Mwenzenu ni mgonjwa hoi kitandani!

Zinduna

JF-Expert Member
Nov 6, 2011
2,378
3,379
Habari zenu wana JF wapendwa.Ni wiki ya pili sasa niko hoi kitandani baada ya kufanyiwa operesheni .....No, sorry nilikuwa namaanisha upasuaji wa kidole tumbo. Unajua kuna maradhi mengine ukiyatamka kwa kiingereza yanavutia tofauti na kuyatamka kwa kiswahili. kwa mfano ni vyema kusema nina Appendex badala ya kusema nina kidole tumbo, au ni vizuri ukisema una diarrhea badala ya tumbo la kuhara, au kusema nina typhoid badala ya kusema nina homa ya matumbo.

Vile vile ni vyema kusema unaumwa tonsils badaya ya kusema unaumwa mafindofindo, au kusema unaumwa AIDS badala ya kusema una UKIMWI.Si mmeona majina ya maradhi yakitamkwa kwa kiingereza yanavyovutia.

Ndio sababu na mie nikasema nimefanyiwa operesheni ya appendex badala ya kusema nimefanyiwa upasuaji wa kidole tumbo.
 
Kwa hiyo walipasuwa injini, wakashusha kilicho chao then wakakuacha na mshono, pole sana dadangu.
Ila kuna kitu hakiko sawa kwenye post yako, umedai uko hoi kitandani, wakata fizikia ya bandiko lako inaonesha kuwa hauko hoi, though unaweza usiwe mzima pia. Mshukuru Muumba kwa afya kidogo uliyonayo, angalau umeweza kupost humu...
WISHING YOU A QUICK RECOVERY!
 
upone upesi....
Kuna wadau wanataka kutaifisha shoo yako....
Ukiendelea kuumwa kiduchu tu utakuta hati miliki ishayeya.....
 
Aisee pole, ndio maana tulikosa show yako this weekend!
Get well sooner!
 
Wacha kudeka bibie. kidole tumbo unakaa kitandani wiki mbili? Nambie basi unapatikana wapi nije nikupe pole.
 
pole sana,inaonekana kuna talk show ulifanya imekukosti,nazan huyu atakua Erickb52 maana aka kajamaa kamwanga ile mbaya,ila kashindwa in ze neimu of jizazi
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Back
Top Bottom