Kwa maana hiyo Nchemba anasema CCM inafanya kazi ili kuanzia 2015 Tanzania iwe chini ya mfumo wa chama kimoja?
Kwa sasa hivi tuna vyama viwili: CCM na CDM. (vingine viko in between). Ukiuwa CCM unabakiwa na CDM, na vivyo hivyo ukuuwa CDM unabakiwa na CCM.
Tanzania tunasonga mbele au tunarudi nyuma? Coca Cola hafanyi kazi kuuwa Pepsi, au Star TV hafanyi mizengwe ya kuuwa ITV, vingenevyo hakuna umuhimu wa kuwa na soko huria. Tukirudi kwenye siasa, nini maana ya kuwa na mfumo wa vyama vingi, na vinatakiwa vifanyaje kazi?
Nchemba na team yake wanaweza kudhani kuwa wanapambana na watu wachache -wamejiaminisha kuwa 'adui yao' ni mtu watu wawili watatu. Pengine wangekaa kitako na kujiuliza kwanini watu na akili zao timamu wanaungana na watu 'wachache'? Na ukiowaondoa hao watu wachache ni kweli umma huo utakaa kimya and CCM will live happily ever after?
Ever heard of Jamsin revolution ndugu Nchemba?