Mwigulu: Naombwa nigombee urais 2015

Hivi CCM ni chuo cha kufundisha urais???

Kuombwa sawa, lakini hakutoshi! Je yeye mwenyewe dhamira yake inasemaje?!
Mimi kwanza kuamini kwamba huyu dogo ameanza kupata mental stability lakini siamini kwamba ameshajenga uwezo WA kuhimili changamoto za Magogoni!!siamini, he is still a rookie in that sense!! Asubiri
 
Mwigulu acha ujinga! Kama hao uliowataja walikuomba ukawaongoze, omba usheikh au uchungaji. Sijui kijana huyu ana maradhi gani. Mara aibuke na hoja safi za kuendeleza nchi, mara jasusi, mara aropoke, vipi?
 
Mimi hata sihangaiki kutafuta gazeti la mengi gazeti lenyewe la kiminga hata hoja yenyewe ya kijinga kwanii kujisumbua.

Tokea lini ukapata akili ya kusoma magezeti yenye maana. Ningeshangaa sana kukuona ukisoma Nipashe. mwananchi, citizen, raia mwema n.k. nafikiri ningevolunteer kuomba madaktari wakutoe mirembe maana ugonjwa wako ungekuwa umepona.
 
Jamani hebu tukijikumbushe: Yule Babu wa kikombe wa Loliondo mbona kimya? Dawa iliisha, iliexpire? au? Baadhi ya viongozi wa serikali ya Tanzania walistahili kushtakiwa kwa kudanganya wananchi na kuwasababishia vifo. Tofauti ya Mwigulu na babu wa Loliondo ni ndogo saaana, labda umri tu!
 
Ikulu imekuwa sehemu ya kupiga dili bana

Kama kikwete kaweza nani anashindwa bana

Acha waende ,acha wagombee bana

Natamani sana Nyerere angekuwa hai...I swear angeshaondoka CCM
 
Duuuh hiyo nchi rais awe mwigulu si vilema wataongezeka? Aende China apewe PhD ya kunyofoa kucha na kumwagia tindikali na kuteka na kutesa wananchi
 
Mwigulu acha ujinga! Kama hao uliowataja walikuomba ukawaongoze, omba usheikh au uchungaji. Sijui kijana huyu ana maradhi gani. Mara aibuke na hoja safi za kuendeleza nchi, mara jasusi, mara aropoke, vipi?

Unaweza kutukumbusha amewahi kilifanyia nini taifa hili likapata kustawi.

Mwigulu amewapumbaza wanyiramba kwa virushwa vya vihela kiasi kwamba wanyiramba wanapenda kuhongwa kuliko kabila lolote tanzania (wanawake kwa wanaume)

Tumeambiwa rushwa hupofusha akili ndio maana tunamuona anavyotumbukia kwenye mashimo, eti awe rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania!!!!

Hao masheikh na maaskofu waliomuomba agombee urais watakuwa wameshapewa zaka na sadaka kupitia account zao binafsi
 
Siku zote kwenye msafara wa mamba na kenge wamo. Mwigulu aendelee kuwa msindikizaji kwenye safari ya urais
 
Back
Top Bottom