figganigga
JF-Expert Member
- Oct 17, 2010
- 25,658
- 55,485
Na Sehba Khan
Tende
Mtume, swallallahu alayhi wa sallam, amesema, “Fungueni swaumu zenu kwa tende, au, vinginevyo, basi fungueni kwa maji, kwani ni twahara.” (Abu Dawud na Tirmidh).
Chakula kilichozoeleka zaidi kwa futari ni tende. Hii inaendana na Sunna ya Mtume, swallalllahu alayhi wa Sallam. Baada ya kushinda kutwa nzima na swaumu, kiwango cha sukari ya mwili hupungua na hivyo, kuhitaji kujazilizwa tena.
Aina ya kwanza ya sukari itumikayo mwilini na hasahasa ubongoni ni glukosi. Mshuko wa sukari walioupata wale ambao hawakula au kunywa kwa kipindi kirefu, unaweza kusababisha ulegevu na kiyangayanga (distraction).
Pindi sukari inapoliwa kwa njia ya chakula au kinywaji, viwango vya glukosi ya mwili hujisawazisha vyenyewe na kumfanya mtu aliyefunga asijihisi kuchoka sana na huwa na nuru zaidi ya macho.
Ingawaje tende, mara nyingi, si chakula kinachopendelewa sana na watu wenye njaa, lakini ndicho chakula kisicho na mafuta, na ni chanzo madhubuti cha sukari.
Nusu ya sukari zitolewazo na tende ni kwa ajili ya glukosi pekee. Usambazaji wa haraka-haraka wa glukosi itokayo kwenye tende huusaidia mwili kuodokana upesi na hali ya ulegevu kiasi kwamba mtu aliyefunga huweza kujimudu sawasawa katika ibada.
Mbali ya glukosi, tende pia ni chanzo kizuri cha nyuzinyuzi ambazo huwezesha michakato ya umeng’enyaji mwilini kuendelea, na huzuia tatizo la kushindikana kwa michakato hiyo ya uyeyushaji wa chakula mwilini.
Vilevile tende ni chanzo kizuri cha potasiamu, madini ambayo ni muhimu kwa usawazishaji wa maji mwilini. Mtume, swallallahu alayhi wa sallam, alikuwa na kawaida ya kula tende kwa idadi ya witiri.
Hivyo, wale ambao hawapendelei ladha ya tende wanaweza kupata manufaa ya chakula hiki kwa kula angalau tende moja, na wale wanaopendelea tende, basi wanaweza kula tatu, tano, na kadhalika.
Maji
Mwili wa binadamu, kwa kiasi kikubwa, unajengwa na maji. Faida za maji ni kubwa. Kama unavyohijati sukari kujirudishia nishati upesi, ndivyo unavyohitaji maji kujijazilizia ili uweze kufanya kazi vizuri.
Sio tu maji huurudishia mwili maji upesi na kukata kiu, bali pia ni kisafishio asilia cha uchafu na sumu ambazo zimejilimbikiza kwa muda fulani.Kwa kutwa nzima, mtu mzima mwenye afya nzuri, hushauriwa kunywa jumla ya vikombe vinane ([http://islamictides] vya maji.
Hii haijumuishi yale maji yatokanayo na vyakula (kama vile matunda na mbogamboga). Kwa vile mtu aliyefunga huwa hanywi maji muda wote wa swaumu yake, basi naye anahitajika kufikisha kiwango hicho cha unywaji wa maji (vikombe [http://islamictides] kabla ya daku na baada ya futari.
Inapendekezwa hivi, kwamba mwanzoni mwa kufuturu, mtu anywe kiasi kidogo cha maji (nusu kikombe au kikombe kimoja), na baada ya kufuturu, anywe maji kwa viwango vidogo muda baada ya muda (mathalani Nusu kikombe au kikombe Kimoja kila baada ya saa moja). Hii itaepusha ujazo mkubwa wa maji tumboni kwa wakati mmoja na itarejesha maji mwilini kidogo kidogo kabla ya swaumu inayofuata.
Kahawa na Chai
Jamaa yangu mmoja aliwahi kunisimulia kuwa yeye alikuwa akiwaona Waislamu nchini mwake wakifungua swaumu zao kwa vikombe viwili au vitatu vya kahawa.
Sio tu utumiaji wa vinywaji vya kahawa na chai huonekana kukata kiu, bali pia hushitua bongo lililodorora baada ya swaumu ya mchana kutwa, na huzuia maumivu ya kichwa “yachokozwayo na swaumu”.
Hata hivyo, katika mwezi wa Ramadhani, unywaji mwingi wa kahawa na chai uepukwe kwa sababu kafino (caffeine) iliyomo kwenye chai na kahawa husababisha ongezeko la safari za haja ndogo. Hii huongeza kiwango cha upungufu wa maji mwilini, jambo ambalo si zuri kwa mwili ambao unahitaji kujazilizwa maji.
Mbali ya hivyo, unywaji mwingi mno wa kahawa unaweza kusababisha mawengewenge na wahaka (hali ya wasiwasi). Mtu ajitahidi kutokunywa zaidi ya miligramu 300 (karibu sawa na vikombe viwili au vitatu) vya kahawa kwa siku nzima.
Kikombe kimoja kinaweza wakati wa daku ili kuzuia maumivu ya kichwa yawapatayo wale waliozoea kunywa kutwa nzima. Inashauriwa kupunguza kidogo kidogo unywaji wa kahawa katika miezi inayoikaribia Ramadhani ili kujikinga na athari za kuacha kahawa wakati wa swaumu.
Maziwa
Yakiwa na takribani asilimia 90 ya maji, maziwa pia ni chanzo kizuri cha laktosi (lactose), hii ni sukari inayovunjwvunjwa na kuwa glukosi mwilini. Mbali ya kusaidia kupandisha viwango vya sukari kwenye damu, maziwa ni chanzo kizuri cha kalisiamu, fosiforasi na potasiamu.
Wakati wa kufuturu, maziwa yanyweke hivi hivi, yachanganywe na sikirimu (ice cream), yatengenezwe yawe ya unga kwa kutumia sukari na maji. Kuchanganya na sikirimu na kutengeneza unga huo kunaongeza kiasi cha nishati lakini hii pia inaweza kuzidisha sukari nyingi mno na kumfanya mtu awe mchovu zaidi.
Isitoshe, maziwa yakizidi mno huweza kusababisha misokoto na adha tumboni kwa sababu ya unywaji mkubwa wa laktosi. Wakati wa kufuturu, inashauriwa kuwa mtu kwanza anywe kikombe cha maziwa na asubiri hadi baada ya swala, kisha aendelee kunywa zaidi.
Matunda na Juisi za Matunda
Kwa rangi, maumbo na ladha zao mbalimbali, matunda huleta shauku zaidi ya futari. Si tu matunda yanatia mwilini vitamini na madini teletele kama vile Vitamini C, potasiamu, na folati, bali pia ni chanzo kizuri cha majimaji na nyuzinyuzi.
Yakiwa na fruktosi ambayo ni sukari inayovunjwavunjwa na kuwa glukosi mwilini, matunda pia ni chanzo kizuri cha nishati mwilini. Si mazuri sana kama tende wakati wa futari kwa sababu wastani wao mkubwa wa kiwango cha nyuzinyuzi hukawiza utokaji wa sukari mwilini.
Asilimia 100 ya juisi za matunda nazo huupatia mwili vitamini hizo hizo, madini hayo hayo na sukari hiyo hiyo, lakini ni vyanzo duni vya nyuzinyuzi. Hata hivyo, ni kikombe kimoja tu cha asilimia 100 ya juisi ya matunda ndicho kinachohitajika kuusaidia mwili kujiweka sawa.
Watu wengi huishia na kikombe kimoja au viwili vya juisi ya matunda ambavyo pia vinaweza kusababisha uchovu unaohusishwa na unywaji wa sukari nyingi kupita kiasi.
Njugu
Jamii ya Njugu ikiwa ni pamoja na ulozi, korosho, njugumawe, ni vyanzo vya kalori nyingi ya protini, chuma, Vitamini E, na asidi muhimu za mafuta. Ni kile kiwango chao kikubwa cha kalori ndicho kinachoweza kuvifanya vyakula hivi viwe tatizo badala ya kuwa na manufaa. Gao moja la njugu linatosha kukidhi mahitaji ya siku ya mwili.
Mapochopocho
Kwa baadhi ya wafungaji Ramadhani haiwi Ramadhani bila karamu ya mapochopocho na vitamutamu wakati wa kufuturu. Sukari na mafuta katika vyakula hivi huburudisha kinywa, na wakati huo huo, hufurahisha nafsi iliyojinyima chakula na maji kutwa nzima.
Mara nyingi, vyakula hivi ndivyo vinavyoliwa pale familia, ndugu na jamaa wanapojumuika pamoja kufuturu. Baadhi yetu tunajua kuwa vyakula hivi, vinapoliwa kupita kiasi, husababisha ongezeko lisitakiwa la uzito wa mwili.
Kwa vile shahamu (mafuta) ndiyo huwa kirutubisho cha mwisho kumeng’enywa, vyakula vya kuaangwa na vyenye kalori nyingi huweza kukaa tumboni kwa muda mrefu na kusababisha adha ya matatizo ya uyeyushaji ikiwa ni pamoja na kiungulia na maumimu ya tumbo.
Hii haina maana kuwa mtu aepuke kabisa kula vyakula hivi. Badala yake, mtu akazanie zaidi kula tende na kunywa maji au maziwa, huku akila vipochopocho na vitamu-tamu kwa siku chache na kwa kiasi kidogo
Jinsi ya Kudhibiti Uzito wa Mwili
“Enyi mlioamini! Mmelazimishwa kufunga kama walivyolazimishwa waliokuwa kabla yenu ili mpate kumcha Mungu.” (2:183)
Kwa Muislamu, Ramadhani ni kipindi cha kujenga maisha ya kiroho ya jamii na ya mtu mmoja-mmoja. Umakini mkubwa katika kipindi hiki uwe katika chakula.
Mtu anapokuwa na njaa na anapokuwa katika mjumuiko, ni rahisi kula kupita kiasi na kuongeza uzito wa mwili hadi kumalizika kwa Ramadhani. Ingawaje binafsi sipendekezi Ramadhani wakati mzuri wa kujipunguzia uzito, lakini pia si wakati wa kujiongezea uzito.
Ili kudhibiti ongezeko la uzito wa mwili, mazingatio ya mtu yasiwe katika kula na kufurahisha tumbo, bali mazingatio yawe katika kumtii na kumshukuru MwenyeziMungu ambaye ndiye aliyejaalia riziki iliyopo mezani au mkukani. Utii sahihi usichanganywe na kuvimbewa kwa sababu ya kula futari kupita kiasi.
Inashauriwa na tena ni jambo linalothibitika katika sunna ya Mtume, swallallahu alayhi wa sallam, kufungua swaumu kwa tende halafu ndipo mtu aswali.
Pale iishapo Swala, damu ya mtu itakuwa imerekebishwa ambapo tamaa ya kula sana itakuwa imepungua. Hapo sasa ndipo chakula cha futari kiliwe. Kanuni iwe hii kwamba mtu asikilize mahitaji ya mwili wake na aache kula anapofikia nusu ya shibe.
Swahaba mmoja Al-Miqdam ibn Ma’diy-karib kasimulia: “Nilimsikia Mtume wa MwenyeziMungu akisema: “Hajawahi mwanadamu kujaza vibaya chombo chochote kama anavyolijaza tumbo lake. Yanamtosha mwanadamu matonge kadhaa ya kunyoosha mgongo wake. Lakini ikibidi, basi theluthi moja (ya tumbo) iwe kwa ajili ya chakula, theluthi moja iwe kwa ajili ya maji na theluthi moja iwe kwa ajili ya pumzi.” (Ahmad na Tirmidhi).
Kula kwa Wastani na Shukuru
Kufutari ni wakati wa furaha kwa Waislamu ulimwenguni kote. Hufungua swaumu zao kwa aina mbalimbali ikiwa ni pamoja tende na maji. Kuna ule utamaduni wetu wa kufuturu pamoja. Sio tu tuhimize umoja huo, bali pia tuzingatia afya zetu. Ifuatayo ni chati ya vyakula na vinywaji vya kufuturia pamoja na faida zake kwa afya zetu.
Vyakula vyote vyaweza kuleta madhara vinapoliwa kupita kiasi. Ni muhimu, hasahasa katika Mwezi huu wa Ramadhani, kula vyakula vyetu kwa wastani. Kwa kufanya hivyo, tutaondosha njaa na kuacha nafasi ya kujaza ndani ya roho zetu dhikri na shukurani kwa MwenyeziMungu.
Mapendekezo ya Mlo wa Futari
Chakula cha Futari
Kiasi cha kula kinachopendekezwa
Faida Zake
Hasara za Kula mno
Tende
Kula kwa idadi ya witri kwa kufuata Sunna ya Mtume
Ni Chanzo cha haraka cha glukosi kurejesha sukari ya damu katika kiwango chake cha kawaida; chanzo kizuri cha potasiamu na nyuzinyuzi
Adha ya Tumbo
Maji
Kunywa Kikombe Kimoja wakati wa kufuturu, na baada ya futari, kunywa kikombe kimoja kila baada ya saa moja
Kurejesha maji mwilini
Kujisikia ovyo kwa sababu ya maji mengi kujaza tumbo
Kahawa au Chai
Isizidi miligramu 300 (kwa mfano, vikombe viwili vya kahawa)
Inaongeza Muda ya kubaki macho, inasadikika kupambana na magonjwa ya moyo na saratani
Upungufu wa maji mwilini (kwa safari za haja ndogo), wahaka (anxiety) na mawenge (nervousness)
Maziwa
Kikombe Kimoja
Ni chanzo cha Majimaji na Nishati; ni chanzo cha Kalisiamu, fosforasi, na potasiamu
Adha ya tumbo; ulegevu, hasa inapochanganywa na sikirimu au majimaji ya sukari
100% ya Juisi ya Matunda
Kikombe Kimoja
Ni chanzo cha majimaji; Chanzo cha Fruktosi na Vitamini C na potasiamu
Kulala-lala, Kuchoka-choka
Matunda
Kipande Kimoja kidogo cha tunda au ndizi
Ni chanzo cha Fruktosi; sukari ya asili na majimaji ya asili; Ni Chanzo cha Vitamini C, Potasiamu, na nyuzinyuzi
Adha ya tumbo kwa sababu ya wingi wa kupita kiasi wa nyuzinyuzi
Jamii ya Njugu
Gao moja dogo
Ni Chanzo kizuri cha nishati;Chanzo muhimu cha asidi za mafuta, na Vitamini E
Ongezeko la Uzito wa Mwili
Mapochopocho na Vitamutamu
Kidogo tu
Huburudisha kinywa na nafsi; chanzo cha haraka cha kalori
Ulegevu, tatizo la uyeyushaji tumboni; Ongezeko la Uzito wa mwili.