Mwigulu Nchemba hafai kuwa Waziri wa Fedha, viatu vimeshampwaya

Freyzem

JF-Expert Member
Jun 29, 2013
10,052
24,442
Wapo watakaosema tunamuonea wivu, n.k!

Lakini huo ndio ukweli! Mwigulu Nchemba kupewa Wizara ya Fedha kwake ni kama kumvisha mtoto wa chekechea kiatu namba 45 cha mtu mzima.

Huyu Mwigulu aliwahi kuwa Naibu Waziri wa Fedha na pengine wengine wanaweza kumtetea kwa kigezo hicho kwamba tayari ana uzoefu na hiyo wizara na zaidi ni kwamba ni msomi mwenye taaluma ya juu ya masuala ya uchumi! Lakini kiuhalisia japo ana sifa hizo lakini kwa mwenendo wake alionaylo hakupaswa kupewa hii nafasi nyeti!

Hakuna cha maana sana atakachofanya kwenye hii wizara, zaidi anaweza kuwa miongoni mwa mawaziri wabovu zaidi katika hiyo wizara.

Alipokuwa Waziri wa Mambo ya Ndani yapo mambo ya hovyo sana alikuwa akiyayafanya hali iliyopelekea akatumbuliwa akiwa njiani na kunyang'anywa hata gari bila kutarajia.

Hali iliyopelekea kuanza kumlamba viatu mwendazake na kupewa Wizara ya Katiba na Sheria lakini nayo wizara hii ilimshinda ni vile tu haiangaliwi sana.

Sasa amepewa wizara nyeti ya fedha, kwa anayoyafanya hata huko bungeni yanaakisi kabisa ubovu wake katika kuiongoza.

Kinachotakiwa ni hatua za haraka zifanyike na ninaamini Mama yetu macho yake yanaona vyema kama alivyosema, pengine hakushauriwa vyema hivyo naamini tayari mezani mwake wapo washauri mahiri ambao tayari wamekwishaona na wamekwisha mshauri vyema la kufanya.

Hivyo naamini mapema tu matokeo yataonekana.
 
yule jamaa kuna baadhi ya Members wanamsifu ana akili , ila mimi ninachoona ana kipaji cha kukalili notices tu, Mwigulu sio tu hafai kuwa waziri bali hafai hata kuwa mbunge.

Elimu yake haiendani na matendo yake pamoja na mambo anayozungumza , to be honest nauona mstari mdogo sana unaowatofautisha Mwigulu na Baba Levo.

kama ukiniuliza mimi maoni yangu, hiyo wizara bora apewe hata Musukuma sio Mwigulu madelu
 
Alipokua Waziri wa Katiba na sheria alibariki uchafuzi uliopewa jina la uchaguzi 2020. Huyu mtu anafaa kuwa kiongozi wa familia yake tu.
Kuna siku nilimsikiliza anamkosoa Tundu Lissu ilibidi nitoe ile video, miongoni mwa hoja zake nzito kwanini Lissu alishindwa uchaguzi ule, anadai ni kwamba Lissu alikuwa na Ticket ya kurudi Belgium.

Hivo basi watanzania hawakumchagua Lissu kwa sababu baada ya uchaguzi alikuwa anaondoka kwenda ulaya, nikapima na hoja ya Lissu kuwa na hiyo Ticket alisema anarudi kwa ma daktari wake kwani Afya yake haikuwa imeimalika nikaona Madelu ni wa kupuuza
 
Kabisa yani, kuna watu wengine wapo kwenye mfumo ukiwaza walipataje nafasi hizo unakosa majibu!
Niliyoona Trump kawa Rais wa Taifa lenye nguvu Sana duniani, nimeacha kuwadharau tena wanasiasa..they are very good at what they do.. anything is possible Kwao..yaani kuna kipindi nataka kufanya kufuru na kutaka kuamini kwamba uchawi upo hapa Duniani but again najiuliza Trump aliroga wapi?!
 
  • Thanks
Reactions: PNC
Huyo Mwigulu Nchemba ni mhuni tu hafai hata ujumbe wa nyumba kumi kumi. Ni mtu hatari sana huyo.
Mh. Mwigulu, simama Bungeni toa muelekeo je umejipangaje kuongeza idadi ya walipa Kodi (kutanua wigo wa Kodi)

Je, utakuzaje uchumi ili uchumi wa Kati ufike kwenye mifuko ya Watanzania mnaowaita wanyonge'

Je, Mwigulu, suala la Mafao ya wafanyakazi... NSSF na PSSSF...

Watu walipwe mafao

Je utakuza uchumi kwa kufufua Kilimo Kwanza? Ufugaji biashara...!

Ita wafanyakazi sekta binafsi, TUCTA, Wafabiashara na Wawekezaji...wape assurance ili biashara zifufuke

Waambie TRA kuwa wao sio police, TRA wawe na customer care na watoe elimu Mara kwa Mara
 
๐Ÿ™Œ๐Ÿพ๐Ÿ™Œ๐Ÿพ๐Ÿ™Œ๐Ÿพ๐Ÿ™Œ๐Ÿพ๐Ÿ™Œ๐Ÿพ๐Ÿ™Œ๐Ÿพ๐Ÿ™Œ๐Ÿพ Huyu jamaa hana uwezo huo Mkuu. Yeye ni kusifu tu mapambio yao yasiyokuwa na kichwa wala miguu. Kazi kutoa data zilizojaa uongo wa kutisha. Juzi alidai kuanzia 2017 hadi 2020 ajira 12.77 zilikuwa created. Tuna matatizo makubwa Mkuu Nchi hii.
Mh. Mwigulu, simama Bungeni toa muelekeo je umejipangaje kuongeza idadi ya walipa Kodi (kutanua wigo wa Kodi)

Je, utakuzaje uchumi ili uchumi wa Kati ufike kwenye mifuko ya Watanzania mnaowaita wanyonge'...
 
๐Ÿ™Œ๐Ÿพ๐Ÿ™Œ๐Ÿพ๐Ÿ™Œ๐Ÿพ๐Ÿ™Œ๐Ÿพ๐Ÿ™Œ๐Ÿพ๐Ÿ™Œ๐Ÿพ๐Ÿ™Œ๐Ÿพ Huyu jamaa hana uwezo huo Mkuu. Yeye ni kusifu tu mapambio yao yasiyokuwa na kichwa wala miguu. Kazi kutoa data zilizojaa uongo wa kutisha. Juzi alidai kuanzia 2017 hadi 2020 ajira 12.77 zilikuwa created. Tuna matatizo makubwa Mkuu Nchi hii.
Anatakiwa kuprove Anaweza, akishindwa...atatumbuliwa.

Rais Samia Suluhu sio Meko, asome alama za nyakati
 
Back
Top Bottom