NUCLEAR BOMB
JF-Expert Member
- Jan 23, 2017
- 342
- 323
Habarini za usiku wakuu.
Wakati wa Ujana kuna zile ndoto huwa tunakuwa nazo juu ya wenza tunaotaka kuwa nao maishani iwe kwa Msichana au Mvulana.
Lakini katika Safari hiyo ndefu ya kuelekea ukubwani tunapitia changamoto nyingi ambazo kwa namna moja au nyingine huzima ndoto zetu na kujikuta tunaingia katika mahusiano na watu ambao siyo wa mioyo yetu kwa kurubuniwa na mazingira mbalimbali.
Binafsi nilitaraji kupata mwenza mchangamfu, rafiki, anayenifanya nitabasamu muda wote, anayejua nafasi yake katika familia, anayejua nimekula nini au nafanya nini yaani kifupi mtu anayajali na kutengeneza mahusiano rafiki, muwazi wa hisia na mjasiri. Kuhusu muonekano hapo naweka kapuni.
Wakati fulani katika maisha nilipata wa hivyo tunaefanana tabia tukafurahia mahusiano hadi ndugu na marafiki zetu walitupenda na tulikuwa na furaha tele kila mtu alipendwa kwa mwenzake coz hata muonekano wetu tulikuwa tunaendana sote majiyakunde yeye mrefu mi mfupi. Maisha yakabadilika kutokana na umbali akanisaliti kwa mtu wa jirani yetu sikuweza kusamehe nikajitenga nae ingawa aliniomba sana nimsamehe lakini moyo ulikataa na nikausikiliza. Akawa kama mwehu alitangatanga na wapenzi wa kila rika mi nilitulia kwa vile sipendi tabia ya kubadilisha wapenzi nilijipa muda isitoshe nilikuwa mbali nae.
Baada ya mwaka kupita nikaona nipate wangu cha ajabu macho yakakataa kuona wengi nikaona mmoja akajionesha kama ana utu ila alikuwa tofauti na vigezo vyangu nilimweka wazi kwamba hanivutii akanimbia naweza kujifunza kupenda sikumpa jibu akaniseduce vya kutosha ikabidi nifungue moyo. Cha ajabu tangu ndoa day one hadi leo zaidi ya miaka saba sijawahi kuwa na furaha nae.
Kila mtu kivyake tukutane kitandani furaha kwa nadra na wala sichepuki akisafiri anaweza wapigia simu wengine ila mi hata akae miezi mitatu hapigi simu na wala simpigii au kumlaumu kwani hata akinipigia sauti yake hainisisimui hivyo nachukia , kukiwa na lolote namtumia text mesage akijisikia atajibu. Hata akiwa online WhatsApp hatuwezi kuchati nae hata nikimtumia sms hajibu hadi siku akirudi ndo tuonane. Imekuwa ndiyo mfumo wa maisha yetu na Kuzima ndoto ya Maisha ya furaha niliyokuwa nayo na niliyolelewa.
Mara nyingi napenda kukaa peke yangu sipendi kelele na hata sipendi kupiga simu ndugu na marafiki wananilaumu, sipendi kwenda kwenye starehe na nikienda nailazimisha tu furaha. Ingawa kila kitu changu kinaenda sawa.
Hivyo leo nikapenda nipate kujua kama nyie wenzangu mlifanikiwa kupata Wenza wa ndoto zenu au wa Mioyo yenu? Kama ndiyo hongera na Kama siyo umewezaje kuishi na huyo ulonaye kwa Sasa? Karibu tupeane uzoefu.