Watanzania tuna tatizo la kufikirisha bongo zetu, eti watu wanafikiri kuvaa bendera ya taifa au nguo yenye rangi za bendera ya taifa ndio kuwa mzalendo! Watu walipewa jukumu na posho kutafuta vazi maalum litakalo kuwa vazi la taifa sijui huu ni mwaka wa ngapi, vazi la taifa limeshindikana! Sasa unamsikia mtu na akili zake tena mheshimiwa kabisa anasema tuvae nguo zenye rangi ya taifa ndio liwe vazi la taifa! Hii inaonesha namna gani watz hatuwezi kukaa na kuja na kitu chenye akili. Sijawahi kuona nchi ambayo vazi lake la taifa limepambwa rangi za taifa! Ndio maana siku hizi utawaona hasa wabunge wanawake wa CCM wanavaa mitandio ya bendera ya taifa. Bado tunahitaji vazi la taifa. Bendera yetu ya taifa tunaiheshimu sana lkn haiwezi kuwa ndio vazi la taifa! Namuunga mkono spika Anna Makinda alivyokataa leo bungeni kwamba hakubaliani na mtindo wa uvaaji wa skafu zenye ya taifa shingoni wa Mhe Nchemba Mwigulu kuwa kama vazi la taifa!!!