Mwenzenu nalia, naomba msaada!

Samahani kama ntakuumiza ila wewe jamani kama mtu alishacheat MARA KADHAA na ukamsamehe (meaning umekubali upungufu wakehuo) unalalamika nini akiendelea???Wakati unamsamehe mara zote hizo ulitegemea nini??Kwamba atajifunza kutokana na msamaha wako???

Ingekua hii ni mara ya pili ningeelewa malalamiko yako kwasababu ungekua ulimsamehe mara moja akaahidi kutorudia ukamwamini ila akajunja ahadi yake. Ila sasa wewe mara kadhaa....zote anatoa ahadi ya kuacha na bado haachi what did you expect???

Neway umeshajua ni mtu wa aina gani...sasa amua kama uko tayari kuishi maisha ya kuwa-cheated kila siku uendelee nae kama sio uangalie ustaarabu mwingine. Maana matumaini ya kubadilika hapo ni madogo kwakua umeshamzoesha kua utamsamehe...hivyo hajali sana matokeo ya matendo yake.

umemwambia vema.
Kwa staili ya msamaha alokuwa akigawa, ni ngumu huyo BF kujifunza na kujirekebisha...si anajua atasamehewa tena.
 
Achana nae. Ona tu mwenyewe what appears to me:

Anahishi Dar, na huyo dada anahishi Dar. Huyo dada hakujui (hajaambiwa kuhusu wewe) na 'mchumba wako' anampenda kiasi kwamba alishindwa kabisa kumwambia asimpigii coz anamkera yeye akiwa na wewe. Milivo amka yeye akarudi dar... Unadhani inakuwaje kule? How do you know hayoko katika harakati za kuomba na yule amsamee? maana kule kasema kuhusu wewe na huku kasema kuhusu yeye, now he is trying to solve huku, maybe he is also trying kule?
Kumbuka ni mtu sio mwaminifu sana as alisha wahi kukukosea in the past...
Sio Mume, hamjaanza hata maisha ya pamoja tayari anakuonesha vitu kama hivyo...
Ushahuri wangu: Achana nae...
Na usiulize sana watu kuhusu hatua ya kumchukulia, watazidi kukuchanganya. Hata mimi hapa nasema kutokana na haya umetwambia ila sijui uzuri wake na ubaya wake... Just think for yourself and decide for yourself.

umemwambia vema.
Bora afanye maamuzi magumu mapema, ili asipoteze mda zaidi, umri ukaenda, akaanza kuchuchuka akaonekana mzee akakosa mchumba buree!
 
Lol. Kama kulia watu tushaliliwa saana; wanaume wengine kulia ni hobby. Unakuta analia kwa wote wawili chezea. Hizo treak ni za kuwadanganya teenagers. Ulie, usilie umechiti; ungejua kuna kilio usingechiti at first place.


I wish ningerudi ujana wangu. Nimemiss adventures. Msichana kuringa bwana. Tuache tulo kwenye ndoa tujiulize mara mbili ila nyie mso na mkataba wala watoto what is that that is making you stick with a person that makes you cry.

Atakuwa anakuchiti analia unamsamehe; miaka inasonga kukuoa hakuoi; ukijashtuka 35 unaanzisha thread ya kuomba ushauri wachumba wamegoma. Kiwingu hicho dada; kiwingu; hakuna atakayekutokea ukiwa kwenye relationship; hata wewe huwezi ona wengine. Zinduka.

Hata akikuoa nina mashaka ndo hao wanaosema (hata humu JF)" ooh kuchiti lazima kwani hata wakati naoa nilikuwa na wasichana watatu kwa hiyo siwezi kuwaacha ghafla". Kuna mtu aliandika hivi kwenye thread ya cheating; I felt sick na huruma yani mtu unaanza ndoa day one na a cheating husband.

umemwambia vema, kama amekuelewa, atafaidi sana kwa ushauri wako. KULIA hata kwenye movie mbona wanaliaga tu. Usidanganywe na kulia.
 
Wanaume watamu jamani...chukua mda kisha fanya maamuzi sahii..tafuta anayekufaa na asiye kuumiza moyo wako.
 
Pole sana, punguza mawazo. Na pia usichukue uamuz wa haraka. Tulia kwa muda muweke huyo mchumba mtegoni, mtege na umpime kama anaweza kubadilika. Ukiona anaweza endelea nae.

Hata hvyo naweza kusema na ww pia una tatizo, why uchumba tu miaka minne? Umesema una kazi nzuri na yeye pia sasa kipi kinachowafanya msioane? Sisemi muoane kama bado hamjawa tayari ila at least angekua mume wa ndoa ile security ingekuwepo na ungejua unambana vipi ila haya mambo ya uchumba tu na kuonjana mmh kazi ipo.
Mungu Akusaidie

Hapo kwenye rangi nyekundu, nimeshawahi kumuambia lakini alinijibu hayupo tayari kwanza hadi asome masters ndio utakuwa muda muafaka kwake.
 
NK huwezi kujua, huyu awe mpole tu. Tatizo wanawake mnakimbilia kuachana na wapenz then later inakula kwenu au anapata mpenzi cheater zaidi.

May b jamaa amecheat kutokana na mzingira tu so kama amekiri tena kwa kulia machozi ni wazi hamtaki huyo mpenz wa nje.
So huyu atulie kwa muda apime then atoe uamuzi sahihi na sio kukurupuka tu.

Ni kawaida yake kulia akiwa ana makosa!
 
Nashukuru rafiki zangu kwa kunipa ushauri mzuri, nipo naifanyia kazia
 
uchumba miaka minne huku anacheat unaangaia? mwanaume ni yeye tu humu duniani? kusema kweli wanawake sisi ni maboya
kama mtu hasomeki achana nae
 
Piga chini huyo jamaa habebeki mwanaume gani unakuwa muongo muongo tu hata hiyo kujifanya analia ni wizi mtupu
 
quote_icon.png
By Mpatanishi

Pole sana, punguza mawazo. Na pia usichukue uamuz wa haraka. Tulia kwa muda muweke huyo mchumba mtegoni, mtege na umpime kama anaweza kubadilika. Ukiona anaweza endelea nae.

Hata hvyo naweza kusema na ww pia una tatizo, why uchumba tu miaka minne? Umesema una kazi nzuri na yeye pia sasa kipi kinachowafanya msioane? Sisemi muoane kama bado hamjawa tayari ila at least angekua mume wa ndoa ile security ingekuwepo na ungejua unambana vipi ila haya mambo ya uchumba tu na kuonjana mmh kazi ipo.
Mungu Akusaidie


By Evarm; Hapo kwenye rangi nyekundu, nimeshawahi kumuambia lakini alinijibu hayupo tayari kwanza hadi asome masters ndio utakuwa muda muafaka kwake.
Pole Evarm ndo ajari hizo kwenye mahusiano. Hapo kwenye Nyekundu kunanipa wasiwasi kidogo. Hiyo ni mipango ya kitoto kwa mtu anayekupenda. Hiyo masters ataisoma lini sasa alivyokwambia wewe na ndoa mtaifunga lini? Kuwa akiwa na mke hatoweza kusoma hiyo masters? Hana upendo wa kweli kwako ndo maana anaku-cheat, na hayo mambo ya kuendelea na shule ni sababu tu ya kuzidi kusongeza mda. Bado upo kwenye Portfolio yake anachunguza ni yupi anakidhi kiwango chake. Utakuja kuumia zaidi utakoposikia anatangaza ndoa kwa mwingine na wewe umekaa miaka 4 ukisubiri.

Hajakupenda kisawa sawa ndo maana hajatangaza ndoa. Funguka macho, japo ni maamuzi magumu kwa mtu uliyejitoa kwake. Lakini pia, huyo si mume bado ni ''Mchumba'' japo sijui kama hata kwenu alishakwenda kujitambulisha kama mchumba.



 
Ni mtu mzima ana miaka 29, anajua mema na mabaya, hata alipocheat alikuwa anajua anafanya nini.
Kuna watu hata huwasemehe vipi bado wataendelea kukucheat wanajifanya wanakuja na gia ya kulia ili uwasamehe kumbuka a cheater will always remain a cheater kama mmeisha kaa kwenye uchumba miaka minne na amekucheat kiasi hiki je akaishakufanya mkeo itakuwaje si ndio utaambulia na kipigo kabisa kutoka kwake. Tafakari kisha Chukua Hatua
 
Dada unapoteza tu muda kwa huyo cheater,Kiufupi ni kwamba ''he is not real into you''. Angekuwa amekuchagua wewe wala asingeliondoka the next day, angebaki aendelee kukubembeleza,ila inaonyesha amewahi kwenda kusawazisha kwa huyo mchumba waa pili.

We mmwage tena fast ili uwahi kupona haraka usonge mbele. Masters si kigezo hata chembe
 
Fuata moyo wako unakwambia nini, mapenzi yana shida zake na mojawapo ni hiyo ambayo imekupata na kama wewe ni muumuni wa mapenzi basi huna budi kuitatua na kuimaliza.

Ukitoka bila kuitatua basi hata safari yako nyingine ya mapenzi unaweza kujikuta unapata misukosuko ya namna nyingine na kutoka, mapenzi si raha tu kuna challenge zake na iliyokupata wewe ni mojawapo,kuna wengine ambao wakikusimulia yanayowatokea utajiona wewe ni afadhali mara milioni kuliko wao.

Pole sana na tafuta suluhisho la kudumu na mwenzi wako.
 
Kama kwenye uchumba ndio hivyo, mkioana tu utaona chamoto.
Kimbia kama bolt dada. Mungu atakujaalia utapata mwingine
 
Du pole sana mwaya,na hongera kwa uvumilivu,kwanza mapnz ya mbali huwa ni tatizo sn kwa baadhi ya wanaume hata km anakupenda vp lzm atachiti,pili uchumba miaka 4! kwa upande wangu hilo siwezi kuvumilia namwaga hata bila kosa hanifai yani anitumie miaka minne alafu bado anasema mda muafaka wa kufunga ndoa bado mpaka asome masters yani haki ya nani namwacha hata bila kosa!
Cha kufanya sikiliza moyo wako coz kuna wengine bwana wanajua kupenda hata na hawana uwezo wa kuacha hapo kazi kwako shost km una moyo wa zege hope utazoea kuchitiwa na hata akioa mwingine na kukuacha baada ya kukutumia vya kutosha hautaumia sn,ila km una moyo wa bigii km wangu yani tena mwenyewe mtu hata future yake haijui km huyobf wako lol siku nyingi nisha mpe red kadi,bota kuumia mara moja ukitulia nianze upya!
 
kwakweli nimesikitika sana pole my dear lakini me naona kutokana na maelezo yako ni msichana msomi na mwenye kazi nzuri ,mume wako wa kwanza ni kazi mamaa wacha kabisa kusikitika mapenzi yapo siku zote hujuhi mungu anakuhepushia nini na wewe unazidi kun'gang'ania wanaume wengi wa siku hizi ni vimeo wewe unaumia mwenzio akirudi dar anasawazisha anazidi kula bata .mawazo yanazeesha haraka jipende kwanza wewe kama wewe na ujue wewe ni wa thamani tena sana .kwa kweli mimi huwa ni mtata kweli kweli mwanaume ni kiona tu anadalili za kutoeleweka huwa huwa namtimua haraka na huwa hawaamini yanayotokeaga alafu huwa ninafanya gafla .na wanawake wengi wanaovumilia huo upuuzi wengi ni kutokana na dhiki na elimu duni .tujiulize tunapenda ili iweje FOR ME CHAKWANZA NIWE HAPPY IF NOT BYE BYE na hao niliowahi kuwaacha wengi wanajutia cause when yo have smthing gud kujua thamani yake ni ngumu sana mpaka kikiwa hakipo. huwa nawapaga pole na kuwahambia sirudiagi matapishi ilishanitokeaga kwa wanaume wangu wawili na huwa nashukuru mungu kila siku nazidi kuwa mrembo sura yenye furahaa maisha mazuri nini cha zaidi i concude by saying that you have to be strog na uwe ni mtu nini unahitaji kwenye maisha yako nafikiri fikiria zaidi kuwa mwanamke mwenye mafanikio more than getting stress and am very sure you will get a right man kama utakuwa makini kitu ambacho hakina future kama uko makini utakifahhamu tu mwanzoni. huyo gumegume muhache ataharibu maisha yako kabisa hasaa furahaa yako leave him usiwe limbukeni wa mapenzi utajutia kama utaendelea nae uwe tayari kusubiri mazito zaidi .maisha matamu mama asikwambie mtu ni kuishi kwa akili tu .
 
Pole sana dear,asikuumize kichwa huyo chukua maamuzi magumu achana nae.Ni heri uwe pekee na amani yako kuliko kuishi roho juu kumuwaza mwanaume ambaye huna hata ndoa nae.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom