Memtata
JF-Expert Member
- Jul 27, 2013
- 552
- 1,800
Habari wakuu,
Leo nakuja na shida yangu hii labda mnaweza kunishauri. Mke wangu hapendi kufanya tendo la ndoa kabisa.
Miezi kadhaa baada ya kuoana alipata ujauzito na tabia hii ndipo nilipoanza kuiona nikajua labda kwasababu ya ujauzito. Alipojifungua na kupumzika mambo ni yale yale, hatufanyi hadi nianze mimi na kuna wakati namuomba anasema hayuko vizuri siku hiyo inapita kavu.
Nimewahi kumuuliza kwanini hajisikii, hana jibu zaidi ya kujibaraguza tu na kuacha lipite. Mwanzo wa ndoa aliwahi kuanzisha kuomba game nadhani alikuwa anatimiza funzo la somo ila kwa sasa daah!... Yani nikikaa kimya mimi hata mwezi unaisha bila kufanya lolote.
Kuna wakati nahisi kama nambaka maana naomba omba kila wakati alafu mwenzangu hana muitikio. Hapa naandika uzi huu amejilaza mwenyewe hana habari wakati tangu jumapili niliomba mchezo akanambia yupo kwenye siku zake hadi leo hata hashtuki kwamba naweza kupata tamaa ya kuchepuka.
Najiuliza ndivyo alivyoumbwa, anachepuka, ana jini mahaba au anajichua? Maana kuna siku nilimuona kama anaweweseka kitandani niliponyanyuka akashtuka sana.
Naomba maoni yenu kiutuuzima bila kejeli tafadhali.