Evarm
JF-Expert Member
- Aug 30, 2010
- 1,936
- 1,400
Ninalia hadi sauti yanikauka yote haya ni sababu ya mapenzi. Ni dada ambaye nipo kwenye uhusiano kwa mwaka wa nne sasa na mchumba wangu. Nampenda sana, ni mwanaume wangu wa kwanza lakini jumamosi ya juzi amenifanyia kitu mbaya sana kila nikumbukapo naona ni bora niwe mwenyewe kwani Mungu kanijalia kazi nzuri tu ambapo napata mahitaji yangu yote bila ya msaada wa mtu yeyote. Nipo naye mbali ingawa kwangu mimi si mbali hata kidogo sababu kila wikiendi naweza kwenda huko alipo na pia Dar ni nyumbani (tunafanya kazi mikoa tofauti yeye yupo Dar).
Hivi karibuni alikuja kunitembelea hapa kwangu ninapoishi tukapiga stori/tukala na kufurahi na baadaye nikaweka filamu fulani tukawa tunaangalia. Na ndio hapa yote yalipoanza, simu yake ikaanza kuita imeita kwa mara ya kwanza hakupokea, ilipoita kwa mara ya pili nikamwambia pokea simu mbona inaita. Akapokea, akaanza kuongea na huyo mtu (ni dada). Alivyokuwa anaongea huyo dada alikuwa anamlalamikia, halafu akasema anaumwa, mchumba akamuuliza umetumia dawa? Pia akasema bado kuna tatizo mchumba akamuuliza tatizo ni vocha? Akajibu hapana ila kuna tatizo, mchumba akakata simu. (sikuwa na uwezo wa kusikia yote yanayoongelewa na mdada)
Muda si mrefu (baada ya dakika kama moja) yule dada akapiga tena akamwambia kwanin anamkatia simu? (muda wote huo nimesimamisha filamu ili yeye aongee maana yake hataki kelele yoyote) wakaendelea na maongezi (sikuwa na uwezo wa kusikia yote) huku mimi nasikiliza baadhi ya maneno lakini huyu dada alikuwa analalamika sana. Alipomaliza nikamuuliza ulikuwa unaongea na nani? Mchumba akanidanganya ya kuwa ni mfanyakazi mwenzie wa kazini, mi nikajibu si kweli kwani analalamika sana, pia ile idara anayofanyia kazi ni wanaume watupu (ni engineer wa kampuni Fulani Dar).
Mara ya tatu akapiga huyu dada wakaongea tena huku mimi nimekaa hapo pembeni, roho yangu ilikuwa inauma sana sababu nilikuwa naona ni hawara yake kwa jinsi alivyokuwa mchumba anaongea, nikakaa zangu kimya. Mchumba akamkatia tena simu
Haijapita hata dakika dada huyu akapiga, nikamnyanganya simu mchumba na kuongea na huyo dada. Akaniambia anataka kuongea na mwenye simu, mm nikajibu amelala (Mungu nisamehe nilidanganya) kwani ana shida gani? Yule dada akasema siwezi kukuambia shida zangu wewe nipe niongee na Abu. Akaniuliza kwani wewe ni nani yake? Mimi nikajibu ni gf wake, akasema nipe niongee na mchumba wangu huyo! Nikamuuliza mmekuwa kwenye mahusiano kwa muda gani? Akanijibu hyo si kazi yangu kujua, yeye shida yake ni kuongea na Abu. Nikakata simu.
Nikamrudishia simu na akazima kabisa na mchumba hakuwa na amani hata kidogo. Hapo ndio nikaanza kumhoji huyo ni nani yake akajibu ni rafiki wa dada yake anayeitwa Tuma (hapa nalidanganywa sababu ni tofauti na aliponijibu mwanzoni), nikamuuliza huyu dada umekuwa kwenye mahusiano naye tokea lini akajibu tokea katikati ya mwaka huu.
Roho imeniuma sana nakawa naona uchungu wa hali ya juu. Wanaume si waaminifu hata kidogo. Nililia kama mtoto mdogo, nikatoka nje huku nalia. Nikakaa huko baada ya dakika kumi nikarudi, nikamwambia mchumba naomba aendelee mahusiano na huyo dada, aniache mimi. Alinisihi sana nisifanye hivyo ila sikuwa radhi.
NB: Kumbuka ya kuwa anafanya hivyo huku akiwa nyumbani kwangu yaani hapa ninapoishi, yaani nahisi alinidharau kupita kiasi.
Nikamuomba yeye alale chumba kile na mimi nilale chumba kingine, akalia sana huku akiomba msamaha ya kuwa nimsamehe na hatorudia tena. Lakini roho yangu yaniambia hii si kweli kwani alishawahi kunicheat mara kadhaa huko nyuma na nilimsamehe kwa yote, lakn sina amani nae tena, wala raha nae kama zamani.
Mchumba aliendelea kuomba msamaha huku akisema yupo tayari afanye lolote nitakalosema, nilimjibu inabidi akae chini na kuamua ni nani anayempenda kati ya mimi au huyo dada, yeye alijibu hamtaki huyo dada nikamwambia inabidi ampigie simu huyo dada na kumwambia ukweli. Alipowasha simu ikaingia msg kutoka kwa yule dada ya kuwa anataka kuhakikishiwa kutoka kwa mchumba ya kuwa yale aliyoongea nami ni kweli, muda si mrefu yule dada akapiga simu, mchumba akapokea akajibu ya kuwa ni kweli yule dada alisikitika sana. Asubuhi yake alipanda basi la kurudi huko Dar.
J3 nikamwambia mm sina amani naye tena naona ni bora niachane nae, mchumba akajibu hayo ni maamuzi ya haraka nikae kwa muda wa wiki moja halafu nimpe jibu kamili ya kuwa nimeamua nini kati ya kuachana nae au kuendelea na haya mahusiano.
Wapendwa sina raha juu ya hili tukio lililonitokea jumamosi ya juzi mida ya jioni. Nimevumilia mengi sana. Nahisi kama ataendelea kunicheat kama huko mwanzo aliweza na hata sasa ameweza nahisi atakuwa anaendelea tu kwani yawezekana ana wanawake wengi.
Nahitaji mawazo yenu, ushauri kuhusiana na huyu mchumba kwani nakosa amani, nakonda kila leo nikikumbuka hili.