Mwenza wa ndoto yako

Mwenza wa ndoto yako

Umefanya kosa kubwa kujicommitte kwenye ndoa ilihali ulijua kabisa humpendi
Mungu akusaidie upate furaha yako ata kwa mambo mengine
Yani wewe?
Ina maana ndio ni kujikamit. Hutaki Ndoa ili ufanye Michezo gani ya siriiiiiiiiiii
 
Tatizo kila mtu anataka kuwa juu katika mahusiano, hakuna anayetaka kujishusha..ndoa ikishaingiliwa na huyo mdudu majivuno inakuwa mbaya kuliko..hebu jaribu kujishusha na kuwa muwazi kwake..japo kwa mara ya kwanza itakuwa ngumu na atashangaa ila ikizoeleka itakuwa ni ya kudumu na hakika furaha itarudi! Huyo ndio wa kwako kwa muda huu!
Kwa hilo niko makini katika kila sekta mkuu kuanzia chakula napika mwenyewe hata nichekewe kurudi, namfulia, nampasia nguo kila kazi nafanya mkuu lakini moyo mgumu kumkubali pia nahofia wazazi nao hawatanielewa nikiwaambia niondoke.

Mkuu mimi nimelelewa kwenye familia yenye maisha ya kawaida sana kabisa lakini yenye furaha sana na walikuwa wananipenda na kunijali karibia watu wote nyumbani kwetu wakubwa kwa wadogo. Walinipa ushirikiano sana hakuna nililoachwa linishinde. Nilikuwa kama kimalikia kidogo. Nikienda mahali nasindikizwa nikichelewa nafatwa na wote watanitafuta jambo ambalo huyu mwenzangu kashindwa kulitimiza anapuuzia na pengine hunambia unafikiri utabembelezwa kama kwenu haaaaa ni ndo nakereka. Ishanikaa ile hali ya kuchukuliwa kama princes nae ananichukulia PoA tu ,hata nikijisahau nikalala kwenye kochi nitashtuka usiku mwenyewe nipande kitandani nilale so kifupi naona kama hajali.
 
Mayoooo hizi ndoa hizi khaaaaa....kupata mwenza mnayeandana hata 50% imekuwa mtihani....pepa inayoitwa ndoa mhhhhhh haitabiriki!!!!
 
Yule ambaye alkuw wa kwanza na alkuwa na vigezo kwake.
Baada ya kuachana alibadilika mno na kuwa kicheche kwa vile wengi walitufahamu so nilikuwa napigiwa na kuniambia hadi sasa hajaweza kudumu na mke ni majanga mwendo wa kubadili wanawake. Wakimuuliza hao rafiki zake anadai mwanamke alikuwa ameweza kumfanya atulie ni mmoja tu yaani mimi wakiweza wampelekee ila mi sipo huko kabisa na wazazi wangu hawataki hata kusikia.
 
Kwa hilo niko makini katika kila sekta mkuu kuanzia chakula napika mwenyewe hata nichekewe kurudi, namfulia, nampasia nguo kila kazi nafanya mkuu lakini moyo mgumu kumkubali .

Mkuu mimi nimelelewa kwenye familia yenye maisha ya kawaida sana kabisa lakini yenye furaha sana na walikuwa wananipenda na kunijali karibia watu wote nyumbani kwetu wakubwa kwa wadogo. Walinipa ushirikiano sana hakuna nililoachwa linishinde. Nilikuwa kama kimalikia kidogo. Nikienda mahali nasindikizwa nikichelewa nafatwa na wote watanitafuta jambo ambalo huyu mwenzangu kashindwa kulitimiza anapuuzia na pengine hunambia unafikiri utabembelezwa kama kwenu haaaaa ni ndo nakereka. Ishanikaa ile hali ya kuchukuliwa kama princes nae ananichukulia PoA tu ,hata nikijisahau nikalala kwenye kochi nitashtuka usiku mwenyewe nipande kitandani nilale so kifupi naona kama hajali.
Mkuu hapo kazi ipo aisee..ila hakuna linaloshindikana chini ya jua hili! Endelea kumuomba Mungu atakusaidia!
 
Kiukweli haya mambo yapo ndugu..pole sana usiwaze ukadhani upo pekeyako.Wengi hatusemi sometimes it depend if u decided to keep it open ,katika mapenzi kuna wakati wa mapenzi saaana kwakila mmoja..Then after kama mnabahatika watoto mapenzi huhamia kwa watoto sana.Sasa hapo nihakili ya kilammoja kujua umuhim wa mwezake.Kunajambo ambalo huwa nigum kidogo kwakila mmoja kukumbuka mapenzi ya awali.Lkn hili kwa uchunguzi binafsi ni mmoja kati yenu kuamua kutokuwa muwazi na kuamua kuishi kwa mazoea.
 
Kitu nilichojifunza ni kwamba mara nyingi mwanaume asipokupenda ni hatokupenda milele, sio Ndoa wala watoto watakaomfanya akupende. Mwanaume hana cha kujifunza kupenda kama wanawake wengi tulivyo. Ukiona mwanaume hakupendi na hamjafunga ndoa, please muache tu aende. Hakuna kitu kibaya kama kufunga ndoa na mtu who can't love and appreciates you. Wanawake wengi ndo wanaishiaga kuwa na vichaa vya ndoa, maana ataanza na kuwa insecure, muda wote atahisi kuna mtu huko nje anayekuzuzua, hata kama hayupo, ugomvi hautoisha. Hakuna adhabu mbaya kama kuishi na mtu asiyekuappreciate.
Uko vizuri upstairs..

Kudos..[emoji122] [emoji122] [emoji122]
 
Then yupo makini huyo, post yake haijaweka wazi jinsia zao hata mara moja. Nikaingia chaka lol

Kweli mkuu huwa sipendi kuongeza matatizo lakini kwa kuwa jamii yangu inaona hakuna shida kwetu ndo nikajaribu kupata mawazo ya watu baki nitafakari. Naumia moyoni nimepoteza furaha yangu ya utotoni niliyozoea.
 
Uko sawa mkuu,
Halafu kuna ile kabla ya ndoa mchumba anataka kujionyesha kwa kila mtu kwamba yuko nawe na anakupenda na atakufata kila ulipo. Hivyo baada ya miezi kadhaa marafiki na jamii inamtambua.
Nao wanaanza upambe hivyo hata kama humpendi kuna ile kumuonea aibu ukimuacha jamii itakuelewaje naye kesha jiwahi huko na kama kuna ile roho ya uungwana kidogo kuna ile kumfikiria ataichukuliaje hiyo hali ya kuachwa. Hivyo inabidi tu kumfichia heshima kwa Mungu na jamii. Ndicho kilichonikumba na kunifikisha katika hali hii kwani hakuna ambaye angeweza kunielewa kwamba moyo wangu umekataa kabisa kumpokea naye alijipa matumaini iko siku nitampenda lkn bado haijafika hiyo siku.
Hivi we ni Me or Me?

Napata shida kung'amua jinsia yako
 
Kweli mkuu huwa sipendi kuongeza matatizo lakini kwa kuwa jamii yangu inaona hakuna shida kwetu ndo nikajaribu kupata mawazo ya watu baki nitafakari. Naumia moyoni nimepoteza furaha yangu ya utotoni niliyozoea.
Yani sina hata cha kusema, zaidi ya kukupa pole tu ndugu yangu.
 
Haya Mambo hayaaaa...

Yasikie kwa Jirani tuuu...
 
pole sana
ila mkubali pamoja na mapungufu yake ila kwa kweli mahusiano kukosa mawasiliano kiasi hicho ni hatari
fanya sana ibada mueke Mungu mbele atawaonesha njia na kuwapa furaha
ushinde upweke kwa kumweka Mungu karibu yako
 
Haya mahusiano ya kimapenzi ni very complex (Jambo gum sana).Kwa sababu;
1.Unaeza ukawa unajali na ukaonekana kimbele mbele.
2.Unaeza ukawa kimya ukaambiwa hujali.
3.Akiridhika na personality yako ataleta kutokuridhika kitandani.
4.Ukifaulu personality na sex uchumi utaangaliwa. 5.Body structure ikibadlika nalo ni tatizo.
Nimejarbu kutafakari
Nilichogundua ni vigum sana binadamu kuridhika mara moja na Kwa wakati wote.Akikupenda Leo kesho atakufanyia comparison(Ulinganifu) na wengine Kwa hio bado atabadilika, Ukitaka maisha ya raha usiwe bize sana na mapenzi maana Binadamu hua haridhiki kamwe hadi anakufa
 
omba Mungu kama wewe ni mkristo simama kwenye neno la Mungu mithali 19:14 na ninachojua Mungu hulitazama neno lake akapate kulitimiza isaya 55:10-11 isaya amemthibitisha Mungu kuwa neno lake halitamrudia bure mpaka lifanye lile kusudi ambalo Mungu amelinene na kusudi la Mungu katika kitabu cha mithali nikukupatia mke au mume mwema ninachojua kila chema hutafutwa kwa gharama nawe tumia gharama ya magoti kumuomba Mungu mke au mume kwani ni ahadi yetu kwa Mungu kuwa atatupatia acha kukata tamaa dai haki yako mbele za Mungu.
Ahsante mkuu hadi misa ya asubuhi sikosi ila sijawahi mwambia hata Padre yanayonisibu na siwezi mwambia kwani kwa kadiri atujuavyo hatoamini atajua namtega. Hata Mwenyekiti wa kigagwe nitaanzaje kumwambia si ataniona mzizi huenda.
 
Back
Top Bottom