Mwigulu: Naombwa nigombee urais 2015

Mwigulu: Naombwa nigombee urais 2015

Jamani hata mwigulu!!!!
Haya yote kasababisha Mr Kikwete, yaan jishi nchi ilivyoongozwa kicheki-bob. Imesababisha kila mtu anajiona anaweza kuwa Rais.
 
Hii ndiyo level ya Watanzania eti Mwigulu naye sasa awa gumzo.Iramba sawa awe kiongozi lakini Tanzania yenye mahusiano na Dunia yote ni kosa kubwa kwa Mtanzania kufikiria kuwa na Rais aina ya Mwigulu.Tuwe na fikra pana nje ya siasa zetu za Ki ccm.Huyo ni kijana ndani ya kundi la Wazee wa CCM hivyo wanamuona kama ndiyo ngao yao dhidi ya vitisho toka kwa Wapinzanzani wao.
 
Kizuri chajiuza, KİBAYA CHAJİTEMBEZA!

Hivi hayo makundi yote yaliyomwomba ajitokeze kugombea yalimtokea ndotoni wakati yuko usingizini?

Kwa kuwa kama kweli makundi yote hayo yangekuwa yamemwomba kugombea, basi nasi wananchi angalau tungepata habari kupitia vyombo vya habari.

Umesahau hata Mbowe aliandaa wazee wa Kigoma wampigie debe eti wamemuomba agombee tena?.
 
mwezi desemba nilisafiri Dodoma-Manyoni, kwenye mawe makubwa karibu yote kando kando ya barabara yameandikwa "Mwigulu 2015"

labda mpaka mawe yamemuomba agombee
 
Ni chama kubwa haitegemei majina ya wanachama wawili watatu kama upinzani ulivyo. Kila mwanachama yupo huru kufanya siasa awezavyo ili asivunje katiba ya chama.

Haya bwana ila kuna dola kubwa zilizokuwa na umakini sana duniani zilizoea mpaka kila kitu kikawa kawaida zikastukia maji yamezidi unga. Huenda hii ni dunia nyingine
 
mwezi desemba nilisafiri Dodoma-Manyoni, kwenye mawe makubwa karibu yote kando kando ya barabara yameandikwa "Mwigulu 2015"

labda mpaka mawe yamemuomba agombee

Hiyo kali sana mkuu wangu.
 
Haya bwana ila kuna dola kubwa zilizokuwa na umakini sana duniani zilizoea mpaka kila kitu kikawa kawaida zikastukia maji yamezidi unga. Huenda hii ni dunia nyingine

Hiyo kawaida mkuu wangu.
 
Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba, amesema makundi mbalimbali ya kijamii yamemuomba agombee urais wa Tanzania katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba Mwaka huu. Nchemba ambaye pia ni Naibu katibu mkuu wa CCM Bara, aliyataja makundi hayo kuwa ni pamoja na viongozi wa dini ya Kiislamu na Kikiristo, wanafunzi wa vyuo vikuu, watanzania wanaoishi nje ya nchi, wakulima na hadi watu wa vijiweni. "Hata nilipoenda mwanza hivi karibuni nilikuta bango kubwa limeandikwa 'Mwigulu ni wewe unayekuja, au tumsubiri mwingine?' alisema Mwigulu
Je, anafaa kuwa Rais??


 
Jinsi anavyoshughulika na sakata la Escrow kwa kutafuta sifa za kijinga hana sifa hata za kuwa Mbunge.... anadai kodi kwenye michango ya zawadi badala ya kwenda kutafuta kodi ya mabilion iliyofichwa kule stanbic.

Mpuuzi mkubwa.
 
Hivi gaidi akiwa ikulu si kuna siku atajilipua tu
 
Afae kwa sababu tu ya kujionyesha amebadilika tabia baada ya kwenda kwa TB Joshua, au baada ya kupata unaibu waziri? Huyu kijana alifanya vitendo vingi sana vya kiharamia miezi michache iliyopita, kuanzia kule Igunga, Arumeru na hata sakata la Lwakatare. Tulimsikia sana bungeni kwa kiasi kikubwa alivivyokuwa amekusa utulivu, busara na ushawishi wa hoja. Ghafla, leo anaonekana ni kijana mwenye ueledi, mnyenyekevu, mpenda watu na mpenda Tanzania!!!!!!! HAPANA HAPANA. Tunahitaji kumuweka kwenye mizani miaka michache atushawishi kuwa Mwigulu tuliyemfahamu siye huyu tuliyenaye sasa.
 
Mimi hata sijajitangaza wakati familia ya Karume na Nyerere wameniomba kugombea urais pindi muda ukifika.
 
Kikwete ameshusha hadhi ya urais, mpaka mwehu mwigulu mchemba naye anautaka urais.Labda akawe rais wa wanyiramba...nyambafff kabisa
 
Kuna mahali huyo bwana kaonyesha amepambana na mafisadi kwny wizara yake? Mi nadhani sio sahihi!!! These guyz are scrumbling for creating New Deals!! Najua wananchi hawatasikia kelele za mavuvuzela kuingia ikulu isipokua watu makini tu!!!
 
kudeclare presidential candidate kwa ccm members ni wimbo mpya uliokosa beat!et mwigulu naye kaombwa by whom?apewe urais mtu anayeamin democracy kwa maana upinzan ni uasi na si uzalendo!!mwigulu hawez kuongoza nchi yenye mfumo wa vyama vingi atawalipulia mabom wapinzan koz hamin ktk siasa za ushndan!!alafu anapenda sifa laini(jk).haiwezakani hata siku moja mazur ya mtu yakahalalisha maovu!!i dont trust him.
 
Sasa kama tayari anazo pesa anataka Urais hili iwe nini wajameniiiii ??????
 
MH Mwigulu Nchemba amenukuliwa katika gazeti moja leo akidai makundi mbalimbali yamemuomba agombee Urais mwaka 2015.

Ameyataja makundi hayo kwamba ni makundi ya dini wakiwemo waislamu na wakristo, vijana wa vyuo vikuu na makundi mengine.

Amesema alipotembelea Mwanza hivi karibuni akikutana na mabango makubwa yakisema hivi kweli wewe ndio Mwigulu unakuja kutembelea kuonyesha kwamba jambo hilo ni bahati kubwa kwa wanaMWANZA!!?.

Maoni yangu: Mwigulu pamoja na kuheshimu mchango wako mkubwa katika kukijenga chama na kupambana na mafisadi ndani ya nchi na hasa wizara ya fedha lakini nakuomba uwe mvumilivu bado hujawa na uwezo wa kukabiliana na changamoto za nchi hii. Ni wakati mzee wa maamuzi magumu kuongoza au kijana bright January wa Makamba au MwanaCCM mwingine aliyekomaa katika siasa za nchi hii.



who is brighter between mwigulu & january makamba? ur are realy stupid
by the way rais,ni slaa ,hyyo mamvee awe rais wa richmond labda
 
Back
Top Bottom