Mwezi wa Ramadhani,wengi wanashinda njaa,wengine wanafunga

Idd Ninga

JF-Expert Member
Nov 18, 2012
5,136
4,297
SIFUNGI NASHINDA NJAA.

1)Siku yangu imeisha,bila hata ya kuswali

Funga nimetamatisha,na mengi yangu maswali

Funga yangu bila swala,sifungi nashinda njaa.

2)Hii yangu funga gani,hata swala sijafanya

Siendi msikitini,madhambi nayakusanya

Funga yangu bila swala,sifungi nashinda njaa.

3)Swala ni nguzo ya dini,ila Mimi nimeacha

Sijui nafanya nini,bila ya mungu kumcha

Funga yangu bila swala,sifungi nashinda njaa.

4)Funga ya kubahatisha,misingi sijaishika

Na hofu inanitisha,siku zaanza katika

Funga yangu bila swala,sifungi nashinda njaa.

5)Funga haina furaha,kumbe nimeacha swala

Hii funga ya karaha,kama nimetiwa jela

Funga yangu bila swala,sifungi nashinda njaa.

6)Mola wangu ninusuru,nisije pata khasara

Siwe kwenye msururu,kuona yako khasira

Funga yangu bila swala,sifungi nashinda njaa

7)Bure nitajikondea,bila hata ya faida

Muda nao wapotea,sipati hata ziada

Funga yangu bila swala,sifungi nashinda njaa.

8)Funga ya namna gani,mwenzenu ninayofunga

Hakika nipo shakani,Funga ya kuunga unga

Funga yangu bila swala,sifungi nashinda njaa.

SHAIRI-SIFUNGI NASHINDA NJAA

MTUNZI-Idd Ninga,Arusha

iddyallyninga@gmail.com

+255624010160
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom