Mwigulu: Mama Samia kajifunza kuendesha nchi kutoka kwa Kikwete

Gwiji la maendeleo gani kaangusha mapato ya bidhaa za kilimo kama kichaa kwa kuingilia biashara ya korosho?

Kafuga majambazi kina Sabaya na Bashite.

Kajenga uwanja wa ndege kwao ambao haufanyi kazi mpaka watu wanatakankuutumia kuanikaia nafaka sasa.

Wacha mzaha wewe.

Magufuli alikuwa kawashikia akili wajingawajinga kama wewe tu, watu walioweza kuchuja mambo walimuona mshamba tu.
Chini ya utawala wake wa ovyo ovyo, nilikuwa naona aibu mgeni akijua kuwa mm ni mtanzania, rais wa ovyo kuwahi kutokea dunian.
 
Huwa najiulizaga huyo magu alifanya nn Cha Cha ajabu mpaka mumuabudu hivi...... maana kwa raia maisha yalikuwa magumu,wafanyakaz hali zilikuwa hoi,kutekwa kuliongezeka,deni la taifa kuliongezeka,watu hawakuwa huru kuongea chochote wanachojisikia....
Hawa ng'ombe ndio waliomuharibu kwa kumsifia ovyo kwenye mambo ya ovyo mpk akajiona na yy ni Mungu wa pili.
 
Kwa kauli hizi, Mwigulu Nchemba umewadhulumu heshima zao Rais mstaafu JK na Rais Mama Samia. JK hakuwa laissez faire kama unavyotaka kum-portray. Mifano ipo mingi, lakini mfano wa haraka ni ile issue ya aliyekuwa DC Albert Mnali alipowachapa waalimu viboko, Rais JK alichukua hatua mara moja akatengua uteuzi wake. Ati huyu ndiye unayesema "kadi nyekundu aliiacha nyumbani!".
Lakini huyo uliyemtaja kuwa alikuwa na "kadi nyekundu" muda wote ndiye aliyenyamazia mkuu wa wilaya aliyecharaza watu viboko huko Arusha, mkuu wa mkoa aliyehimiza polisi waue vibaka hata akashuhudia jinsi yeye mwenyewe alivyoua kibaka na kufurahi sana huko Mbeya, mkuu wa mkoa aliyevamia radio station akiwa na bunduki huko Dar, mkuu wa wilaya aliyekuwa anazunguka na genge la watekaji huko Hai, na wengine wengi. Wote hawa hakuna aliyeoneshwa kadi yoyote wala hata kukemewa tu! Actually yule DC aliyevamia shamba la raia na kuliharibu na yule DC aliyerekodiwa akishawishi kutoa rushwa walipandishwa vyeo kuwa RCs, ndiyo kadi nyekundu hizo?
Kwa jinsi ulivyomponda JK, unaposema Mama Samia kajifunza kwa JK unamaanisha nini, kajifunza hicho unachobeza?
Umewasilisha bajeti nzuri sana, nimeona mambo mengi innovative ndani yake, lakini hiyo conclusion uliyotoa ni sawa na kukojolea mchuzi! Yaani umepika vizuri sana, ukapakua, halafu ukakojolea.
 
Back
Top Bottom