Mwigulu Nchemba: CHADEMA itakufa 2015

Last edited by a moderator:
Unapoteza muda tu na siasa zenu uchwara hapa jf,cdm tupo field juzi tulikuwa magu na nyanguge tukitoa elimu ya uraia tukiwa na makamanda PAMBA na GWAKISA wakati nyie mmejificha nyuma ya key board

Acha Porojo, elezea kwa nini SABODO kasitisha udhamini!
 
Ila na wewe kaka bwana. ukionahuna cha kuandika afadhali uwe unasoma thread za wenzako tu. Usiwe kama akina Fox (Machangu Do)
Chadema ni matapeli wa kisasa.

Nawasifu kwa kutumia matatizo ya wananchi kama mtaji, na wanavuna mihela kweli!
 
Chadema ni matapeli wa kisasa.

Nawasifu kwa kutumia matatizo ya wananchi kama mtaji, na wanavuna mihela kweli!

ivi chilosis, wakiweka picha yako apo kwenye id yako, wakaweka na ya member yoyote apa jf, nani anaonekana ni msukule kamili?ivi umekosa picha mpaka ukaweka picha mbaya ivo as if umebanwa na screw, huwezi ukawa unatania braza. Ivi na wewe ni msukule?maana ulishajiunga chadema ukatimuliwa na usukule wako. Dr slaa alikutimua chadema huwezi kumsahau milele....
 

ivi kuna mtu alishawahi kusema dr Slaa ni mtakatifu hapa jf au hata uku duniani?braza au ndo ivo unataka kutupa yaliyo moyoni kwako kuwa unamuona ni mtakatifu?be sincere, express your mind wala hatutakushangaa...ivi wewe afande Lukosi ndo unaweza kuomba cdm ifanye uchaguzi ili iimarike ili iwatese wapinzani wake ccm?au unaona uongozi uliopo sasa ni mwiba kwa ccm(sio kwako kwa kuwa wewe sio ccm, ccm wapo wametulia ila nyie chadema- waasi ndo mnaangaika i.e mwampamba, juliana, lukosi,etc_)...pole
 

viongozi wote wa chadema ni vijama na ndio tunanaowataka ni kiongozi mmjatu tu ndio mtu mzima na nafasi aliyonayo anastahili kwa sababu inaitaji busara ya hali ya juu, kwa hiyo usitegemee yatatatokea hayo hunayoyataka
 
kama kweli nyie wana ccm mnaujua ukweli tuambieni pesa za uchaguzi huwa zinatoka wapi?za kugharamia kampeni kama si wahindi wakina patel wale wanaohusika na epa na kuuza madawa ya kulevya nchini?semeni ukweli vijana wa bavicha
sabodo...?
 
Misukule ya CCM inataka kuuawana katika hizo picha hapo juu huku wenzao kicheko kwa kwenda mbele.


dah eeeh bana umetisha sana na nadhani umezungumza sana, kwani picha zina maneno mengi sana hizo hata kama hukuweka andishi hata moja


haya sasa zamu yako mleta uzi hebu weka ushahidi wako katiuka jamvi hili ili mjadala uwe mkali
 

Our BELOVED PRESIDENT NYERERE alisha wahi kusema KUNGUNI NI ADUI MKUBWA wa SERIKALI YETU... Sasa nyie ndio VIKUNGUNI Mnavyofaidika kwa kunyonya DAMU za WALALA HOI mkiwa NJE ya NCHI...

Bro unatumia nguvu zako just for nothing, kujibu sred za namna hii!

Heshima pekee unayoweza kumpatia mtu mwenye dhamira kama hii ni kuiacha sred yake... ie Kumpuuza tu!
 
Huyu jamaa nngu007siamini kama ndiye huwa analeta post kwa niaba ya Serikali hapa jamvini na hasa post za taarifa za Wizara ya Mambo ya Ndani na hasa za Idara ya Uhamaji. Ni mtumishi wa Serikali lakini ni mamluki amejisahau. Vyombo vya Usalama vimmulike huyu hawa ndiyo wale wakati mwingine huwa wanatoa siri za Serikali nje.

 

Kwani unapotoa mchango kanisani, padri/mchungaji anakua hana hela ya kula?

Unapolipa kodi wakati huna hela ya ada ya mwanao, unakua chizi?

Kutoa ni moyo sio utajiri...!!
 

Hicho kifo cha magwanda tumekisikia toka mwaka 2000 na mwimbo umekuwa huohuo miaka 13 imepita sasa
 
MOSI:
KUHUSU MIGAWANYIKO NDANI YA CHADEMA
Sijajua hata sasa ulizingatia nini uliposema kuwa CHADEMA imegawanyika katika team tatu, ila pamoja na hayo kama umezingatia hizi VURUGU za kwenye mitandao ambazo asilimia kubwa ya vurugu hizi zinaratibiwa na CCM na vijana wachache wa CHADEMA wanaotumika bila kujielewa pamoja na usomi wao, UTAKUWA umejidanganya, tena sana.

Hakuna kipindi ambacho CHADEMA inabidi iwe imara na yenye mashirikiano kama kipindi hichi ambacho CCM imechoka, na kwa bahati nzuri VIONGOZI wakuu wa CHADEMA wanalijua hili na wanazijua hila zenu CHAFU za kutaka kuonesha kuwa ndani ya CHADEMA kuna migawanyiko. CCM mnaibua mijadala humu JF kwa kuonesha kuwa Zitto hapatani na viongozi wenziwe, alafu mnajifanya mnaunga mkono upande wa Zitto ili wale waliongia kwenye mtego huu waone kuwa Zitto ni msaliti kisa tu mnamuunga mkono nyie CCM, hizi ni mbinu za kikoloni na katu viongozi wetu hawatayumba na wameishinda hii mbinu. Maneno ya Zitto aliyoyasema Tabora ni kiashiria tosha kuwa MAGAMBA mshashutukiwa na 2015 hamna chenu.

[video=youtube_share;zh5tiBoZKjw]http://youtu.be/zh5tiBoZKjw[/video]

PILI:
Pili kuhusu mahesabu ya CHADEMA pia acha kujidanganya na kupotosha, chama kimeshatoa vielelezo vya kukaguliwa kwake hivyo hakuna haja ya kupika au kuchakuchua, kinachosubiriwa ni hivyo vielelezo kupelekwa PAC na si vinginevyo. Shaka yangu iko kwa CCM kwani yenyewe ndio yenye dola hivyo ni rahisi kwao kuchakuchua.

TATU:
Hivi CCM suala la uchaguzi wa CHADEMA linawahusu vipi? mbona sisi wenyewe hatuhoji hilo? Je, kutokuhoji kwetu mwatufanya tu wajinga? Elewa kwamba sasa chama kinaimarisha misingi na matawi ambayo ilifunguliwa kwa kupitia M4C na mimi binafsi sioni kama kuna umuhimu wa kufanya uchaguzi ndani ya CHADEMA sasa, bali naona bora viongozi wa sasa waendelee hadi mara baada ya uchaguzi mkuu, pamoja na hayo, hata kama ukifanyika uchaguzi basi nafasi nne za chama zisifanyiwe uchaguzi,,,ambazo ni mwenyekiti na makamu zake wawili na katibu na manaibu wake.

MWISHO:
Endeleeni kutumia mitandao kwa nia ya kuichafua CHADEMA na endeleeni kutumia mizombi ya vijana wa CHADEMA yenu mnayoitumia bila kujijua kwa lengo la kuibomoa CHADEMA,,Lakini jueni hamtafanikiwa,,,,CHADEMA haipo kwenye MITANDAO chadema ipo kwenye mioyo ya wananchi.

Njano5.

0784845394
 
Leo natamani niwasaidie kidogo watani zangu wa chadema.
.............. acheni mbwembwe zooote, fuatilieni daftari la wapiga kura.
 
Chadema ni matapeli wa kisasa.

Nawasifu kwa kutumia matatizo ya wananchi kama mtaji, na wanavuna mihela kweli!

mmmh hupo sahihi ungesema CCM inatumia umbumbu na umaskini wa watanzania kuendelea kuwa madarakani ningekuelewa
 
tatizo kubwa nikuchanganya mambo... mapenzi, uchumi, siasa, na mengineyo kazi kuchanganya bwana maswala ya hela wasiweke siasa kila kitu kijiendeshe chenyewe though vinategemeana jamani.

WA KUIKOMBOA HII INCHI NI WANANCHI NA SIYO VYAMA VYA SIASA KAMA WENGI WETU WANAVYODHANI SI SAWA... tuweke siasa pembeni tutafute ukweli ni hupi, kwa akil za watanzania wengi tuanahisi kunachama ambacho kitashika madaraka kisile apo cha juu kuumizwa kupo pale pale kama tusipofungua macho kwa kweli.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…