Mwigulu: Naombwa nigombee urais 2015

Mwigulu: Naombwa nigombee urais 2015

Paw naomba uunganishe uzi wangu huu na mwingine nilioanzisha unaoendana na huu.
 
Last edited by a moderator:
CCM tafute mgombea, UKAWA tunamtafute Rais.
 
MH Mwigulu Nchemba amenukuliwa katika gazeti moja leo akidai makundi mbalimbali yamemuomba agombee Urais mwaka 2015.

Ameyataja makundi hayo kwamba ni makundi ya dini wakiwemo waislamu na wakristo, vijana wa vyuo vikuu na makundi mengine.

Amesema alipotembelea Mwanza hivi karibuni akikutana na mabango makubwa yakisema hivi kweli wewe ndio Mwigulu unakuja kutembelea kuonyesha kwamba jambo hilo ni bahati kubwa kwa wanaMWANZA!!?.

Maoni yangu: Mwigulu pamoja na kuheshimu mchango wako mkubwa katika kukijenga chama na kupambana na mafisadi ndani ya nchi na hasa wizara ya fedha lakini nakuomba uwe mvumilivu bado hujawa na uwezo wa kukabiliana na changamoto za nchi hii. Ni wakati mzee wa maamuzi magumu au kijana bright January wa Makamba au MwanaCCM mwingine aliyekomaa katika siasa za nchi hii.

hamna lolote.
 

Attachments

  • BORA UKIMWI KULIKO CCM.jpg
    BORA UKIMWI KULIKO CCM.jpg
    25.1 KB · Views: 142
Hajasema kwamba anayejiita nabii TB Joshua na waganga wa kienyezi wamemwomba agombeee
 
Huyu anayesema fedha za wizi za escrow zilipiwe kodi.mafiiiiii, siku zijazo hata pesa za madawa ya kulevya zitalipiwa kodi kama rais atakuwa Nchemba
 
Pole pole naanza kuziona dalili za Tanzania kumegeke vipande vipande, Mwigulu akiwa rais, hivi wana Arusha watakubali kuitwa Watanzania? Na mabomu yale ya Soweto kweli!? Hapana, hili jambo Mungu na alipishilie mbali kabisa!
 
Uongozi wa juu wa CCM si uliweka zuio hakuna mtu yeyote kujitangazia nia ya kugombea mpaka hapo watakapo ruhusiwa?
 
Nakumbuka waliwekewa zuio na Mzee Mangula hakuna mwanaccm yeyote kutangaza nia ya kugombea urais mpaka,
atakapo waruhusu?
 
kama kaweza mkwer e kila mtu anaweza.
 
Nani asiepende kuwa kiongozi tena wa ngazi ya juu popote duniani? Ni haki ya kila mwanasiasa kutamani kufikia kiwango cha juu katika ngazi za uongozi.

Sawa lakini wengine wanapotamani wasiitwe waraho wa madaraka. Mkuki kwa nguruwe mtamu.........
 
Mbona unatishia watu wazima mkuu? Watanzania wana akili wala hawapo tayari kuona amani ya nchi yao inapotea kwasababu ya watu wenye njaa ya madaraka.

Kweli watanzania hatutaki amani yetu ipotee, lakini je ccm wanaitaka hiyo amani? Upuuzi wa kuapisha watu ambao hawakuchaguliwa unaweza kuvumiliwa? Kama ni amani lazima wote watekeleze wajibu wao kwa mujibu wa sheria na taratibu bila kubagua. Kinyume chake hapatakalika na hu ndio ukweli popote katika historia, tupende tusipende.
 
Makundi gan hayo yamtake awe rais? Mbona kila mtu ccm anajipgia debe? Hakuna cha Mwigulu wala Makamba anayefaa kuwa rais wa nchii hii!
Kizuri chajiuza, KİBAYA CHAJİTEMBEZA!

Hivi hayo makundi yote yaliyomwomba ajitokeze kugombea yalimtokea ndotoni wakati yuko usingizini?

Kwa kuwa kama kweli makundi yote hayo yangekuwa yamemwomba kugombea, basi nasi wananchi angalau tungepata habari kupitia vyombo vya habari.
 
Jamaa anajipigia debe..
Kura yangu na familia yangu haziendi CCM
 
Back
Top Bottom