Ukweli ndo huu,naiona Chadema inaelekea mwisho hata kama hawatakubali,naiona Chadema kupungua nguvu kutoka chama kikuu cha Upinzani Mpaka kuwa msindikizaji kama wengine,Chadema kimekuwa Chama chenye Nguvu ya watu wachache ambao hao ukiwakosoa basi utaonekena Msaliti,tofauti na CCM inaweza kumkosoa Mwenyekiti Taifa lakini usionekane Msaliti
Nitaendelea
Ndugu zangu Wanachadema. sasa chama chetu kinapitia katika wakati mgumu sana kuliko wakati mwingine wowote!
Kuna mapandikizi ambao wamo ndani ya chama ambao wana tafuta kila njia kukiua chama.Hawa wakina Mwigamba na wengine naomba tuachane nao kabisa, kama yeye anania nzuri na chama na kama bado hawezi kikihujumu chama kama anavyodai mwenyewe, kwa nini anaendelea kubwabwaja maneno kila mahali?Swala la uongozi wa chama kuwa kuna kutokuelewana kati ya Zito na viongozi wengine ndani ya chama hilo sio lake, kuna kamati na idara zinazohusika ndani ya chama kusaidia hilo!! Sasa kila kila Mwenyekiti wa chama mkoa akaamka na kuanza kujiona anatetea katiba na kuongelea mahusiano ya viongozi wa chama kweli itawezekana???
Chadema tuchunge sana tunapoelekea uchaguzi wa mitaa 2014 na ule mkuu 2015.Wapo watu wameshaanza kushirikiana na ccm kuhamasisha vurugu ndani ya CHADEMA kwa kisingizio eti uchaguzi uitishwe!!Kuna hatari hapa!!
Kuna mapamdikizi wamo ndani ya chama wanajidai ni wakereketwa wanaotaka kutumia mwanya huo, kuwaondoa viongozi wa juu kimapinduzi na hata kuwaweka viongozi wengine ambao huenda ni mamluki na hatimaye wakakifutilia mbali chama na hapo ndio ukawa mwisho wa CHADEMA na aliyosema Wasira kuwa CHADEMA kitasambaratika kabla ya 2013 yakatimia.
Wazo langu, tuendelee kupambana kukiimarisha chama ili mwaka kesho kichote viti vingi serekali za mitaa ili kukiimarisha kuchukua dola 2015 na sio vinginevyo.Wasaliti wanaoendelea kutimuliwa ndani ya chama tuendelee kuwapuuza wao na maneno yao.Tuwapuuze kama tulivyowapuuza wale madiwani waliofukuzwa na hatimaye walipokuja kugombea kwa mlango wa vyama vingine tukawaaibisha kwa kutowachagua.
CHADEMA tuwe macho sana wakati huu, kila kona wabaya wetu wamejipanga; Mwigamba ni nani? yeye ameondolewa aondoke tu na nawahakikishia kuwa ataaibika kama wale madiwani.Ukweli ni kwamba! Hata Dr.Slaa akikisaliti chama Au Mbowe bado kitabaki imara.Watanzania hatuburuzwi tena na watu wanao kimbiakimbia kuita waandishi wa habari kuchafua wenzao tunachokihitaji ni mabadiliko ya kweli na sio vinginevyo.
Watanzania wanahitaji maisha bora,hali bora,uwazi,uwajibikaji na sio propoganda za watu.Huyo aliyeondoka aondoke ili chama kisonge mbele.Aende chama kingine. Na akigundulika mwingine naye atimuliwe bila kujali yeye ni nani.
Yangu ndiyo hayo naomba CHADEMA tushikamane na tusiburuzwe.