Mwenzenu Narogwa au?

Ndibalema

JF-Expert Member
Apr 26, 2008
10,956
4,648
Wadau naomba msaada wenu.
Nipo kikazi huku kusini mwa Tanzania. ni karibia wiki moja sasa, na nitakaa kwa wiki nne.
Mara ya kwanza nilifikia katika gest moja hivi ya kawaida tu. Lakini kuna rafiki yangu ambaye anaishi huku aliniomba sana nikafikie kwake.
Nami bila hiana nikakubali, sasa naishi kwakwe.
Sasa cha ajabu kila nikiamka asubuhi nakuta nimechanjwa mwilini yaani kama nilijikwaruza hivi kwenye michongoma. Mara ya kwanza nikapuuzia.
Jana kabla ya kulala, baada ya sala nikaamua kulala na kitabu cha dini ninayoiamini.
Lakini leo nimeamka asubuhi, hadi usoni sasa nimekuta nina alama za kuchanjwa chanjwa.
Nimemweleza rafiki yangu kasema ni mambo ya kishirikina tu endapo nitayapuuzia basi sitopata madhara yeyote.
Kwa mwenye kuwa familiar na mambo kama haya, nini mwisho wa haya yote yanayonikuta?
Nifanye nini mwenzenu kwani hofu inanizidi sasa.
 
Nenda kalale Gest Bwana huyo rafiki yako labda anaishi Gamboshi usiku:becky:

amini katika mungu hakuna jambo linalomshinda yeye
 
Kama shida hiyo imekuanzia hapo kwa jama yako, basi shida itakuwa kwenye nyumba hiyo. Muage huyo mwenyeji wako. Nenda kapange guest. Endelea pia kusali na kumtegemea Mungu.
 
Pole sana mkuu, wahi Gesti tena rudi ile uliyolala kwanza kabla ya kuhamia kwa jamaa !
 
Ukiwa guest hakikisha kabla ya kulala unapata glasi moja ya bia ukikosa hiyo lala na goma. wachawi huwa hawatii mguu katika hali hizo
 
Ukiwa guest hakikisha kabla ya kulala unapata glasi moja ya bia ukikosa hiyo lala na goma. wachawi huwa hawatii mguu katika hali hizo

Goma unamaanisha mdudu a.k.a kitimoto?
Kuhusu pombe sinywi nilishaacha zamani sana.
 
Kwa sasa hata ukikimbiilia gesti haisaidii maana jamaa ameshapata alichotaka.Hapo atakuwa alitaka damu ya mtu kidogo kwa ajili ya mambo yake.Hivyo jamaa kukuchanja ni ili kuipata hiyo damu,kwa sasa hiyo damu atakuwa ameisemea maneno ambayo hata ukikimbia haisaidii.
Unaweza kuyafuta maneno yote aliyotamka ili yasikupate kwa kutumia damu ya Yesu.Sema nafuta maneno yote yaliyotamkwa juu yangu kwa jina la Yesu.Imeandikwa Hakuna silaha yoyote itakayofanyika juu yangu itakayofanikiwa na kila ulimi utakaoinuka juu yako utauhukumu mkosa.Weka imani yako katika mistari ya biblia na usitetereke vinginevyo utapatikana.Kumbuka Mungu hasikii maombi ya mwenye dhambi.Kama unaishi katika dhambi,omba sala ya toba na umpokee Yesu mara moja halafu endelea na shughuli zako,hakika yake hakuna baya litakalokupata.
 
sawa nitahama. Na hizi chale ambazo tayari ninazo mwilini kwangu hazinamadhara?

Wala usifikirie sana kuhusu hizo chale. Hutadhurika chochote. Ila nashauri ushike Doria usiku kucha uweze kudadisi ni nini linakusibu. Ukishindwa basi hamia guest house. Umwambie rafiki yako lakini usimwambie jina la guest house hiyo. Ubarikiwe sana.
 
sawa nitahama. Na hizi chale ambazo tayari ninazo mwilini kwangu hazinamadhara?

Pole aisee. Kamuone physician. Hicho kifaa kilichotumia kukutia chale kisije kikawa kimetumika kabla kuchanja wengine bila kuwa 'sterilized'.
 
Mtumaini Mungu kwa kila jambo hakuna linaloshindikana kwake, usiwe na imani haba. Tafuta hata maji ya baraka kama ni mkatoliki nyunyuzia chumba kizima na kitandani kisha sali utalala kwa amani
 
Back
Top Bottom