Kushambuliwa Tundu Lissu: Mwigulu aahidi vyombo vya dola vitawatia mbaroni watu wasiojulikana!

HOMBOY

JF-Expert Member
May 16, 2016
1,432
924
upload_2017-9-26_18-6-16.jpeg


Singida. Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba amesema hakuna haja ya kuanza kuhangaika kutafuta wachunguzi kutoka nje kwa ajili ya kufuatilia wahusika wa shambulizi la Mbunge wa Singida Mashariki(Chadema), Tundu Lissu kwa vile vyombo vya ulinzi na usalama nchini vinajitosheleza na vina weledi na kazi hiyo.

Waziri huyo amesema haoni kwa nini baadhi ya watu wanasisitiza kuletwa kwa wataalamu wa nje kwani hata kama wataletwa bado watalazimika kufanya kazi kwa mazingira ya Kitanzania wakitumia wataalamu waliopo na hata ikiwekezana watahukumiwa kwa kutumia sheria za nchini.

“Nchi yetu inajitegemea hakuna haja ya kuleta vyombo vya nje kufanya uchunguzi...upelelezi utafanywa na vyombo vyetu, watafikishwa katika vyombo vya muhumu na watahukumiwa na watoto wetu,” alisema.

Hivi karibuni Chadema ilitaka wachunguzi nje kuendesha upelelezi kuhusiana na tukio la kushambuliwa kwa Lissu ikidai kuwa hatua yake hiyo haimaanishi kuwa vyombo vya ulinzi na usalama havina uwezo bali vimetuhumiwa katika tukio hilo.

Hata hivyo, Waziri Nchemba alisisitiza kuwa vyombo vya ulinzi na usalama daima viko macho na vinaendelea na kazi ya kuwasaka wale wote wanaojihusisha na matukio ya kushambulia watu.

Amesema suala la uchunguzi haliwezi kukamilika kwa siku moja akitolea mfano jinsi Marekani ilivyotumia muda mwingi kumsaka mtuhumiwa wa ugaidi, Osama bin Laden aliyekuwa kiongozi wa kundi la Al Qaida.

“Uchunguzi hauna ukomo...unaisha pale tu wanapokamatwa wahusika wote lakini vinginevyo uchunguzi hauishi maana hata Marekani walimtafuta Osama kwa muda mrefu sana hawakusema sasa tumesitisha kumsaka,” amesema.
Kiongozi huyo wa Al Qaida aliuawa Mei 2, 2011 na vikosi vya Marekani vilivyoendesha operesheni maalumu iliyoratibiwa kutoka Pentagon na kufuatiliwa kwa karibu na Rais Barack Obama ambaye hivi sasa amestaafu.

Osama alikuwa amejichimbia katika maficho yake nchini Pakistan katika eneo lililojulikana Abbottabad.

Waziri Nchemba aliwatumia salamu wale wanaojulikana kama ‘watu wasiojulikana’ akisema kasumba ya wahalifu wachache kufanya mauaji na kisha kujinadi kwa jina la watu wasiojulikana inaelekea ukingoni.

Ameeleza kuwa dakika za wale wanaojihusisha na uhalifu huo kufikishwa kwenye mkono wa sheria zinahesabika.
 
Kwa maoni yangu tu lakini; Namshauri Mh Mwingulu, ili kuiosha serekali yetu tukufu na pia jeshi letu pendwa la polisi, waseme hivi; Kama mlimpeleka wenyewe Nairobi kutibiwa, basi malizieni pia kwa kuwaleta hao wapelelezi wenu waje kupeleleza kwa gharama yenu.
Si Chadema wanataka hayo?? Wapeni ruksa kwani mtoto akililia wembe mpe.
 
Mi huwa najiuliza kila siku tofauti kati ya ngedere, nyani, kima, tumbili, sokwe, chimpanzee, gorilla et al.

Hope ipo siku ntapata tofauti yao.
 
Criminal state! Frankly speaking, If were him I would never waste my time and energy making comment on such a matter.
 
Rahisi Tu Cdm Watumie Ij(investigation Journalism) Wa Ndani Ikiwezekana Hata Wa Nje Km Bbc,kipindi Kile Cha Slaa Cdm Walikuwa Wazuri Sna Kwnye Masuala Km Haya Walikuwa Wanadukua Mawasiliano Ya Wanaowashuku Nakuanika Kwnye Mawio Sijui Kinashindikana Nn?
 
Najuta kusoma huu ujumbe. Maana hawako sriaz na hili swala. Mungu yupo atawakamata tu. Walifanya kwa yeye atafanya mchana kweupe
 
Huyu mwigulu hakuelimika Bali ali-graduate

Hakuna aliyesema vyombo vyetu havina weledi wa kushughulikia suala la Lissu. Tatizo ni kuwa according to CHADEMA serikali ni kati ya SUSPECTS wa shambulio hilo hivyo wanapoteza credibility ya kuchunguza suala hili..
 
Waziri wa mambo ya ndani mh Mwigulu Nchemba ameahidi kwamba vyombo vya dola lazima vitawatia nguvuni watu ' wasiojulikana' waliomdhuru ndugu yetu Lissu pamoja na jenersli wa jeshi na yule hakimu wa kule Mtwara. Amesema watu hau wanaotajwa kama ' wasiojulikana' siku zao zinahesabika. Source EATV habari!
 
Waziri wa mambo ya ndani mh Mwigulu Nchemba ameahidi kwamba vyombo vya dola lazima vitawatia nguvuni watu ' wasiojulikana' waliomdhuru ndugu yetu Lissu pamoja na jenersli wa jeshi na yule hakimu wa kule Mtwara. Amesema watu hau wanaotajwa kama ' wasiojulikana' siku zao zinahesabika. Source EATV habari!
HUYU NAYE NI TATIZO KUBWA.
 
Back
Top Bottom