mbingunikwetu
JF-Expert Member
- Feb 17, 2015
- 13,909
- 18,551
Hapo mkuu umemaliza! Mkanda ulianzia clouds hiyo tarehe 17/03/2017 kwa uvamizi wa Bashite ukihusisha askari wenye silaha waliowatisha wafanyakazi wa clouds TV, Ukahitimishwa kwa Nape kutishiwa bastola hadharani na watu wa kitengo!kwanza hata kabla hatujaenda mbali lile swala la clouds yeye kama ni waziri analiona lipo sahihi..? kama lipo sahihi iweje hili la nape lisiwe sahihi hlf lile liwe sahihi..? ama ndo kuuma na kupuliza kwa kuogopa meno ya bwana mkubwa!
Kama Mwigulu umeamua kushughulikia anzia mwanzo wa drama kule clouds hadi huyu aliyetoa bastola! Askari wote waliohusika mnawafahamu vizuri maana walitumwa na wakubwa wao! Sio wa kutafutwa! Ni wa kukamatwa! Kama hamna dhamira ya dhati acheni! Watanzania wana akili wala hawawezi kudanganywa katika hili!