Lowassa Ngoyai Edward
Kashfa ya Richmond bado inamfukuza na haitaki
kumuacha. Mbaya zidi mzee wa kupitiliza na
uzee ukizidi sana sio hekima bali ni nakama, na
lolote linaweza kutokea kwa mzee na nchi ikawa
shakani.
Bernard Kamillius MEMBE Fans Page
Fedha ile kashfa ya fedha za OIC haitamuacha
salama, na binafsi namtilia shaka huyu jamaa, na
sioni kama anatosha.
Samwel Sitta
Uzee ni shidaa lakini pia alilivuruga bunge la
katiba kutokana na tamaa yake urais. Mtu kama
huyu hafai kukukabidhiwa nchi hii.
Wilbroad Slaa.
Dikteta, ameshiriki katika kukinyofoa kipengere
cha ukomo wa uongozi katika katiba ya
CHADEMA, lengo Mbowe awe mwenyekiti na yeye
aendelee kuwa katibu mkuu, na ni muumini wa
majungu katika taasisi. Hafai kukabidhiwa nchi
sababu atafukuza kazi mawaziri kwa maneno ya
makorido na ataweza kubadilisha katiba ili
kujiongezea miaka zaidi ya kukaa ikulu. Pia mzee
kama lowassa.
The Legend of Mizengo Pinda
Pinda ni kigeugeu, na haaminiki hata kidogo, kauli
zake juu ya escrow na maamuzi ya pupa na
mawaziri kuwa mizigo ni sababu tosha ya
kumfanya asifae pia Pinda ni mwizi kwenye kashfa ya escrow na sukari na mbaya zaidi huyu mzee hajitambui maana kila kitu yeye huwa anazani na kufikiri tu yaani hana maamuzi
Magufuli
Kwa uwezo wake anafaa zaidi kuwa waziri mkuu
kuliko kuwa rais, ila naye ni mkurupukaji wakati
mwingine....
Mwiguli Lameck Nchemba
Ninamkubali Mwigulu kuliko wagombea wote
urais 2015 ccm kwa sababu walau ametuonyesha
uthubutu wake na utendaji wake
uliotukuka,amekua mstari wa mbele ktk kubuni
namna ya kuongeza pato la nchi na kujitegemea
na ss tumejionea ongezeko kubwa la ukusanyaji
wa mapato kutoka bil 300 hadi 800 kwa
mwezi,leo hii misamaha ya kodi isiyo ya lazima
ni mwiko chini ya utawala wake,Mwigulu
nchemba amekua akikemea maovu na ubadhirifu
wa fedha za serikali wazi wazi bila kificho wala
uoga hii yote ni ktk kuonyesha uthubutu na
mapenzi yake kwa watanzania
maskini...tunashukuru kwa kuungwa mkono na cc
ya chama ccm kuungana naye ktk kupambana na
ubadhirifu na wote tumeshuhudia tamko lilotolewa
na ccm kuwa hatua stahiki zichukuliwe,mh
Mwigulu huwa habahitishi ktk maaumizi yake
anatenda kwa uhakika bila unafiki, uoga wala
chuki,ila zaidi kwa uwazi na kuwashirikisha
wananchi wa Tanzania kila leo kupitia media
kwani ni haki yao msingi kusikia ama kwa hakika
watanzania wenzangu huyu ndiye mtu sahihi
kwetu 2015...
Lipumba.
Huyu ni dikteta, kabla sijabalehe na sasa
nakwenda katika uzee huyu mshikaji bado ni
mwenyekiti wa CUF, akipewa nchi ataweza
kufanya ubakaji wa katiba kama alivyofanya Slaa
na Mbowe kwa katiba ya CHADMA.
Mbaya zaidi ansemwa kuwa na tabia za udini, na
kiukweli mgombea mwenye kusemwa hivyo ni
shida,
Pia naye mzee kama lowassa.
Kigwangala
Kigwangala ni mtu wa siasa za kisasi, mtu kama
huyu hafai kuwa rais wa nchi, wapinzani wake
watafute nchi huyu akiwa rais.
Freeman Aikaeli Mbowe
Huyu mtu ana upungufu wa uadilifu, rejeeni ile
video yake ya kubusiana mate mkewe hadharani
na mbele ya kamera, mbya zaidi ndio mshiriki
mkuu wa kuichakachua katiba ya chadema kwa
nia ovu, kwa nia ya kujipatia nafasi ya kuongoza
tena chadema. Akipewa nafasi ikulu yetu itakuwa
ni danguro kutokana na vitendo anavyowafanyia wabunge wake wa vitu maalum (Joyce Mukya) ataweza kuwa dikteta pia wizi wa pesa za Ruzuku za chadema na ukabila unaweza ua Nchi kabisa