa lengo moja tu zuri la kutaka kumsaidia naibu katibu mkuu wangu aone kuwa yeye ni sehemu ya uongozi wa juu wa Chadema kwahiyo asipende kujitenga na wenzake kwamba hataki kuonekana kuwa naye ni sehemu ya uongozi wa juu wa chama, sijui ni kwasababu zipi lakini kama anaona kwamba hawezi kuhimili vishindo vya kuwa katika top brass kwakuwa hapendi kushirikiana na wenzake kwanini asijivue hicho cheo cha naibu katibu mkuu ili kipate mtu mwingine atakayesaidiana na katibu mkuu katika kutekeleza majukumu yake.

Kwa hali ilivyo sasa hivi ni sawa na kutokuwepo kabisa kwa naibu katibu mkuu bara kwakuwa tangu alipoteuliwa kushika wadhifa huo sikumbuki amewahi kufanya kitu gani katika kutekeleza majukumu yake. Mara zote tumemuona katibu mkuu mwenyewe akihangaika, na mara kadhaa asipokuwepo tunamuona mzee Kimesera na Mnyika wakikaimu nafasi hiyo wakati naibu katibu mkuu yuko busy na mambo yake mwenyewe binafsi.

Kwa kumalizia kwa mtazamo wangu, naibu katibu mkuu wa Chadema ni lazima abadilishe mbinu zake za kufanya siasa vinginevyo nakuhakikishia anazidi kupoteza ushawishi kwa wanachama wenzake na atafika mahali atayakumbuka maneno haya tunayoyaandika kila mara tukimsihi abadilike na kukijenga chama chake badala ya kuwa chanzo cha migogoro ndani ya chama chake.
 
Last edited by a moderator:
Mwita Maranya,
Hongera sana kwa uchambuzi makini

Pamoja na ushamba wa kisiasa alio nao linapokuja suala la masilahi ya taifa ukichanganya na siasa zake za kifedhuli lakini huyo naibu katibu mkuu wa CCM hajawahi kufikia hatua hiyo

chanaga united unabonge la kiherehere yaani kama wale wamagoti
 
Last edited by a moderator:
Nakumbuka chambuzi kama hizi ndio zilinisukuma kujiunga na Jamiiforums miaka hiyoooo
Nimegundua watu wengi hawajakuelewa na haswa ulipotumia falsafa ya kumuweka katikati Mwigulu kujengea hoja yako

Binafsi pia sioni kama ni sahihi kwa katibu na naibu katibu wake amabao kimsingi wanatakiwa kuwa na ukaribu wa kipekee kiutendaji wakaishia kuandiakiana barua za kutaka ufafanuzi wa utendaji wao wa kazi............hili halipo sawa

Nachukulia kama kuna tataizo kubwa la kiuongozo ndani ya CDM, na haswa linapokuja swala la migogoro ya ndani ya chama, kutofautiana ni sehemu ya maisha kwenye siasa tatizo kubwa ni jinsi ya kuzikabili tofauti hizo kama chama na kuwa kitu kimoja...........kwa CDM hili linatatizo
 
Back
Top Bottom