Mwenza wa ndoto yako

Mwenza wa ndoto yako

Uko sawa mkuu,
Halafu kuna ile kabla ya ndoa mchumba anataka kujionyesha kwa kila mtu kwamba yuko nawe na anakupenda na atakufata kila ulipo. Hivyo baada ya miezi kadhaa marafiki na jamii inamtambua.
Nao wanaanza upambe hivyo hata kama humpendi kuna ile kumuonea aibu ukimuacha jamii itakuelewaje naye kesha jiwahi huko na kama kuna ile roho ya uungwana kidogo kuna ile kumfikiria ataichukuliaje hiyo hali ya kuachwa. Hivyo inabidi tu kumfichia heshima kwa Mungu na jamii. Ndicho kilichonikumba na kunifikisha katika hali hii kwani hakuna ambaye angeweza kunielewa kwamba moyo wangu umekataa kabisa kumpokea naye alijipa matumaini iko siku nitampenda lkn bado haijafika hiyo siku.
Ujue hata maandiko matakatifu yameandika "mpende jirani yako", hayajasema "mu-impress jirani yako". Wengi wetu tunashindwa kufanya vitu ambavyo tunaona vina faida kwetu, simply because watanionaje. Maisha ni yako, usiyapoishi vile unavyotaka wewe, hakuna atakayekusaidia kuyaishi
It's high time tuanze kujisimamia juu ya vile tunavyovihitaji, instead of kuangalia judgements za watu.

Hakunaga mapenzi ya huruma hata siku moja. Ukishindwa kupata hata sababu moja ya kuwa na mtu, muache tu aende. Huko mbeleni mtajuta tu na situation itakuwa complicated zaidi mkishakuwa na watoto. You couldn't leave her mkiwa wachumba, utaweza kumuacha leo akiwa mke na mna watoto tayari? Ile huruma yako imekusaidia nini? Wale uliotaka kuwaimpress wanaishi maisha yao happily, ilihali wewe kwako kila leo ni afadhali ya jana. Wa kukupa furaha ni wewe mwenyewe kwanza, na furaha haipatikani kwa kuwafurahisha wengine ilhali moyoni unaumia. Better kuvunja uchumba, kuliko kuvunja ndoa. Anyway, pole sana
 
Pole mkuu naelewa unachopitia.usifeel guilty kwa kutafuta furaha yako.vitisho vyake vya kujiua na mengineyo visikufanye ukagive up furaha yako. Hiyo ndoa inawaumiza nyote wawili bora muivunje tu.
Many people exist but don't live nanyie unaweza kuwa mna exist tu.
 
Habarini za usiku wakuu.

Wakati wa Ujana kuna zile ndoto huwa tunakuwa nazo juu ya wenza tunaotaka kuwa nao maishani iwe kwa Msichana au Mvulana.

Lakini katika Safari hiyo ndefu ya kuelekea ukubwani tunapitia changamoto nyingi ambazo kwa namna moja au nyingine huzima ndoto zetu na kujikuta tunaingia katika mahusiano na watu ambao siyo wa mioyo yetu kwa kurubuniwa na mazingira mbalimbali.

Binafsi nilitaraji kupata mwenza mchangamfu, rafiki, anayenifanya nitabasamu muda wote, anayejua nafasi yake katika familia, anayejua nimekula nini au nafanya nini yaani kifupi mtu anayajali na kutengeneza mahusiano rafiki, muwazi wa hisia na mjasiri. Kuhusu muonekano hapo naweka kapuni.

Wakati fulani katika maisha nilipata wa hivyo tunaefanana tabia tukafurahia mahusiano hadi ndugu na marafiki zetu walitupenda na tulikuwa na furaha tele kila mtu alipendwa kwa mwenzake coz hata muonekano wetu tulikuwa tunaendana sote majiyakunde yeye mrefu mi mfupi. Maisha yakabadilika kutokana na umbali akanisaliti kwa mtu wa jirani yetu sikuweza kusamehe nikajitenga nae ingawa aliniomba sana nimsamehe lakini moyo ulikataa na nikausikiliza. Akawa kama mwehu alitangatanga na wapenzi wa kila rika mi nilitulia kwa vile sipendi tabia ya kubadilisha wapenzi nilijipa muda isitoshe nilikuwa mbali nae.

Baada ya mwaka kupita nikaona nipate wangu cha ajabu macho yakakataa kuona wengi nikaona mmoja akajionesha kama ana utu ila alikuwa tofauti na vigezo vyangu nilimweka wazi kwamba hanivutii akanimbia naweza kujifunza kupenda sikumpa jibu akaniseduce vya kutosha ikabidi nifungue moyo. Cha ajabu tangu ndoa day one hadi leo zaidi ya miaka saba sijawahi kuwa na furaha nae.
Kila mtu kivyake tukutane kitandani furaha kwa nadra na wala sichepuki akisafiri anaweza wapigia simu wengine ila mi hata akae miezi mitatu hapigi simu na wala simpigii au kumlaumu kwani hata akinipigia sauti yake hainisisimui hivyo nachukia , kukiwa na lolote namtumia text mesage akijisikia atajibu. Hata akiwa online WhatsApp hatuwezi kuchati nae hata nikimtumia sms hajibu hadi siku akirudi ndo tuonane. Imekuwa ndiyo mfumo wa maisha yetu na Kuzima ndoto ya Maisha ya furaha niliyokuwa nayo na niliyolelewa.

Mara nyingi napenda kukaa peke yangu sipendi kelele na hata sipendi kupiga simu ndugu na marafiki wananilaumu, sipendi kwenda kwenye starehe na nikienda nailazimisha tu furaha. Ingawa kila kitu changu kinaenda sawa.

Hivyo leo nikapenda nipate kujua kama nyie wenzangu mlifanikiwa kupata Wenza wa ndoto zenu au wa Mioyo yenu? Kama ndiyo hongera na Kama siyo umewezaje kuishi na huyo ulonaye kwa Sasa? Karibu tupeane uzoefu.
Daaaaaahh pole sana Broo Mungu akusaidie kwa hayo unayoyapitia.
 
Salute to you brother, umeonyesha ukomavu wa hali ya juu sana, maisha ya ndoa mostly ni convenience, kuwa na mwenza ambaye mnaweza mkafanya maisha na mkazaa na kuwalea watoto vizuri wakasimama kama watu. Mapenzi na furaha ni sehemu pia ya ndoa, yes hili liko wazi, ila one thing for sure at times when there is no perfect moment, you take the moment and make it perfect. Usitumie muda mwingi sana kufikiri kuhusu historia, huyo uliyenae unatakiwa kumfanya akupe furaha na wewe umpe furaha. Zungumzeni kwa uwazi maisha yatakua mazuri tu.
 
Nimekata tamaa Mkuu.
Sijui kama nitaoa.
omba Mungu kama wewe ni mkristo simama kwenye neno la Mungu mithali 19:14 na ninachojua Mungu hulitazama neno lake akapate kulitimiza isaya 55:10-11 isaya amemthibitisha Mungu kuwa neno lake halitamrudia bure mpaka lifanye lile kusudi ambalo Mungu amelinene na kusudi la Mungu katika kitabu cha mithali nikukupatia mke au mume mwema ninachojua kila chema hutafutwa kwa gharama nawe tumia gharama ya magoti kumuomba Mungu mke au mume kwani ni ahadi yetu kwa Mungu kuwa atatupatia acha kukata tamaa dai haki yako mbele za Mungu.
 
Pole sana kaka, Mimi ninakishauri uvumilie tu, kwa sababu ndoa tayari imeshafungwa, japo huna mapenzi nae lakini kama hakusumbui hakuna shida, kwa mfana kama siyo Malaya, anawapenda wazazi wako na ndugu zako nk. Kwa upande wangu naona huo ndo msalaba wako inakubidi uubebe mpaka mwisho, usitafute mwanamke mwigine wa pembeni au kumwacha huyu ulienae kwan unaweza kujitafutia majanga mengine.
 
Kitu nilichojifunza ni kwamba mara nyingi mwanaume asipokupenda ni hatokupenda milele, sio Ndoa wala watoto watakaomfanya akupende. Mwanaume hana cha kujifunza kupenda kama wanawake wengi tulivyo. Ukiona mwanaume hakupendi na hamjafunga ndoa, please muache tu aende. Hakuna kitu kibaya kama kufunga ndoa na mtu who can't love and appreciates you. Wanawake wengi ndo wanaishiaga kuwa na vichaa vya ndoa, maana ataanza na kuwa insecure, muda wote atahisi kuna mtu huko nje anayekuzuzua, hata kama hayupo, ugomvi hautoisha. Hakuna adhabu mbaya kama kuishi na mtu asiyekuappreciate.
Ndiyo maana unaambiwa mwanaume hupenda na mwanamke hupendwa. Hapo ndoa inadumu ila ikiwa kinyume ni hatari tupu
 
learn how to love.. anza kufocus na mazuri yake , angalia vitu gani mpo common , ukishavijua anza kuishi maisha ya kawaida na uache formality ,, tatizo mkiolewa mnahisi hulka zenu zinakufa au kuna maisha tofauti unatakiwa kuishi ni noo.. ishi maisha yako be free open .. yani unamaisha magumu sana aisee
 
Uko sawa mkuu,
Halafu kuna ile kabla ya ndoa mchumba anataka kujionyesha kwa kila mtu kwamba yuko nawe na anakupenda na atakufata kila ulipo. Hivyo baada ya miezi kadhaa marafiki na jamii inamtambua.
Nao wanaanza upambe hivyo hata kama humpendi kuna ile kumuonea aibu ukimuacha jamii itakuelewaje naye kesha jiwahi huko na kama kuna ile roho ya uungwana kidogo kuna ile kumfikiria ataichukuliaje hiyo hali ya kuachwa. Hivyo inabidi tu kumfichia heshima kwa Mungu na jamii. Ndicho kilichonikumba na kunifikisha katika hali hii kwani hakuna ambaye angeweza kunielewa kwamba moyo wangu umekataa kabisa kumpokea naye alijipa matumaini iko siku nitampenda lkn bado haijafika hiyo siku.
duh pole na anza kumpenda
 
Ujue hata maandiko matakatifu yameandika "mpende jirani yako", hayajasema "mu-impress jirani yako". Wengi wetu tunashindwa kufanya vitu ambavyo tunaona vina faida kwetu, simply because watanionaje. Maisha ni yako, usiyapoishi vile unavyotaka wewe, hakuna atakayekusaidia kuyaishi
It's high time tuanze kujisimamia juu ya vile tunavyovihitaji, instead of kuangalia judgements za watu.

Hakunaga mapenzi ya huruma hata siku moja. Ukishindwa kupata hata sababu moja ya kuwa na mtu, muache tu aende. Huko mbeleni mtajuta tu na situation itakuwa complicated zaidi mkishakuwa na watoto. You couldn't leave her mkiwa wachumba, utaweza kumuacha leo akiwa mke na mna watoto tayari? Ile huruma yako imekusaidia nini? Wale uliotaka kuwaimpress wanaishi maisha yao happily, ilihali wewe kwako kila leo ni afadhali ya jana. Wa kukupa furaha ni wewe mwenyewe kwanza, na furaha haipatikani kwa kuwafurahisha wengine ilhali moyoni unaumia. Better kuvunja uchumba, kuliko kuvunja ndoa. Anyway, pole sana
nimeacha wanaume wawili na nilikuwa nafahamika kwao na baadhi ya ndugu kwangu wala sikuona tabu kuwaacha wanakatabia cha kuridhika na uvivu mi siwezi ... nikaona nikifika huko mbele nitawatafuna bure bora niachane nao
 
Pole mkuu naelewa unachopitia.usifeel guilty kwa kutafuta furaha yako.vitisho vyake vya kujiua na mengineyo visikufanye ukagive up furaha yako. Hiyo ndoa inawaumiza nyote wawili bora muivunje tu.
Many people exist but don't live nanyie unaweza kuwa mna exist tu.
Kuvunja ndoa kiubinadamu ni sawa na kuua ndugu zangu. Ajifunze kumpenda hakuna jinsi hata sie katika ndoa mambo ni hayo hayo
 
Salute to you brother, umeonyesha ukomavu wa hali ya juu sana, maisha ya ndoa mostly ni convenience, kuwa na mwenza ambaye mnaweza mkafanya maisha na mkazaa na kuwalea watoto vizuri wakasimama kama watu. Mapenzi na furaha ni sehemu pia ya ndoa, yes hili liko wazi, ila one thing for sure at times when there is no perfect moment, you take the moment and make it perfect. Usitumie muda mwingi sana kufikiri kuhusu historia, huyo uliyenae unatakiwa kumfanya akupe furaha na wewe umpe furaha. Zungumzeni kwa uwazi maisha yatakua mazuri tu.
huyu ni dada mbona
 
nimeacha wanaume wawili na nilikuwa nafahamika kwao na baadhi ya ndugu kwangu wala sikuona tabu kuwaacha wanakatabia cha kuridhika na uvivu mi siwezi ... nikaona nikifika huko mbele nitawatafuna bure bora niachane nao
Haya mambo ya watanionaje, me sina kwa kweli. Hata kama ndoa imekaribia, nikiona kuna mambo yameshindikana, better kila mtu ashike njia yake tu. Kisa cha kuspend the rest of your life unagugumia na kununa ni nini?
 
Duniani kila mtu na bahati yake,,,,,huenda bahati yako bado haijafika
 
Haya mambo ya watanionaje, me sina kwa kweli. Hata kama ndoa imekaribia, nikiona kuna mambo yameshindikana, better kila mtu ashike njia yake tu. Kisa cha kuspend the rest of your life unagugumia na kununa ni nini?
na presha juu ufe mapema hapana hata mi siwezi
 
Back
Top Bottom